Coach Slamah Hamad
JF-Expert Member
- Nov 12, 2014
- 3,740
- 4,938
Miaka ya kustaafu ipunguzwe 45 mwisho mtu aachie ngazi sasa wazee wamekaza eti mpaka miaka 60 ni mingi sana 45 tu astaafu akiwa a nguvu zake akaanzishe mradi ili awaajir wengine na wengine warithi nafasi yake. pia ajira za mkataba n sawa sasa sirikali inaangaika mbowe tu
No haliko practical mkuu, kama ishu ni mitaji kwa nini badala ya kuwaongezea mishahara waajiriwa kwa nini wasiwape graduates hio pesa wafanye mitaji??Hela inayopotea kwa wizi na ufisadi ni nyingi kuliko ambayo ingetosha kulipa watu 5M kwa mwezi! Kwa sasa tuna tozo pia mbona linawezekana!
Sasa kumbuka hapa tunazungumzia mpango maalumu ili kunusuru janga la ajira kwa graduates! Yani lengo ni upewe hela nyingi kwa muda mfupi ili upishe wenzio! Mbona hili swala liko practical sana.
Ambaye ataonekana hatoshi pia ataondolewa kupisha wengine, ili kulinda ufanisi! Cycle ya ajira inakuwa ya muda mfupi tu.
Wataitoa kwa minajili ipi sasa?No haliko practical mkuu, kama ishu ni mitaji kwa nini badala ya kuwaongezea mishahara waajiriwa kwa nini wasiwape graduates hio pesa wafanye mitaji??
Hapo Kuna Kitu utasaidia Ila Kuna Mambo Utaharibu Kabisa. Naona Umeangalia Kwa Upande mmoja Kwamba Unawasaidia Wasio na Ajira Pekee
Kumbuka Makazini Kunahitaji Uzoefu Pia Wa Kazi huwezi Kuingiza Watu na Kutoa Tu na Kuweka Wasio na Uzoefu
Kubeti na boda boda ndio suluhisho enyi wenye madigrii na diploma msiogope njooni huku tusukume gurudumu la maendeleo[emoji205]
Sawa sawa mkuu! Wacha niendelee na genge langu mkuu[emoji1666] sawa mr.extrovert ila tusubiri kidogo Hadi 2030..ili tuupeleke mswada bungeni.
Namaanisha badala ya kuongeza mshahara mpaka 5M kwa mwezi,hio hela wapewe graduates kama mtaji.Wataitoa kwa minajili ipi sasa?
Wakijiua ni mipango binafsi! Kama una 60m una uwezo wa kuizalisha kama huna jiunge na wanaoweza! This is how we create wealth
Naendelea kusisitiza ingewezekana bodi ya mkopo iwakopeshe wahitimu wa chuo wote boda boda na hela ya kianzio cha kubeti wapambane na maishaKuna muda nilihisi Upo humu kuvuruga mada kwa bahati mbaya, hapa leo nimepata jibu sahihi!
Hiyo haiondoi uzuri wa hoja yakekwakweli. Mleta mada akipata ajira serikalini sidhani kama atabakiwa na ili wazo
Watu wengi uwezo wao kufikiri kwa mantiki uko chini.RAISI AJAE
Tanzania kuna watu wengi ukiwaambia katiba mpya ni kitu muhimu sana watasema siyo muhimu lakini akigeuka analalamikia mambo yanasababishwa na katiba mbovu. Kwa kifupi wengi hawaoni correlation kati ya vitu kama ulivyoandika na katiba.
Roho mbaya ipi? Hii nchi si ya watanzania wote? Kwa nini wengine wafe wakiwa vikongwe kwenye ajira za umma ambazo ni kodi za watanzania wote huku wengine wakionekana hawastahili?Mmeanza roho mbaya
Ukimaliza na miaka 30 miaka 15 ya ajira inatosha, uwapishe wengine.Hapo Itabidi hata Miaka ya Masomo Ipungue Pia. Maana Mtu anamaliza Masomo Wengine 30+ ishagonga
Hiyo training waliyoipata na uzoefu kazini wataenda kuutumia kwenye sekta binafsi, hicho ndicho kinachofanyika Marekani ndio maana unaona watu wengi sana kwenye siasa na sekta binafsi ya Marekani ni wanajeshi wastaafu ila bado ni vijana.Hii haina tija. Unawaajiri watu ná kuwapa training yenye gharama kubwa katika utendaji wa kazi zao za kila siku. Baada ya miaka mitatu wakati tayari wana experience ya kutosha katika utendaji wa kazi zao unawaondoa na kuwaleta wapya ambao hawajui chochote na zoezi la kutoa training upya linaanza tena!!!. Kuna wizi, ufisadi na ubadhirifu mkubwa sana Serikalini kama mianya hii ikiondolewa basi Serikali inaweza ikatoa ajira nyingine kati ya laki 5 mpaka milioni bila matatizo yoyote yale.
RAISI AJAE
Umeanza kupata akili sasa, enzi za jiwe ulificha ubongo wako kabatini kwake.Inabidi kumuondolea powers hizo raisi na mpini tuushike wananchi!
Miaka mitano mtu anakuwa bado hajaiva kiutumishi hivyo taasisi zitayumbaSio kusaga rumba! Unapewa miaka 5 ya kulipwa vizuri tu hili wazo nilishakujaga nalo jamaa ameamua kulianzishia uzi pia too good kumbe kuna mtu alikuwa na maono sawa na mimi tu!
Chukulia mfano mtumishi alipwe 5M kila mwezi bila kujali cadre! Kuwe na kiwango fixed kwamba kulingana na uchumi wa sasa we need to pay atleast 5M itampa nafasi ya kila mtumishi kuishi na ku save kiasi flani kila mwezi nje ya pension yake anayokatwa na NSSF! Chukulia mfano una save million kila mwezi tu..after 12 months utakuwa na million 12...after 5 years una million 60! Ukijumlisha na yale makato ya NSSF hamna hamna una 85M hivi kwa hii pesa mtu hajapata pa kuanzia tu?
Ikifika miaka mitano mkataba unaisha unaondoka na mtaji wa kutosha kabisa usiopungua 50M! Utashindwa kujiajiri kweli?
Itapunguza sana tatizo la ajira kila mwaka kunaweza kuwa na watu wapya zaidi ya laki watakoukuwa wanaingia kwenye mfumo wa ajira wa serikali huku wengine wengi wanaotoka serikalini wakiwa wanaingia kwenye mfumo wa wa sekta binafsi kupitia mafao yao kama mitaji.Ni kweli mkuu kazi nyingi zina value experience ya mtu,kwa kampuni the cost ya kusubiri new graduates wapate uzoefu wa kazi sio sawa na ku retain employees ambao wana uzoefu.
Plus hii HAITAPUNGUZA TATIZO LA AJIRA since kila mwaka kuna wahitimu wengi wanashushwa mtaani, jibu ni kutafuta njia za kuongeza ajira na sio njia za kutafuta kugawana hicho kidogo kilichopo
Hiyo training waliyoipata na uzoefu kazini wataenda kuutumia kwenye sekta binafsi, hicho ndicho kinachofanyika Marekani ndio maana unaona watu wengi sana kwenye siasa na sekta binafsi ya Marekani ni wanajeshi wastaafu ila bado ni vijana.