Ushauri kwa Rais Samia: Kwenye mabadiliko ya Cabinet kufuatia Ripoti ya CAG, tumia wazoefu; Fedha mpe Dkt. Kimei, Biashara Uwekezaji mpe Deo Mwanyika

Ushauri kwa Rais Samia: Kwenye mabadiliko ya Cabinet kufuatia Ripoti ya CAG, tumia wazoefu; Fedha mpe Dkt. Kimei, Biashara Uwekezaji mpe Deo Mwanyika

Mwigulu is an Economist in Profession but not a Financial Economics expert.
Hajawai ku-practice taaluma yake ya Uchumi kama akina Dr Mpango, Marehemu Professor Beno Ndulu,Dr Kimei nk.
Kaka Pascal ingia LinkedIn kuna Watanzania wana CV nzito na wanafanya kazi kwenye reputable organization and companies lakini mpaka unafika mahala unashangaa inakuaje tuna ongozwa na watu wa ajabu!

Sent from my V2111 using JamiiForums mobile app
Sawa katika hao uliowataja ,mbona Hadi Sasa Mwigulu anaonekana kuwazidi wote kwenye Management ya Uchumi?

Pili Uchumi sio Fedha tuu,elewa hii kwanza maana mnadhani kuongoza Wizara ya Fedha ni kuongoza firm.Na Kwa taarifa Yako Duniani kote Wizara ya Fedha inaongozwa na Wataalamu wa Uchumi na sio Wakuu wa firm Fulani.

Mwisho nitajieni Waziri mwenye mafanikio Mkubwa kwenye Wizara ya Fedha kumzidi Mwigulu Ili tuwaringanishe.

View: https://twitter.com/BusInsiderSSA/status/1721624598385504379?t=FzHpkfZ2eQyHjTTdQCiJdg&s=19
 
Huyo Mwigulu kazi kumsifia Rais hata katika lisilo muhusu, ndio jambo anaweza. Wizara yake imeshindwa kusimamia mambo mengi mno, fedha zinapotea huku miradi ikiendelea kwa kukopa madeni makubwa mno ambayo wakati wa kulipa sio yeye au boss wake watakuwepo madarakani kisha tutawalaumu walio madarakani.
Kwa nini ujinga wa leo tusiuzibiti na kuuacha uwe mzigo kwa wengine?
 
Hata utengue na kupangua Baraza na Hao wengine usipobadili Baadhi ya sheria ni kazi Bure.

Kwa mfono kwani kubadili Baraza ndio kunazuia Ufisadi? Kuna sehemu Mawaziri wametajwa?

Labda Kama hizo panga pangua ni za kujipangia Kisiasa Kwa Ajili ya uchaguzi sawa nothing else.
soma vizuri mapendekezo ya ya mtoa bandiko, wadau ambao anadhani wanaweza kusaidia, mthalani wizara ya fedha n.k.
kwa maoni sioni mbadala wa aliyoko hapo fedha hadi 2025.

Jambo la pili,
Mabadiliko ya sheria huchochewa na udhaifu wa sheria zilizopo, lakini pia huchochewa na malengo fulani ya kisiasa au kijamii. Politics is all about interest, nothing happens out of mere coisidence every thing is well planned, organized and executed to achieve a certain specific political objectives.

Kwa mfano kesi ya ugaidi mbowe, uteuzi wa Makonda Uenezi, kupigwa chini akina mpina Baraza la mawaziri, uteuzi Naibu Waziri Mkuu, kuongezwa badgeti ya kilimo, maji na miundombinu these are polical driven changes kusafisha njia kuelekea 2025 n.k..

Jambo la tatu,
Kupambana na ufisadi kunahitaji kuwa na utashi na uthubutu wa kuchukua hatua kwa sheria zilizopo.
Zilizopo huzitumii utaka zingine?
Mbunge moja alisema juzi kama sio jana, kwamba we need to realistic habari ya kusema at fisadi anyongwe ni mbali sana,
hebu kwanza tumkamate ajulikane ajitetee tujue ukweli awajibishwe kisheria....

Baadhi ya mawaziri kisekta wameanza kuchukua hatua muhimu,ni Imani ya waTz hatua zaidi zitafuata dhidi ya wengine wote...
 
Naunga mkono hoja.

