LGE2024 Ushauri kwa CHADEMA: Susieni uchaguzi wa serikali za mitaa

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024
Dah! Watu tulivyo na NCAA, wakisusa tunakulaaa
 
Mna susa, susaaaaaaa, susaaaaaa...
Hivi kumbe maandamano yalikua ya chadema na si wananchi?

Yalikuwa ya CHADEMA maana wao ndio waliomba kibali. Lengo la maandamano ni kupinga utekaji na mauaji ya wananchi yanayofanywa na watu wasiojulikana.
 
Nyie mkisusia, wengine wanakula. Tuone nani atagalagazwa na njaa.
Hasira za mkizi ni furaha kwa ccm. Mawazo ya kipuuzi sana hayo.

Kwako mwana CCM ni mawazo ya kipuuzi. Ila kwa CHADEMA ni mawazo sahihi, maana lengo ni kuuchakachua huu uchaguzi ili kuonesha mama Samiah anakubalika.
 
ninahisi upo uwezekano mkubwa wa matokeo ya uchunguzi unaoendelea yakaishangaza chadema na umma wa waTanzania..

Inasikitisha sana, Inauma sana, Inatafakarisha sana. Uongozi tu ndrugu zangu tena wa chama?🤭

Mbona unaropoka?. Wewe umejuaje yaliyomo kwenye uchunguzi?.
 
Uhalisia udhihirike wakati uhalisia unafahamika kuwa hizo chaguzi zinafanyiwa uhuni, na wanaotangazwa washindi ni kwa matakwa ya ccm? Yaani hadi leo hujajua uhalisia bali unategemea uchaguzi unaokuja ndio uhalisia ufahamike?!

Kweli mkuu. Fikiria TAMISEMI isimamie uchaguzi wakati Waziri wake ni mkwe wa mwenyekiti wa CCM . Ni ujinga kushiriki uchaguzi Kama huo.
 
Baada ya kususa kuna athari gani itatokea?

Kama za akina Halima Mdee. Itabidi serikali ianze kuhonga wanachama ili ipate angalau wabunge wa upinzani.
 
CHADEMA tusishiriki huu uchaguzi wa Serikali za mitaa.
 
Hiyo itakuwa political suicide kwa Chadema. Wakisusia CCM itawapa vyama shikizi vile vya kwenye briefcase nafasi chache za udiwani na ubunge hata kama havikupiguwa kura za kutosha ili ku justify uharamu wao na kuihadaa dunia kuwa uchaguzi wa vyama vingi umefanyika na ndiyo itakuwa mwisho wa Chadema. Wakijaribu kufurukuta kuandamana watapigwa na hata kuuwawa na Mahakamani nako wataangukia pua kwani majaji wote wanapokea maagizo toka kwa mwenyekiti wa CCM.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…