econonist
JF-Expert Member
- Jul 11, 2015
- 20,189
- 29,663
Kutokana na Hali iliyojitokeza jana , nashauri ya kwamba CHADEMA watangaze kususia uchaguzi Mkuu ujao na uchaguzi wa Serikali za mitaa. Hii ni kutokana kwamba Serikali kupitia polisi imeshaonesha biasness na kwamba uhalifu wowote dhidi ya CHADEMA polisi hawatashughulika nao.
Itakuwa ni aibu kwa CHADEMA kuaminika kwamba TAMISEMI chini ya mkwe wa Rais ambaye ana mamlaka juu ya polisi atakuwa na haki kwa CHADEMA kwenye uchaguzi wa Serikali za mitaa.
Nashauri ya kwamba kwa jinsi polisi walivyojipanga Jana dhidi ya CHADEMA ni onyo kwa CHADEMA kwamba haitaruhusiwa kukaribia madaraka ya Rais na kwamba polisi wapo tayari hata kuua ili tu CCM ibaki madarakani.
CHADEMA ijiulize Kama Mzee Ally Kibao kauawa kikatili na hakuna yeyote aliyewajibishwa, Soka kapotea mazima, hakuna wakuwajibishwa. Kama uhai wa mtu haupewi thamani yake sembuse kura kwenye uchaguzi.
CHADEMA itangaze hadharani kwamba haitashiriki chaguzi zozote hapa Tanzania mpaka haki ya waliopotea na kuuawa inapatikana.