Moja ya makosa tunayofanya nikuwapa watu nafasi kubwa huku hawana historia yeyote ya kufanya kazi kwenye serious business yeyote duniani wakaleta matokeo.
Hizi jamii za watu waliokulia kwenye chama sijui UVCCM na kuwaamini kwenye serious position zinazohitaji watu wenye akili waliozoea kufanya kazi za pressure na zenye kupimwa na matokeo, ndio failure yetu ilipo pia naamini.

Mwanyika anaweza kutusaidia maana amehudumu kwenye serious, busy and pressure mining business kwenye higher position.
Kimei pia amehudumu kwenye busy and serious bank business kwenye highest level na greatest perfomance.
 
Unampa mtu uwaziri sijui uRC mara UDC sikui ukatibu mkuu kwa kigezo tu ni mpambe au chawa mzuri, au alimvulia chupi fulani mara sijui kijana wetu wa chama halafu tunataka matokeo.

Ni wakati sasa wa kuachana na hizi damu za vijana waliokulia pale Lumumba na wale baba zao waliowahi kuwa waheshimiwa, ni wakati sasa wakupima akili za watu na mafanikio yao ya nyuma kwenye utendaji ulioleta matokeo chanya hasa kwenye hizi international entity ndio tuwape mavyeo..

Shida inaanzia pale Lumumba kwa hofu yakuogopa mageuzi ndani ya chama na wale kamlete waliozoea kubebwa kukosa ugali tena.

Wapo watanzania wengi wenye akili wanaweza kuivusha hii nchi haraka sana ila shida inaanzia kwenye uoga wa chama kwa kuogopa damu mpya yenye akili za kisasa na yenye kuamini kwenye matokeo ya haraka na utendaji wa nguvu na smart.
 
mfano, huyu Waziri wetu wa fedha ni wapi alishawahi kuhudumu na mkuu wa kitengo na kuleta matokeo chanya yanayotufanya tumuamini kwenye nafasi kubwa kama hiyo.

Yule Kijana Makamba ni wapi brain yake ilishawahi kufanya kazi na kuleta matokeo? mpaka tumuamini kwenye nafasi nyeti?.

Yule Nape, ni wapi alishawahi kufanya kazi na kuleta matokeo chanya mpaka tumuamini kwenye hizi nafasi nyeti?

Huyu Ummy na Tulia, ni wapi waliwahi kufanya kazi na kuleta matokeo chanya mpaka tuwaamini kwenye nafasi hizi kubwakubwa.

Rizmoja, alishawahi kuleta matokeo chanya wapi kwa kutumia brain yake mpaka tumuamini kwenye ngazi hizi za maamuzi?

Chain ni ndefu na inakwenda mpaka chini huko kwa watendajo wadogo kabisa, ni michongo michongo tu..

Taifa linahitaji watu serious ili liweze kuendelea na sio mzahamzaha tu.
Taifa letu bado ni changa na masikini, linahitaji sana big brains wanaoweza kuset mipango na kulinasua kutoka kwenye umasikini na kuliweka mahala pazuri.
Hizi akili za siasa siasa za Lumumba zinazowaza kutawala tu haziwezi kutusaidia asilani baadala yake tutaishia kuendelea kuwa ombaomba na kuchekwa tu.

Mataifa yote yaliyoendelea huko nyuma wakati wakuset mipango nakujinasua kwenye matope hayakuwahi kuwa na viongozi wazembewazembe wapenda mizaha mizaha.
 
Huu ni Ushauri wa Bure kwa Rais Samia kwenye mabadiliko tarajiwa ya cabinet kufuatia Ripoti ya CAG, namshauri Rais Samia, asibabaike sana na kuangalia ma vyeti ya usomi kwenye uteuzi wa cabinet yake, atumie watu wenye uzoefu, mfano Waziri wa Fedha wa sasa Dr. Mwigulu Mnchemba ni msomi mzuri wa uchumi, ana 1st Class ya degree ya uchumi kutoka UDSM, lakini sio mtu wa ki fedha fedha!. Hajawahi kushika na B na ma B na ma B mikononi mwake kama Dr. Charles Kimei alipokuwa CRDB, hivyo Wizara ya Fedha akimpa Dr. Kimei, fedha zitakuwa zimefika kwenyewe.

Kwenye biashara na uwekezaji, kuna wasomi wawili, madaktari wa PH.D, je, wanewahi kufanya chochote hata kuuza nyanya tu? Kwenye Biashara Uwekezaji ampe Deo Mwanyika, kina Sumri, kina Shabiby, Abood etc, watu wenye uzoefu wa kufanya biashara.

