Ushauri kwa CHADEMA: Japo ni Haki, lakini chondechonde Msiandamane. Mwenye Nguvu Mpishe!

Serikali ikitenda kwa kukiuka, kutokutenda au kukandamiza, mahakama kupitia powers zake inatoa executive orders, au writs za prohibition, certiorary na mandamus kuiamuru serikali itake isitake!
Pasco, between the law and political science notions there is something practical on how we run the government in the real world. Ninaamini kuwa wanataaluma wengine wakitoa mawazo na uzoefu wao wa kuendesha serikali wataweza kupanua mjadala kufukia hapo katika real world state governance. Hata hivyo umenikumbusha mipango yetu tuliyokuwa tukisuka enzi za DARUSO change miaka hiyo, tukilenga kuishitaki Serikali. Ni bahati mbaya hata washauri wetu, waadhiri wa sheria wa enzi hizo, walikuwa hawaamini we would achieve anything with the ......certiorari, mandamus, et cetra strategies.
 

Ushauri mbaya huu maana wakifanya hivi, watakuwa wamefungua cycle ya violence ambayo hawataweza kuizima, kumbuka kule Soweto mauaji ya wale watoto waandamanaji yalivyofungua moto wa Resistance kwa nchi nzima.
Kinachotakiwa hapo ni Kutoa haki kwa mujibu wa katiba na sheria za nchi.
 
Wajibu wa vyama vya siasa kanuni zipo wazi kabisa !!
Na kwa upande wa katiba ya jamhuri
ya muungano ipo wazi kuhushu sheria za jamhuri kuzifuata! Soma ibara ya 26
 
Mimi napenda tuoneshe kuwa nguvu ya umma kamwe haijawahi kushindwa! Chadema tufanye mikutano kila kijiji. kila wilaya, kila mkoa na ngazi ya Taifa tena muda uleule halafu tuone itakavyo kuwa. Haiwezekani watu tulijinyima ili tumtoe Dikteta IDD AMINI halafu mwingine anakuja karne hii kuonesha udikteta wake! haiwezekani.
 
Ushauri mzuri
Chama cha siasa kama taasisi inayojitegemea shughuli zake nini?
Unajua kutofanya mikutano ya hadhara
na maandamano!watakuwa wamepoteza sifa ya kuitwa chama cha siasa?
Ila tu niseme ya kwamba huyo mheshimiwa akipiga marufuku chama tawala kutofanya shughul za kisia mpaka 2020.ni sawa kwa kuwa yeye ndiye mwenyekiti wa hicho chama ila kwa vyama vingine aviache kwani vina
Wenyeviti wao na wasemaji wao.

Na pia kila chama kina m/kiti taifa!
 
Tuko kwenye the reign of terror nchi haiendeshwi tena kwa sheria na katiba bali kwa kauli na utashi wa rais, siku ile anawaambia polisi mkiwakamata majambazi malizaneni nao wasiinuke ,nitawapandisha vyeo, maadam ameishasema hataki na wala hapendi kujaribishiwa, ndio maana nawashauri jamaa zangu wasijaribu! . Kule Pemba Cuf ilisumbua sana lakini baada ya kuwafyatulia za moto na kuwazika faster kwa kuwatosa baharini mpaka leo hutakaa usikie tena CUF wanaandamana Pemba. Mwenye mamlaka ya nchi akisema hataki ni hataki, atakaye kaidi cha moto atakipata! .

Sisi waona mbali tumeishaiona nia ovu kwenye katazo lile, tumesema humu ili kila mwenye masikio asikie na mwenye macho aone! .

Pasco
 
Wacha kujifanya kutabiri jua wakati wa kiangazi
Tarehe 1 utaingia barabarani kamanda? Najua siku hiyo Mbowe atakuwa amepumzika Mikocheni na Lowassa kapumzika Masaki akisubiri kuona majeruhi kwenye TV au maiti hili wapate mtaji wa siasa.
 
Tarehe 1 utaingia barabarani kamanda? Najua siku hiyo Mbowe atakuwa amepumzika Mikocheni na Lowassa kapumzika Masaki akisubiri kuona majeruhi kwenye TV au maiti hili wapate mtaji wa siasa.
Tunashukuru kwa kutuwekea ukweli kuwa mmejiandaa kuwaua watu...asante sana Ritz
 
Tarehe 1 utaingia barabarani kamanda? Najua siku hiyo Mbowe atakuwa amepumzika Mikocheni na Lowassa kapumzika Masaki akisubiri kuona majeruhi kwenye TV au maiti hili wapate mtaji wa siasa.
Kuhusu kwenda tutaenda
ni lazma kuwa tayari kupamba
na namna yoyote ya uonevu,ukandamizaji.udhalilishaji
na uonevu.
 
Kuhusu kwenda tutaenda
ni lazma kuwa tayari kupamba
na namna yoyote ya uonevu,ukandamizaji.udhalilishaji
na uonevu.
Kamanda nakushauri ukiondoka nyumbani acha kabisa umeandika wosia kuna uwezekano usirudi au ukarudi miguu imevunjika. Huyu siyo JK huyu ni Magu.
 
Kamanda nakushauri ukiondoka nyumbani acha kabisa umeandika wosia kuna uwezekano usirudi au ukarudi miguu imevunjika. Huyu siyo JK huyu ni Magu.
Unamwogopa ww sisi siyo
Lelemama!kama yeye hajaribiwi
na sisi hatujaribu!na hatuogopi vitisho vyako wala vyake!
ina maana endapo tutakuwa tunaogopa
kila kitisho kuna hatari kubwa nchi yetu
kurudi kwenye utawala wa chama kimoja!ambayo si dalili nzuri kwa mutakabali wa nchi
 
WASWAHILI WALISEMA "UOGA NI ADUI WA HAKI"

Chadema wanatakiwa wajifunze misukosuko mbinu ambazo CUF wamepitia hadi wakafanikiwa kuingia katika serikali ya Zanzibar tena kikatiba (ijapokuwa kwa kipindi hichi hawamo)

CUF inao mtaji mzuri sana wa wapenzi na wanachama wake hasa linapokuja suala la kutetea haki yao, mara nyingi huwa hawarudi nyuma pindi wanapoamua kusimamia haki yao hasa viongozi wao wanapokuwa wako nyuma yao.

