Ushauri kwa Rais Samia kuhusu panya road

Ushauri kwa Rais Samia kuhusu panya road

Umasikini unatofautina ndugu,nafuu mm na wewe Ni masikini lakin tunamiliki smart phone/computer na tumepata hela ya bando mpaka tukaja kuriply apa Kuna mwingine tangu asubuhi mpaka Sasa mdomo haujaenda kinywan
..

Lakini pia naungana na wewe umasikini sio sababu pekee ya kufanya uwe panya road Kuna watu n maskini zaidi yao na sio panya rodi
Kweli mkuu
 
Maana yake Kuna sababu kubwa nyingine ambayo siyo hiyo aliyoitoa mtoa mada.

Kwa ufupi mtoa mada ameandika uongo.
Sababu kuu ni UMASKINI! ingawa zipo sababu nyingine!.
 
Huu ushauri wanatoa panya road wenyewe labda wanaona maji yanataka kuzidi Unga.
Polisi, piga risasi hawa wapumbavu kwanini wanajichagulia adhabu? Mbona wao wanapotukata mapanga hawasemi tuchague adhabu.?
Jino kwa jino ndo dawa yenu.

Mkuu nitake radhi kwa kuninasibisha na panya road

Mimi kuja kulifaham geraza hilo kuna muaustralia anampango wa kuanza uchimbaji wa dhahabu . Sikutarajia kama nitafika huko lakini mikazi ya watu ndoo nikafika

Usije ukasimuliwa funga safari mwenyewe ufike huko ,sizani kama atakaekuwa anapingana na mawazo yako anakuwa nae ni panya road

Pole saana
 
Mtoa mada hajaandika uongo , na pia zipo sababu nyingine zinazo sababibisha kuwapo hawa panya rodi Kama vile malezi,,ushawishi kutoka katika maraki zoa ambao Ni panya rodi nakadhalika
Ameandika uongo kwa kuifanya sababu hiyo kuwa ndiyo msingi.
 
Hapa ndipo umeandika uongo na unaurudia uongo huo. Ingekuwa ni sababu kuu basi sote tungekuwa Panya road, sababu ya msingi ni malezi mabovu kutoke hapa yanazalika mambo ya hivyo kama hayo.
Toeni AJIRA acha kuleta utetezi wa kitoto! Sababu kuu ya uhalifu ni UMASKINI!
 
Hao panya Road lazima watambue kuwa hawawezi kucheza na usalama wa Taifa hili wakabaki salama, lazima wajuwe kuwa njia walioichagua kupita Ni ngumu na yamajuto Sana, lazima wajuwe kuwa serikali hii haiwezi ikawafumbia macho watu wanaohatarisha usalama wa Taifa Hili, lazima wajuwe hawawezi wakajeruhi watu, wakapora watu, wakaua watu wasio na Hatia halafu wabaki salama na kutamba mitaani,

Lazima wajuwe kuwa usalama wao Ni kuachana na vitendo hivyo vya kiharamia na kinyama, Haiwezekani watu waishi kwa hofu kwa ajili yao hao vibaka, lazima wajuwe kuwa kazi hiyo haina manufaa na niyamoto Sana,

Nampongeza Sana mh mkuu wa mkoa wa DSM mh Amos makala kwa namna yeye na vyombo vyake vya ulinzi na usalama wanavyoendelea kuhakikisha hao panya Road wanamalizwa na jiji linarudi katika utulivu na Amani, lazima wasakwe wote, lazima wakamatwe wote na lazima wajuwe kuwa huwezzi ukashindana na serikali Wala huwezi ukaishinda serikali
 
Hao Panya road sio watukutu sana?
Hivi Hilo gereza unalifaham kweli?

Hao ni vijana wadogo kiumri tunaweza kwenda kuwadidimiza zaidi tofauti na kuwafunza/kuwafundisha

Usione nawatetea sana hapana kama ni wahalifu wanapaswa washughulikiwe kisheria

Cha kushangaza Leo hii tumeshupaza shingo kwa panya road tunasahau kuna kundi la watu ambao ni zaidi ya panya road wao kila uchwao tunawasifu na kuwaabudu huku wao ndoo chanzo cha kupatikana kwa hao panya road

Mkuu jiulize Kwa nini Hawa watoto wadogo wanakuwa na tabia hizi ? Kama malezi wazazi wawajibike na kama ni hao tunaowaimbia mapambio na kuwasifu tumewawajibisha vipi ?

Kwa bahati mbaya Afrika huwa tunatibu matokeo badala ya chanzo nafikili nawe unamlengo huo huo mku, niwie radhi kama nimekukwaza
 
Dah,Gereza la Ngwala kule ni jehanamu ndogo Mkuu.Hawa watoto wakienda kule alafu warudi uraiani lazima watakuwa masheikh,wachungaji au washauri wa maadili mema kwa wenzao.🤣🤣🤣🤣
Lipoje??
 
Dawa nzuri kabisa ya kumaliza panya road ni kuwaua tu. Wakionekana mahali na mapanga na nyundo zao ni kuwapurula risasi tu, wataacha tu.
Kuwapeleka gerezani ili tukawalishe kwa kodi zetu ni kutuongezea hasara.
Kwanza wanaua watu - muuaji hastahili kuishi.
Pili wanatupunguzia nguvu kazi kwa kuua na kuumiza wajenzi wa taifa.
Tatu, kwa nini kodi zetu zitumike kulisha majamba na wauaji? Ni afadhali hiyo pesa itumike kujenga madarasa na kununua madawa huku vijijini.
 
Dawa nzuri kabisa ya kumaliza panya road ni kuwaua tu. Wakionekana mahali na mapanga na nyundo zao ni kuwapurula risasi tu, wataacha tu.
Kuwapeleka gerezani ili tukawalishe kwa kodi zetu ni kutuongezea hasara.
Kwanza wanaua watu - muuaji hastahili kuishi.
Pili wanatupunguzia nguvu kazi kwa kuua na kuumiza wajenzi wa taifa.
Tatu, kwa nini kodi zetu zitumike kulisha majamba na wauaji? Ni afadhali hiyo pesa itumike kujenga madarasa na kununua madawa huku vijijini.

Uko sahihi sana, ripoti ya CAG imejaza taarifa za majizi ya fedha za umma kuliko hao panya road, je hao mnawaua lini?
 
Rais hao panya road wakikamatwa wasiuliwe bali wapelekwe Chunya gereza la Ngwala wakalime na kujifunza mambo mbalimbali yatakaowasaidia katika maisha yao.

Gereza la Ngwala halina fence yoyote na wafungwa wanaishi kindugu na kufanya shughuli mbalimbali za uzalishaji.

Kwanini gereza halina fence? Lipo katikati ya pori lenye wanyama wakali. Ukitoroka lazima simba wapite na wewe!
Kwanini wewe Panya road unataka kujichagulia adhabu? Dawa ya panya road ni chuma
 
Officially Tanzania is no longer the worst country to GET poor but the worst country to REMAIN poor!
 
Back
Top Bottom