LGE2024 Ushauri kwa CHADEMA: Susieni uchaguzi wa serikali za mitaa

LGE2024 Ushauri kwa CHADEMA: Susieni uchaguzi wa serikali za mitaa

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024
Kutokana na Hali iliyojitokeza jana , nashauri ya kwamba CHADEMA watangaze kususia uchaguzi Mkuu ujao na uchaguzi wa Serikali za mitaa. Hii ni kutokana kwamba Serikali kupitia polisi imeshaonesha biasness na kwamba uhalifu wowote dhidi ya CHADEMA polisi hawatashughulika nao.

Itakuwa ni aibu kwa CHADEMA kuaminika kwamba TAMISEMI chini ya mkwe wa Rais ambaye ana mamlaka juu ya polisi atakuwa na haki kwa CHADEMA kwenye uchaguzi wa Serikali za mitaa.

Nashauri ya kwamba kwa jinsi polisi walivyojipanga Jana dhidi ya CHADEMA ni onyo kwa CHADEMA kwamba haitaruhusiwa kukaribia madaraka ya Rais na kwamba polisi wapo tayari hata kuua ili tu CCM ibaki madarakani. CHADEMA ijiulize Kama Mzee Ally Kibao kauawa kikatili na hakuna yeyote aliyewajibishwa, Soka kapotea mazima, hakuna wakuwajibishwa. Kama uhai wa mtu haupewi thamani yake sembuse kura kwenye uchaguzi.

CHADEMA itangaze hadharani kwamba haitashiriki chaguzi zozote hapa Tanzania mpaka haki ya waliopotea na kuuawa inapatikana.
Dah! Watu tulivyo na NCAA, wakisusa tunakulaaa
 
Mna susa, susaaaaaaa, susaaaaaa...
Hivi kumbe maandamano yalikua ya chadema na si wananchi?

Yalikuwa ya CHADEMA maana wao ndio waliomba kibali. Lengo la maandamano ni kupinga utekaji na mauaji ya wananchi yanayofanywa na watu wasiojulikana.
 
Nyie mkisusia, wengine wanakula. Tuone nani atagalagazwa na njaa.
Hasira za mkizi ni furaha kwa ccm. Mawazo ya kipuuzi sana hayo.

Kwako mwana CCM ni mawazo ya kipuuzi. Ila kwa CHADEMA ni mawazo sahihi, maana lengo ni kuuchakachua huu uchaguzi ili kuonesha mama Samiah anakubalika.
 
ninahisi upo uwezekano mkubwa wa matokeo ya uchunguzi unaoendelea yakaishangaza chadema na umma wa waTanzania..

Inasikitisha sana, Inauma sana, Inatafakarisha sana. Uongozi tu ndrugu zangu tena wa chama?🤭

Mbona unaropoka?. Wewe umejuaje yaliyomo kwenye uchunguzi?.
 
Uhalisia udhihirike wakati uhalisia unafahamika kuwa hizo chaguzi zinafanyiwa uhuni, na wanaotangazwa washindi ni kwa matakwa ya ccm? Yaani hadi leo hujajua uhalisia bali unategemea uchaguzi unaokuja ndio uhalisia ufahamike?!

Kweli mkuu. Fikiria TAMISEMI isimamie uchaguzi wakati Waziri wake ni mkwe wa mwenyekiti wa CCM . Ni ujinga kushiriki uchaguzi Kama huo.
 
CHADEMA tusishiriki huu uchaguzi wa Serikali za mitaa.
 
Hiyo itakuwa political suicide kwa Chadema. Wakisusia CCM itawapa vyama shikizi vile vya kwenye briefcase nafasi chache za udiwani na ubunge hata kama havikupiguwa kura za kutosha ili ku justify uharamu wao na kuihadaa dunia kuwa uchaguzi wa vyama vingi umefanyika na ndiyo itakuwa mwisho wa Chadema. Wakijaribu kufurukuta kuandamana watapigwa na hata kuuwawa na Mahakamani nako wataangukia pua kwani majaji wote wanapokea maagizo toka kwa mwenyekiti wa CCM.
 
Back
Top Bottom