LGE2024 Ushauri kwa CHADEMA: Susieni uchaguzi wa serikali za mitaa

LGE2024 Ushauri kwa CHADEMA: Susieni uchaguzi wa serikali za mitaa

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024
Kutokana na Hali iliyojitokeza jana , nashauri ya kwamba CHADEMA watangaze kususia uchaguzi Mkuu ujao na uchaguzi wa Serikali za mitaa. Hii ni kutokana kwamba Serikali kupitia polisi imeshaonesha biasness na kwamba uhalifu wowote dhidi ya CHADEMA polisi hawatashughulika nao.

Itakuwa ni aibu kwa CHADEMA kuaminika kwamba TAMISEMI chini ya mkwe wa Rais ambaye ana mamlaka juu ya polisi atakuwa na haki kwa CHADEMA kwenye uchaguzi wa Serikali za mitaa.

Nashauri ya kwamba kwa jinsi polisi walivyojipanga Jana dhidi ya CHADEMA ni onyo kwa CHADEMA kwamba haitaruhusiwa kukaribia madaraka ya Rais na kwamba polisi wapo tayari hata kuua ili tu CCM ibaki madarakani. CHADEMA ijiulize Kama Mzee Ally Kibao kauawa kikatili na hakuna yeyote aliyewajibishwa, Soka kapotea mazima, hakuna wakuwajibishwa. Kama uhai wa mtu haupewi thamani yake sembuse kura kwenye uchaguzi.

CHADEMA itangaze hadharani kwamba haitashiriki chaguzi zozote hapa Tanzania mpaka haki ya waliopotea na kuuawa inapatikana.

Kina imhotep na wale wenzao watasema wewe ni CCM
 
kwanza hapatakua na athari zozote za kikatiba, kisiasa au kidemokrasia nchini, ikawa ushauri huo utapokelewa na kutekelezwa vyema na Chadema, na kwahivyo vyama vingine vyenye uwezo vinaweza kushiriki uchaguzi huo bila mbambamba yoyote..

Infact,
Tanzania kuna vyama vya kisiasa zaidi ya 22 vyenye usajili wa kudumu, na kwakweli hiyo itakua fursa ya kipekee sana kwa vyama hivyo vya siasa, kuvuna wanachama na kura za wanachadema waerevu, wenye fikra huru na wanaofahamu vyema haki na wajibu wao katika maamuzi ya uongozi wa nchi na uongozi wa maeneo wanakoishi...

Itakua ni fursa muafaka sana kwa wanachadema waliochoshwa na ngonjera za uongozi wa chama chao uliopo sasa , ambao umekosa kabisa mawazo mapya wala fikra mbdala, zenye kuwatia matumaini wanaChadema na wananchi kwa ujumla, bali daima wamekua wakiwavunja moyo na kuwakatisha tamaa wanachadema , kwa mipango na uelekeo wa kukurupuka na usio eleweka..

Hiyo itakua Fursa ya pekee sana na muafaka kwa viongozi waandamizi wa Chadema waliopo madarakani sasa, kuondoka uongozini mara moja, kwa kushindwa kwao kazi ya kusimamia misingi na malengo ya kuanzishwa kwa Chadema..

Hata hivyo,
kuzira, kususaa, kuandamana au kugomea jambo lolote humu nchini, hakujawahi kuisaidia Chadema au wananchi kitu chochote, na hivyo huu utakua ni muendelezo wa ushauri au maamuzi ya hovyo na mabovu zaidi katika historia ya Chadema..

Naunga mkono hoja 🐒

Mungu Ibariki Tanzania

CHADEMA wagomee uchaguzi. Ili kushinikiza ajenda yao ya kupata uwajibikaji wa walihusika na utekaji.
 
Mambo ya kususa yamepitwa na wakati. Shiriki uchaguzi uhalisia uthihirike kuanzia mchakato hadi uchaguzi na matokeo ya uchaguzi. Hata hivyo hitaji la Katiba mpya ni muhimu na mazungumzo yaendelee kuhusu Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi.

Kwa Hali ya Jana hata CHADEMA wakiibiwa nani atawatetea?
 
Fried chicken dance

msikimbie mtanange mvune mlicho panda

Kama wanachama wetu wamepoteza na Wala hakuna anayewajibika je kushiriki huo uchaguzi Kuna lolote la maana? Maana hata wakiibiwa kura hakuna wa kuwajibika.
 
Kutokana na Hali iliyojitokeza jana , nashauri ya kwamba CHADEMA watangaze kususia uchaguzi Mkuu ujao na uchaguzi wa Serikali za mitaa. Hii ni kutokana kwamba Serikali kupitia polisi imeshaonesha biasness na kwamba uhalifu wowote dhidi ya CHADEMA polisi hawatashughulika nao.

Itakuwa ni aibu kwa CHADEMA kuaminika kwamba TAMISEMI chini ya mkwe wa Rais ambaye ana mamlaka juu ya polisi atakuwa na haki kwa CHADEMA kwenye uchaguzi wa Serikali za mitaa.

Nashauri ya kwamba kwa jinsi polisi walivyojipanga Jana dhidi ya CHADEMA ni onyo kwa CHADEMA kwamba haitaruhusiwa kukaribia madaraka ya Rais na kwamba polisi wapo tayari hata kuua ili tu CCM ibaki madarakani. CHADEMA ijiulize Kama Mzee Ally Kibao kauawa kikatili na hakuna yeyote aliyewajibishwa, Soka kapotea mazima, hakuna wakuwajibishwa. Kama uhai wa mtu haupewi thamani yake sembuse kura kwenye uchaguzi.

CHADEMA itangaze hadharani kwamba haitashiriki chaguzi zozote hapa Tanzania mpaka haki ya waliopotea na kuuawa inapatikana.
Tanzania remains a dangerous country in which to be a member of the political opposition, despite a change of president in 2021.
 
CHADEMA wagomee uchaguzi. Ili kushinikiza ajenda yao ya kupata uwajibikaji wa walihusika na utekaji.
ninahisi upo uwezekano mkubwa wa matokeo ya uchunguzi unaoendelea yakaishangaza chadema na umma wa waTanzania..

Inasikitisha sana, Inauma sana, Inatafakarisha sana. Uongozi tu ndrugu zangu tena wa chama?🤭
 
Mambo ya kususa yamepitwa na wakati. Shiriki uchaguzi uhalisia uthihirike kuanzia mchakato hadi uchaguzi na matokeo ya uchaguzi. Hata hivyo hitaji la Katiba mpya ni muhimu na mazungumzo yaendelee kuhusu Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi.
Uhalisia udhihirike wakati uhalisia unafahamika kuwa hizo chaguzi zinafanyiwa uhuni, na wanaotangazwa washindi ni kwa matakwa ya ccm? Yaani hadi leo hujajua uhalisia bali unategemea uchaguzi unaokuja ndio uhalisia ufahamike?!
 
Back
Top Bottom