Ushauri kwa CHADEMA: Japo ni Haki, lakini chondechonde Msiandamane. Mwenye Nguvu Mpishe!

Mkuu Danny, nakubaliana na wewe, dawa ya adui sii kumkimbia au kumpisha bali kukabiliana nae, na hata kama utaangamia katika kukabiliana huko, na kupoteza maisha, jina lako ndilo litabaki kama shujaa, cha muhimu cha kujiuliza, ni nani muhimu zaidi kati ya shujaa mfu, au mfungwa hai aliye gerezani?!, au aliyejificha mwituni?!.

Kwa maoni yangu, kama unakiona kifo kile, halafu unakikimbilia na kufa tuu ili uonekane shujaa, wewe ni shujaa mjinga!. Kama unataka kushindana au kupigana na mtu mwenye nguvu zaidi yako, hivyo unaingia kwenye mapambano ili hali unajua utawawa, wewe pia ni shujaa mjinga!. Shujaa mwerevu ni yule ambaye hawezi kuingia kwenye vita ambayo anajua atashindwa!, bali atampisha huyo mwenye nguvu, huku yeye akijijenga mpaka awe na nguvu za kukabiliana na kushinda!.

Naomba take time kasome bandiko langu hili, utanielewa ninamaanisha nini
Tuko Vitani Tuna Wapiganaji Shupavu, Wapiganaji Makini na ...

Pasco
 
Mkuu Kitaturu, kuna siasa za aina tatu, siasa za maendeleo, (developmental politics), siasa za kujifurahisha (politics of politiking), na kuna siasa za migogoro, (politics of confrontation).

1. Siasa za Maendeleo.
Hizi ni siasa zenye malengo ya kuleta mabadiliko chanya, changing for the better. Kila political move unayofanya, ila malengo chanya ya kuleta mabadiliko, siasa hizi zimefundishwa sana na Mwalimu Nyerere katika kitabu chake cha Binadamu na Maendeleo. Siasa hizi ni siasa zenye sera, ilani, malengo, mikakati na time frame, hizi mimi naziita SMART Politics, ni siasa zenye
S - specific, significant, stretching
M - measurable, meaningful, motivational
A - agreed upon, attainable, achievable, acceptable, action-oriented
R - realistic, relevant, reasonable, rewarding, results-oriented
T - time-based, time-bound, timely, tangible, trackable

2. Siasa za Kujifurahisha.
Hizi ni kauli za kisiasa kwa ajili ya kujifurahisha tuu to gain political mileage lakini hakuna chochote kinachofanyika, hizi zinajumlisha ahadi zisizotekeleka, hizi ni politiking, mtu unazungumza ili tuu uonekane na wewe upo upo. Kwenye kundi hili, zile siasa za bendera fuata upepo pia zimo kwenye kundi hili. Hizi ni siasa ambazo hazina maana yoyote kwa maendeleo!, huku ndiko siasa za fitna, majungu, uongo, zengwe etc, etc.

3. Siasa na Migogoro
Hizi naziita ni siasa za attention seeking, yaani kupinga tuu kila kitu ili tuu kuonekana na kutafuta public sympathy, lakini hizo moves hazina faida yoyote wala manufaa yoyote ya maana!. Hapa ndio pale watu wanapinga kila kitu hata kile chenye manufaa kwao kwa lengo la kutafuta tuu mgogoro. Siasa hizi hufanywa sana kwa mikutano ya hadhaa na maandamano ambayo hayana manufaa yoyote!.