Ni vijana wa CUF ndio walioondoa kashfa ya vinyesi katika mashule, visima na masoko Pemba pale walipoweka mtego na kuwakamata Polisi na ndoo zao za mavi tayari kuharibu.

Ni vijana wa CUF ndio ambao walipambana kishujaa katika maandamno ya January 2001! Pamoja na athari zote zilizowapata lakini bado wakafanikiwa kugain kitu.

Hivyo basi vijana na wapenzi wa CHADEMA inabidi wasimame imara na kusapoti kwa vitendo kauli za viongozi wao.
 
Umetoa maelezo mareeeeefu alafu pointless ndio zimejaa, unaweza ukajiona umeongea logic lakini asilimia kubwa ya hii insha uliotuandikia hapa ni uharo tu...

Labda nikuulize unawelewa nini maana ya upinzani?
Na nini faida na dhamira kuu ya vyama pinzani katika nchi yoyote ile?

Nijibu hapa kisha tuurefushe mjadala ufahamu na makosa yako!!

Na ulivyosema elimu ya kiraia/siasa Tanzania ina mapungufu sana hata ukukosea kwa sababu hata wewe mwenyewe kwa hichi ulichokiandika ni uthibitisho tosha wa kauli yako.
 
pole sana,maybe wewe ndo uwe careful
 

Wewe naona hujui unaongea kitu gani bali unabwabwaja tu kufurahisha genge.

Wewe huwajui WAPEMBA zaidi ya unaowaona hapa wakifanya biashara.

Serikali zote mbili zinawafahamu vizuri wapemba ninani linapokuja kusimamia suala wanaloliamini, Kama CUF PEMBA hawatakaapo waandamane tena mbona serikali zote mbili zinawagwaya mno wakati Wapemba hata GOBORE hawana!!????

Ulikuwepo wapi wakati wa uchaguzi wa marudio pale serikali zote mbili zilipomimina Pemba Askari kwa maelfu huku wakisapotiwa na silaha nzito nzito zikiwamo gari za kivita!!!!???
Hawa wote walikuwa njiani kuelekea Pemba na hiyo Gari ya kivita ikivinjari mitaa ya Pemba.

Unajua nikwanini serikali zote mbili ziliwagwaya wapemba wakati wa uchaguzi wa Marudiol!!??? Nikwasababu mara hii wapemba walikuwa na mbinu Mpya za kupambana na vyombo vya dola, msikilize Kijana hapa halafu uje na shombo zako juu ya wapemba.


Kumbuka hivi sasa WAPEMBA wako kimya nikwasababu wanawasikiliza viongozi wao wa juu waliotaka watulie ili wao wapapatue haki yao iliyodhulumiwa!! Wala hawako kimya eti kwa sababu niwaoga!!!!! Hilo haliko kwa Wapemba ambao dini yao inawakataza kumuogopa mtu kupita kiasi.
 
Ninavyofahamu mimi hakuna mahali po pote ambako majeshi yanatumika kukandamiza wananchi yaliwahi kufanikiwa. Tayari majeshi ya nje yanaingia Burundi kwa kuwa tu Nkuruzinza aliamua kuvunja katiba. Je, sasa ana amani gani? Wananchi wa chama chake na wale wa upinzani wote wanakufa. Marafiki zake wanajeshi nao wanauawa. Furaha ya kutawala iko wapi? Kuna shida gani kufuata kanuni na sheria zinazotawala nchi? Ndugu zangu, VITA HAINA MACHO.
 
Sasa Pemba kuna amani? Sawa. Watu watakufa. Je, wenye kuua wenzao hawatakufa? Unadhani mtu akifa ndiyo mwisho wa maisha? Kama alikuwa muuaji ndipo mateso ya milele huanza. Maisha hapa duniani ni mafupi sana.
 

Wewe Pasco naona unazidi kuchafua hali ya hewa baada ya thread yako na sasa hii comment.

Huo ushauri unaojaribu kutoa hapa ni kutuletea habari za kijima, we unaona sawa tu watu watii kila agizo wanaloambiwa na wasichukue yoyote hata kama ni agizo la kipuuzi? huo ni utwana...

Unasema eti waende mahakamani kuomba tafsri sahihi ya sheria inayohusu maandamano.. hivi unaishi Tanzania wewe?

Mahakama gani hizo? hizi za kibongo ambazo zimewekwa mfukoni na CCM na hata sheria zenyewe zinatafsiriwa kuendana na matakwa ya watawala..!!?

Kama waliweza kufanya amendment ya sheria ya mita 200 hili kuendana na kauli ya raisi, watashindwa nini kutwambia safari hii tena kwa kiongozi huyu aliyopo kwamba "SHERIA INASEMA MAANDAMANO YOYOTE YALE NI KOSA LA JINAI"....?

leo hujawaza kabisa Pasco.
 
Pasco acha hahari zako wengine tunahamu ya kuvunja watu wewe unaleta sanaa za kuwapa ushauri sisi tutapata wapi watu wa kupiga? Acha waje tufanye kazi yetu tupate posho za kazi ya kutukuka.
Eeeh Mungu wa mbinguni msamehe kiumbe wako huyu hajui alisemalo! Amen
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…