Pre GE2025 Ushauri kwa Kassimu Majaliwa: Mjomba kesho yako imevurugwa kwa Makusudi, fuata nyazo za Dkt. Mpango Philip

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Katiba najua, ndo maana logic yangu imejikita kwenye kutogombea ili bungeni awe mbunge wa kawaida.

Term limit ya urais ni miaka mitano Tena mitano, kuhusu uwaziri mkuu hamna kizuizi, uwaziri inatokana na mbunge wa kutoka jimbo la uchaguzi, Muhimu ateuliwe tu na Rais na bunge lipitishe!!
 
Hawezi kuwa mjinga kama wewe mtoa mada.
 
Hawezi kuwa mpumbavu kama wewe mtoa mada.
Mkuu aksante sana Ubarikiwe kwa matusi!!
Matusi Yako nitafanya Lunch MODS wataona utaratibu unaofaa, mara nyingi Matusi ni short cut way ya mtu aliyeshindwa kujibu hoja 🙏🙏🙏

Karibu mkuu kwa MATUSI ZAIDI, Mungu akubariki sana kwa Matusi haya 🙏🙏🙏
 
Majaliwa ni msimamizi wa shughuli zote za serikali lakini wizi serikalini umetamalaki, matumizi ya hovyo na ufisadi tupu, nchi imejaa vijana wakubet tupu, Simba na Yanga, haoni aibu Tanzania kuagiza ngano, mchele, mafuta, sukari nje n.k?
Excutive power kuadabisha wezi ipo mikononi mwa nani???

PM au Rais??
Don't over smart your boss!! anatembea kwenye msingi huo
 
Majaliwa ana uwezo wa kutosha kupima mambo na kufanya maamuzi sahihi haitaji ushauri wako .

Kawawa alukuwa waziri mkuu kwa muda mrefu lakini aliwahi kubadilishwa na akawa waziri wa kawaida na akiendelea na ubunge. Msuya na Malecela waliwahi kuwa mawaziri wakuu na waliondolewa wakaendelea kuwa back benchers bungeni, sasa nini cha ajabu ikiwa Rais ataona inafaa ampe mtu mwingine jukumu la uwaziri mkuu.

Nchi hii vyeo vya juu vinatolewa kwa kuangalia vigezo mbakimbali ikiwemo uwiano wa kidini ili kuleta utulivu.

Ili mtu aweze kuwa mchambuzi mzuri ni vyema akapitia literature review ya jambo analitaka kulitolea maoni kabla ya kuàndika.
 
Umeharibu ulipoanza kuleta udini tu kwani sisi tunachagua ma askofu au ma sheikh?
 
Unafikiri nimeandika kwamba nimeombwa ushauri?? la hasha!!

Ushauri sio shurti mtu anaweza kuchukua au akaukataa pia.

Vipi wewe amekuambia umjibie kuwa haitaji ushauri?? au umeamua kutoa maoni yako??🤔🤔

Nimeandika nikiwa na background ya mawaziri wakuu waliomaliza muda, ndo maana nmeona wakati wa sasa sio vyema kuwa na Waziri Mstaafu akihudumu kama mbunge wa kawaida bungeni.

Sbinafsi naona sio vema yeye kupitia mkondo wa Msuya, kawawa, warioba ,malechela.

Zama zimebadilika, by the way response yako imekosa LOGIC Kabisa!!!
Jitahidi sana kutumia logic unapoandika, kama unaelewa LOGIC lakini!!🤔🤔🤔
 
Umeharibu ulipoanza kuleta udini tu kwani sisi tunachagua ma askofu au ma sheikh?
Naona wewe ni mgeni Tanzania, Kuna mambo hayapo katika maandishi ,hayajawa Institutionalized, lakini yanafanyika kubalance kwa ajili ya National Interest.

Top layers katika nchi yoyote ile hasa TZ haiwezi kuwa ya watu wa dini Moja tuu.

Hapo hakuna udini!! Labda huelewi na hutaki kuelewa!!!
🤔🤔
 
Ushauri mzuri sana. Ila kama anajipata sawa sawa angemaliza uwaziri wake mkuu akapumzika ale pesa zake alizowekeza. Shabani mpwa wake mzee wa ulisi wa ruge angeachiwa achukue jimbo
Shabani naona analinyemelea Jimbo la Ndanda,, Yuko na projects nyingi sana pale..
Mara ligi za mpira, mara mikesha ya burudani, mara misaada,
Bila shaka Ndanda ya Mwambe anaitaka
 
Kuna mtu nimewahi kuongea naye kuhusu hili, ilikuwa kabla ya kuchapishwa Fomu Moja kule Dodoma juzi.

PM alikuwa na ndoto ya kwenda kule juu zaidi, lakini yale maamuzi ya Juzi Dodoma ndiyo yamemwondoa kwenye reli.

Hata hivyo amepanga kuendelea kuwa Mbunge ili Mipango ya kwenda juu zaidi isife.

Ndiyo maana akina Edo hata baada ya kupata ile ajali ya 2008 lakini bado aliendelea kuwa karibu na Wajumbe ili kupata sapoti ile ya Mwaka 2015 (Tunaimani na Edo)

Kwahiyo PM ataendelea kuwa Mbunge wa kawaida ili asiwe nje ya ulingo

Waswahili wanasema "Fimbo ya mbali haiui Nyoka"
 
Katika stadi za mawasiliano, alifanya vizuri sana, alijua ukweli, lakini
Kiongozi hatakiwi kuwa muongo kwa Taifa analoliongoza! Majaliwa aliliongopea Taifa kuhusu kifo cha Magu ; that disqualifies him from any leadership position.
Hakuwa na mmlaka ya kutoa Tangazo la kifo, msiba wa Kitaifa , mwenye mamlaka balikuwa makamu wa Rais AMBAYE nkikatiba ndiye Rais.

Msiba wa Kitaifa Rais kufia madarakani sio jambo dogo, maandalizi yanatakiwa,ilitaka aingilie kazi ambayo siyo yake??

Alichofanya ni ku fill information gap!! Vacuum, nature does not allow Vacuum!!!
 
Sijamjibia nimejibu hoja yako maananunafikiri uko katika better position kuelewa situation kuliko Majaliwa mwenyewe.

Kukuongezea Warioba alikuwa waziri mkuu na makamo wa kwanza wa rais lakini aliondolewa akawa waziri wa kawaida tu. Salim pia alikuwa waziri mkuu akaondolewa akawa waziri wa kawaida japo alipewa cheo ambacho hakipo kikatiba cha naibu waziri mkuu. Kwa hiyo hakuna cha ajabu uwaziri mkuu wa Majaliwa ukiondoka.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…