Mfano hai ni hii kampeni ya UKUTA!, Rais Magufuli ambaye kweli ni dikiteta, amevunja katiba kwa kupiga marufuku maandamano na mikutano ya hadhara kinyume cha katiba!. Chadema wanasema wao wataandamana na kufanya mikutano nchi nzima!. Lengo la mikutano hii na maandamano wameiita kupinga udikiteta nchini!. Sasa kitakachofanyika kwenye mikutano hiyo na maandamano ni mabango na kauli chonganishi kuupinga udikiteta ili wananchi waone Chadema inapinga udikiteta wa Magufuli!. Kupinga huku ni kwa kujifurahisha tuu, kwa sababu hakutabadilisha lolote wala chochote katika udikiteta wa Magufuli, sana sana Magufuli atawatandika tena kwa kutumia "za moto" japo taarifa ya polisi itasema ni rubber bullets, na miili ya baadhi ya wataotandikwa, itachukuliwa na polisi na ku vanish into thin air!, hakuna atakayejua nini kiliwasibu!.

SMART politics kwenye kuupinga udikiteta wa Magufuli, ni kwa kutumia katiba na sheria, imeeleza wazi nini kinachotakiwa kufanywa pale kiongozi aliyeapa kuilinda katiba, akawa ndie wa kwanza kuivunja hiyo katiba!. Mikutano ya hadharra na maandamano sio njia sahihi ya kudeal na udikiteta wa mkuu wa nchi, haswa ukizingatia dikiteta mwenyewe, ni dikiteta mzalendo!, hicho anachofanya rais Magufuli, ndicho wananchi wanachotaka na ndicho kinachoweza kufanyika kututoa hapa tulipo, na kutufikisha kule tunakotaka kwenda!.

Kama ulifuatilia ule mkutano wa Chadema wa Mwembe Yanga, ulioitangaza list of shame, Katibu Mkuu wa Chadema na viongozi wote walikuwa wakali sana kuhusu rushwa na ufisadi, huku wakiendesha siasa za uanaharakati. Miongoni mwa sala za wanahaakati ni kumuomba Mungu, atupatie rais dikiteta mwenye uwezo wa kudeal na rushwa na ufisadi!. Mungu katusikia sala zetu, katupatia rais dikitate kweli, John Pombe Magufuli!, sasa wale wale waliokuwa wakipinga rushwa na ufisadi, sasa ndio wamewakumbatia mafisadi wale wale wa kwenye list of shame na sasa ndio wanaopiga kelele kulaani rais dikiteta!.

Pasco
 
Chonde Chonde ndugu zetu wa Chadema, ili chama chenu kifanikiwe, ni lazima sana mjifunze kubadilika na wakati!, sasa tuko kwenye wakati tofauti, JK alikuwa ni mtu wa mchezo na kiukweli, tulimchezea sana!. Magufuli sio mtu wa mchezo mchezo, huyu ni mtu wa kazi tuu!, hataki mchezo!. Sasa Chadema pia ibadilike ifanye kazi ya siasa na sio kuendelea kucheza michezo ya siasa!, jamaa hataki mchezo!, nasisitiza wito wangu humu, msishindane na mwenye nguvu!, mwenye nguvu mpishe!.

Pasco
 
THEN KWA KIFUPI PASCO HAKUNA HAJA YA VYAMA VINGI UNTIL 2020
Vyama vingi ni wakati wa uchaguzi au uchaguzi mdogo, uchaguzi ukiishaisha sasa ni wakati wa kufanya kazi, kazi tuu!.

Pasco
 
Kwa maneno yako,nchi nyingi leo zisingekuwa huru!Kuna watu walienda kupigana Vita wakijua hawatapona lakini uhuru utapatikana!
 
Vyama vingi ni wakati wa uchaguzi au uchaguzi mdogo, uchaguzi ukiishaisha sasa ni wakati wa kufanya kazi, kazi tuu!.

Pasco
Pasco mwaka 2025 jamaa akiamua atagombea tena kwa mabavu na kuvunja katiba,tutulie tu!Akishindwa akajitangaza mshindi tutulie tu kisa mkubwa ana jeshi?
 
Ni kweli kabisa Pasco kuwa Rais wetu ni Dikteta!! Lakini ni dikteta ambaye hataki kuitwa dikteta!!.
Mengi sana tutayaona!!
Pasco unasema jamaa wasiandamane je wafanye nini ili uhuru huu na haki wanayopigania vipatikane!!!!!????
 
