Ushauri kwa Rais Samia: Kwenye mabadiliko ya Cabinet kufuatia Ripoti ya CAG, tumia wazoefu; Fedha mpe Dkt. Kimei, Biashara Uwekezaji mpe Deo Mwanyika

Huu ni Ushauri wa Bure kwa Rais Samia kwenye mabadiliko tarajiwa ya cabinet kufuatia Ripoti ya CAG, namshauri Rais Samia, asibabaike sana na kuangalia ma vyeti ya usomi kwenye uteuzi
wa cabinet yake, atumie watu wenye uzoefu, mfano Waziri wa Fedha wa sasa Dr. Mwigulu Mnchemba ni msomi mzuri wa uchumi, ana 1st Class ya degree ya uchumi kutoka UDSM, lakini sio mtu wa ki fedha fedha!. Hajawahi kushika na B na ma B na ma B mikononi mwake kama Dr. Charles Kimei alipokuwa CRDB, hivyo Wizara ya Fedha akimpa Dr. Kimei, fedha zitakuwa zimefika kwenyewe.

Kwenye biashara na uwekezaji, kuna wasomi wawili, madaktari wa PH.D, jee wanewahi kufanya chochote hata kuuza nyanya tuu?. Kwenye Biashara Uwekezaji ampe Deo Mwanyika, kina Sumri, kina Shabiby, Abood etc, watu wenye uzoefu wa kufanya biashara.

Aunde Baraza dogo lenye mawaziri wenye uzoefu, ukiwa na mtu mwenye uzoefu, hawezi kupigwa kirahisi kama msomi mwenye vyeti lakini hajawahi kuuza hata toothpicks!.

Ni ushauri tuu

Paskali
Tatzo nani atatekeleza ushauri wako shida iko hapo
 
Heri yako upo unbiased wengine wanaotaka mabadiliko ya baraza la mawaziri wanavizia uwaziri mkuu. Waziri Mkuu hajatajwa popote lakini wanalazimisha aondolewe, aibu nasikia mimi mtu mwadilifu kama yule kuundiwa zengwe ili atolewe.
Msimamizi mkuu wa shughuli za serikali ni nani? acha aondolewe haraka
 
Huu ni Ushauri wa Bure kwa Rais Samia kwenye mabadiliko tarajiwa ya cabinet kufuatia Ripoti ya CAG, namshauri Rais Samia, asibabaike sana na kuangalia ma vyeti ya usomi kwenye uteuzi
wa cabinet yake, atumie watu wenye uzoefu, mfano Waziri wa Fedha wa sasa Dr. Mwigulu Mnchemba ni msomi mzuri wa uchumi, ana 1st Class ya degree ya uchumi kutoka UDSM, lakini sio mtu wa ki fedha fedha!. Hajawahi kushika na B na ma B na ma B mikononi mwake kama Dr. Charles Kimei alipokuwa CRDB, hivyo Wizara ya Fedha akimpa Dr. Kimei, fedha zitakuwa zimefika kwenyewe.

Kwenye biashara na uwekezaji, kuna wasomi wawili, madaktari wa PH.D, jee wanewahi kufanya chochote hata kuuza nyanya tuu?. Kwenye Biashara Uwekezaji ampe Deo Mwanyika, kina Sumri, kina Shabiby, Abood etc, watu wenye uzoefu wa kufanya biashara.

Aunde Baraza dogo lenye mawaziri wenye uzoefu, ukiwa na mtu mwenye uzoefu, hawezi kupigwa kirahisi kama msomi mwenye vyeti lakini hajawahi kuuza hata toothpicks!.

Ni ushauri tuu

Paskali
Mkuu CCM inabidi ipotee ktk uso wa Dunia.
Shida ni hiyo.

Sasa kama Rais wako anasema Katiba ni kijitabu tu... Wtf...
Kuna nchi hapo..kuna kuwajibishana..

Wacha tufe tu.
 
Wananchi tunataka pesa irudi na watu wafungwe!!
Hapa kwenye kufungana sisiemu ndo hawataki, kama civics ya form 2 inasema mbunge lazima awe na chama, lakini tupo na genge bungeni japo bunge lote nalo genge tu ila lile genge dogo linakesi mahakamani siku zinaenda tu. Ndo washindwe kulinda hawa wagawanaji percent za miradi
 
Waongeaji wengi matapeli na chawa ...Tunataka uwezo basi Kimei anafit kabisa.
Mkuu, sikumaanisha wapiga porojo nilimaanisha watu wenye uwezo wa kueleza sera na ikaeleweka, katika misingi hiyo itakuwa ngumu sana kwa Dr. Kimei. Nadhani pia hilo la kushindwa kuwasilisha kitu kikaeleweka ndio limemkosesha wizara.

Uwaziri ni nafasi ya kisiasa, huwezi kuitenga siasa na uwezo wa kujieleza.
 
Back
Top Bottom