Aunde Baraza dogo lenye mawaziri wenye uzoefu, ukiwa na mtu mwenye uzoefu, hawezi kupigwa kirahisi kama msomi mwenye vyeti lakini hajawahi kuuza hata toothpicks!

Ni ushauri tu.

Paskali
Tengeneza list kamilli kisha tengeneza poll tupige kura humu ... kura ya maoni
 
Hamutaki mvinyo ule ule ndani ya chupa mpya ??!!
😅😅 watu wamechoka na majina yale yale miaka yote ! Naunga mkono hoja !! 🙏🙏
Mkuu mzeewaSHY majina yale yale yanawafanya baadhi yao waamini kwamba wao ndio wana hatimiliki ya uongozi wa nchi hii.
Acha tushauri wajaribu upande wa pili kwa wasomi wawili watatu, nako tuone itakuaje 😂😂😂
 
Utendaji upi bila kuongea utakapilizwa wakati wa Changamoto? Unadhani kuwa Waziri wa Fedha ni sawa na kuwa MD wa CRDB?
Sema Tanzania tunapenda kuongozwa na wajinga na ndiyo maana huwezi kuona potential ya Dr.Kimei.
Tunasema Kimei kwasababu ana ujuzi na uzoefu na masuala ya fedha na pia ata kudhibiti uhuni wa Mabenki anajua wapi pa kuanzia.
Mwigulu ni Economist in Profession but not an Economics expert.Mwigulu amewai ku-practice wapi taaluma yake nje ya kuwa Mwanasiasa tu?
Wakina Kimei wame-practice taaluma zao na wana uelewa mkubwa wa changamoto zilizopo mtaani kuliko hao Wanasiasa uchwara wanaobebwa na Msoga Kingdom.

Sent from my V2111 using JamiiForums mobile app
 
Huu ni Ushauri wa Bure kwa Rais Samia kwenye mabadiliko tarajiwa ya cabinet kufuatia Ripoti ya CAG, namshauri Rais Samia, asibabaike sana na kuangalia ma vyeti ya usomi kwenye uteuzi wa cabinet yake, atumie watu wenye uzoefu, mfano Waziri wa Fedha wa sasa Dr. Mwigulu Mnchemba ni msomi mzuri wa uchumi, ana 1st Class ya degree ya uchumi kutoka UDSM, lakini sio mtu wa ki fedha fedha!. Hajawahi kushika na B na ma B na ma B mikononi mwake kama Dr. Charles Kimei alipokuwa CRDB, hivyo Wizara ya Fedha akimpa Dr. Kimei, fedha zitakuwa zimefika kwenyewe.

Kwenye biashara na uwekezaji, kuna wasomi wawili, madaktari wa PH.D, je, wanewahi kufanya chochote hata kuuza nyanya tu? Kwenye Biashara Uwekezaji ampe Deo Mwanyika, kina Sumri, kina Shabiby, Abood etc, watu wenye uzoefu wa kufanya biashara.

Aunde Baraza dogo lenye mawaziri wenye uzoefu, ukiwa na mtu mwenye uzoefu, hawezi kupigwa kirahisi kama msomi mwenye vyeti lakini hajawahi kuuza hata toothpicks!

Ni ushauri tu.

Paskali
Paskali njaa akiamua kutumia miakili yake ile ya zamani anaitumia kweli..
 
Wewe ndio kilaza,huyo mtu wenu ana kigugumizi Sasa atafanyaje kazi za siasa?
Kwani unamjua peke yako?Kigugumizi umempa wewe?mtu mwenye Kigugumizi anawezaje kuchangia mijadala Bungeni kama yeye Kimei anavyofanya?
Sema mifumo yenu ya uwizi mlioyoijenga mnaogopa watu wa Private sector watakuja kuibomoa![emoji1787][emoji1787]
Kimei amekaa BOT miaka 13,amesoma Economics Russia na ana PhD ya Money and Finance(Uholanzi).
Utamlinganisha na uyo mchunga ng'ombe na punda wa Singida.Ficha upumbavu wako kidogo basi!

Anaongea kama anakunywa uji 😂😂

Kuchangia Mjadala sio sawa na kujibu hoja under pressure elewa Hilo we kilaza.
 
Back
Top Bottom