Pasco anatumika vibaya sana sijui ni kwa hicho kibarua anachopewa?
Mkuu , Pasco wa jf ni independent, hatumwi na mtu!, hivyo situmiki vibaya kwa sababu situmwi na yeyote!. Labda useme najitumia vibaya!.

Pasco
 
Ushauri umefika!!
 
Ritz ni bora Ben ateswe mpaka kufa kuliko afe kwa ngoma alafu tuone aibu kusema marahemu hakuvaa condom
 
Naona Maelezo yako Pasco hayajakata kiu,umepita juu juu tu ukikwepa swali la msingi!Mpaka ikafikia wananchi wakataka mabadiliko hata wagombea wote wakaimba mabadiliko ni kutokana na mambo kwenda hovyo awamu ya 4!Wananchi walijua udhaifu huo wa serikali kupitia hasa kwa wapinzani hasa CDM ambao walifanya mikutano kuwaamsha wananchi!Nakumbuka Zitto aliingia matatizoni ikiwa kufungiwa ubunge kwa miezi 5 alipoibua sakata la buzwagi na mirahaba,Dr slaa alichachamaa kukosoa serikali hasa kwa ufisadi!Ni kwa mambo hayo wananchi wakaona wanahitaji mabadiliko!Kama JK angekuwa Dikteta kama JPM angeweza kuwazuia kina Dr slaa na wapinzani kwa kuzuia mikutano yao na kuwachapa risasi pale wanapokaidi!Na nina uhakika hilo lingefanyika wananchi wasingejua uovu wa serikali!Kwahiyo movement zile ziliwaamsha watanzania!Impact yake ikaonekana kwenye uchaguzi baada ya kuwa na mchuano mkali!
Siasa unayofanya Leo sio lazima ikupe matokeo papo kwa papo!Unaweza Fanya jambo leo lakini ukategemea results hapo baadaye kama mtawala hatojirekebisha!So unaposema Ukuta haina impact unajidanganya au huna uelewa wa kutosha!Movement hiyo itawapa awareness wananchi juu ya nini kinaendelea na kuwapa tahadhari ya kuwa na viongozi wa namna hiyo!Nkirunzinza alianza taratibu,akanogewa sasa anang'ang'ania madaraka!Hii inaweza kuwajenga kwa ajili ya uchaguzi ujao!
 
Pasco mwaka 2025 jamaa akiamua atagombea tena kwa mabavu na kuvunja katiba,tutulie tu!Akishindwa akajitangaza mshindi tutulie tu kisa mkubwa ana jeshi?
Mkuu Bomee, kama katiba yetu inasema mwisho ni vipindi viwili, mwisho ni vipindi viwili, ni kichaa tuu pekee anayeweza kuona mwisho ni vipindi viwili, akataka kugombea kipindia cha tatu!.

Ila pia katiba sio Biblia au Msahafu, inaweza kubadilishwa wakati wowote!, katiba ni yetu sisi Watanzania kwa ajili yetu, tukimuona Magufuli ni mzuri sana, na taifa bado linamuhitaji, tutaibadili katiba, kukiondoa hicho kipengele cha mwisho ni vipindi viwili vya miaka 5 mitano, na badala yake, tuweke mwisho vipindi viwili vya miaka 10 kumi!, tena kwa uzoefu hakuna rais amewahi kutumikia kipindi kimoja tuu, lazima vitimie viwili, then tunaweza kabisa kuamua 2020 hakuna haja ya uchaguzi wa rais, ni wastage of time, money na resources, Magufuli anatosha!, na baada ya hapo tukaamua endelee, kuna ubaya gani?!.

Nisome hapa
Kwa Kasi hii ya Magufuli, kuna haja Kufanya Uchaguzi wa Rais 2020 ...

Pasco
 
Kwa hali hii waandishi kuna haja ya kuangaliwa upya taaluma zenu au mfumo wa upatikanaji elimu yenu!Si bure,kuna tatizo sehemu!
 
Kwa hali hii waandishi kuna haja ya kuangaliwa upya taaluma zenu au mfumo wa upatikanaji elimu yenu!Si bure,kuna tatizo sehemu!
Hakuna tatizo lolote, sifa ya kuwa mwandishi ni kujua tuu kusoma na kuandika!, mimi elimu yangu ni daasa la saba la UPE na nilipasi ili sikuchaguliwa kuendelea na masomo ya sekondari!. Kuwa mwandishi hukitaji elimu yoyote zaidi ya kujua kuandika!. Tatizo ni nini?!, niliposema katiba sio Msahafu, tuibadili kutoka vipindi 2 ya miaka 5 hadi vipindi 2 vya miaka 10?!.

Pasco
 
Mkuu Pasco!
Kwani itakuwa ni Kuandamana nchi nzima au Kuandamana kuelekea wapi na kwa nani alafu ili iweje?
Isije ikawa unafahamu/umeelezwa mbinu ya kuandamana, kumbe maana ikawa nyingine kabisa.
Binafsi nauona ufisadi unaofanywa na wanasiasa kuilazimisha serikali kutumia gharama kulinda Amani ya nchi.
Kwa muktada huo watu watapigwa kwa kodi zao na huku wengine wakilipwa kwa kodi zao na wengine kufurahia kuzidi kuaminiwa na wakubwa /wafadhili wao.
Siasa ni mchezo hatari unaotumia watu kama ngao dhidi ya wengine ili wachache wafurahi na wengi watakaofurahi ni lazima jasho liwatoke.
Aisee ni hatari sana!
 
Kama katiba inaweza badilishwa ili kukidhi. haja za mtu fulani aweze kuendelea kuongoza tutakuwa tunajenga picha gani kwa viongozi wa bàadaye?Huoni kuwa kuna risk ya kumwaga damu kama Burundi?Namaanisha siku tukipata Rais ambaye ameshaona hayo yanawezekana si anaweza tumia nguvu yake kijeshi na kupeleka katiba bungeni ibadilishwe!Hawezi shindwa hasa akiwa na wabunge wengi!Hata kura ya maoni atatumia power yake kubatilisha kama mambo yakienda kombo!Mambo haya sio yakufanyia mzaha Pasco,hasa kwa mtu wa taaluma yako!
 
Bomee, kwani kuna first and hard rules utawala uwe ni miaka mitano mitano? . Mbona Marekani ni miaka 4 tuu? na Uingereza ni miaka 6?. Nimekupa froof kuwa hakuna rais wa Tanzania aliyekaa miaka 5 tuu, hivyo tunaweza kuamua vipindi vyetu viwe ni miaka 10! .

Katiba ni yetu na sio Msahafu hivyo ni rucksa kuibatilisha wakati wowote wa hitaji la mabadiliko! .

Pasco
 
Unachembechembe za mwanamke sio bure....nmerudia kuusoma huu uzi kutokan na kuanzisha uzi mwingine unaosema utakwenda kuandaman nmebaki kushangaaa kama kweli wew wakiume sijapata jibu...wew na kubenea hamna tofauti
 
Unachembechembe za mwanamke sio bure....nmerudia kuusoma huu uzi kutokan na kuanzisha uzi mwingine unaosema utakwenda kuandaman nmebaki kushangaaa kama kweli wew wakiume sijapata jibu...wew na kubenea hamna tofauti
Dino, pole sana kwa kutokunielewa, tatizo ni uwezo na viwango vya uelewa!. Watu wa levels tofauti za uelewa wanahitaji times tofauti kusoma jambo na kulielewa, nenda kasome tena bandiko lile huku umetulia, ukijiona bado hujaelewa, then utakuwa hujafikia level ya uelewa wa bandiko lile !.

Pole tena.

Pasco
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…