Ushauri kwa Serikali ya Tanzania, hususan Waziri wa Fedha kuhusu misamaha ya kodi

Ushauri kwa Serikali ya Tanzania, hususan Waziri wa Fedha kuhusu misamaha ya kodi

CCM hakuna kitu cha maana ishawahi kufanya...
 
inamankusweke
unaposema
wanyonyaji,hapo bado wanakula sadaka,zaka,fungu la kumi...hawali kwa jasho

hivi unafikili kuanzisha kanisa mpaka lipate hao waleta zaka nijambo rahisi kunavitu vigumu sana msiwe mnasema wanakula bila jasho
Hata Kama,siyo kunyonya hazina kwa ruzuku na misamaha ya kodi,hata hivyo kazi ya kusaka wafuasi ilifanyika zamani,Sasa hivi mtu anazaliwa anafuata dini ya wazazi,so yeah..hawali kwa jasho
 
Kwa mara ya kwanza umeleta hoja ya maana ya kizalendo. Hili la wabunge kupewa misamaha ya kodi, marupurupu kibao na mikopo ya mchongo ni mojawapo ya kansa kubwa katika nchi hii. Kamwe hatutakaa tuwe na siasa safi na maendeleo ya kweli kama tutaendelea kukumbatia mifumo ya kinyonyaji kama hii
Huwa unanisoma kwa uoga tu.
 
We mama unajua kuwa kanisa halifanyi biashara? Usitake kuleta ushauri mbovu kwa serikali wakati unajua serikali haina uwezo wa kutoa huduma kwa jamii peke yake mpaka isaidiwe. Lengo lako hasa unataka kanisa likomolewe, hao wabunge na misikiti umejumuisha tu ili kuficha lengo lako ovu. Kama serikali itafuata ushauri wako na kuutekeleza poa tu, pia irudishe shule na hospitali zote ilizotaifisha zirudi kwa wenyewe wazihudumie kikamilifu
 
Yaaan miaka Ile najiunga JF, nikawa naona wakumention mention, Kwa akili yangu nikawa najua wee ni mtu ambaye una upeo mkubwa wa Akili ,umejaza Kichwa chako Maarifa ya kutosha.
Hapa Jamii forums, hapo zamani tumeshajadili sana kuhusu misamaha ya kodi ya kila namna na jinsi inavyotuumiza. Leo hii sitaki kuchanganya mjadala wa kodi aina nyingi, nashauri hapa misamha ya kodi sehemu mbili tu ifutwe:


1) Wabunge wote wafutiwe misamaha yote ya kodi.
2) Taasisi za kidini zifutiwe misamaha yote ya kodi.


1) Wabunge:

Hakuna asiyeelewa kuwa Tanzania wabunge wanalipwa vizuri sana kuliko sehemu nyingi sana serikalini na uraiani. Licha ya kipato chao kuwa kikubwa, wana upendeleo maalum wa mikopo, hapohapo wanasamehewa kodi.

Naamini hii si haki kwa Watanzania ambao wengi wetu ni vipato vya chini kuendelea kuwasamehe kodi wabunge.

Misaaha ya kod kwa wabunge, imeleta athari ya kuwa na wabunge wengi ambao wapo bungeni kwa maslahi yao binafsi na si kwa kuwatumikia Watanzania. Tujadili.

2) Taasisi za dini.


Hapa ndiyo kabisa siioni sababu ya hizi taasisi kuwa na misamaha ya kodi. Sioni sababu hata moja ya kwanini taasisi za dini ziwe na misamaha ya kodi.


Tunaitaka serikali yetu, ilitazame hili haraka iwezekanavyo, misamha ya kodi yote ifutwe kwa wabunge na na taasisis za kidini.

Enough is enough.

Hili la taasisi za kidini tumeona likipigwa danadana, mara linafungiwa misamaha mara inardushwa. Tuwe na msimamo mmoja ytu na lisijadilike. Kama hatuwezi kuendesha dini etu mpaka tuwe na misamaha ya kodi, tusifunguwe taasisi za kidini, tufundishane dini misikitini na makanisani, misikiti na makanisa yasiweza kujiendesha bila misamaha ya kodi ifunge milango yake na izifanye kumbi za starehe serikali iingize pesa.

Binafsi, misamaha ya kodi naiona kuwa ni wizi mtupu.

Nasikitika sana kugundua kwamba ,nilifanya matumizi mabaya ya Akili yangu .


Wewe ni Mbumbumbu, ulojawa na udini.
 
Mzee #Kinana anasema “wabunge wetu wanalipwa pesa kidogo sana”[emoji848][emoji848][emoji27][emoji27][emoji3596]

MISHAHARA YA WABUNGE NI WIZI NA UNYANG'ANYI WA HALI YA JUU KABISA TANZANIA.

Suala la Mishahara ya Wabunge analoliongea @HecheJohn linaumiza roho sana.

Mwalimu wa Tanzania mwenye TGTS D1 mwenye mshahara take home 531,000 kwa mwezi, akifanya kazi kwa miaka 38 atalipwa shilingi 242,136,000 (milioni 242).

MBUNGE wa Tanzania kwa mwaka mmoja analipwa shilingi 240,300,000 (milioni 240 bila posho za kamati).

Yani mwalimu wa Tanzania mwenye degree analazimika kufanya kazi kwa miaka 38 ili aweze kupata malipo anayopewa mbunge wake (ANAYETAKIWA KUJUA KUSOMA NA KUANDIKA TU) kwa mwaka mmoja tu. Ndio uzalendo huu?????? @SuluhuSamia

YANI IPO HIVI,
Mbunge anayelala tu bungeni @bunge_tz analipwa;

Posho za vikao kwa mwaka ni sh. 42,300,000 (milioni 42.3)
Mshahara na marupurupu kila mwezi 16,500,000 × miezi 12 = 198,000,000 (milioni 198).
Jumla kwa mwaka mmoja ni sh. 240,300,000 (milioni 240, hii haihusishi posho za kamati za kudumu).

Kwa miaka mitano, mbunge wa Tanzania analipwa 1,201,500,000 (Bilioni moja na milioni 200) bila kuhusisha posho za kamati.

TUCHANGANUE MALIPO YA MBUNGE VIZURI.

Sitting Allowance - 220,000
Per Diem - 250,000
Jumla kila siku mbunge analipwa 470,000/= (haijalishi ameongea au lah).
Mshahara na marupurupu kwa mwezi - 16,500,000/=

Mshahara wa mbunge kwa mwaka mmoja ni shilingi 198,000,000 (milioni 198).
Mshahara wa mbunge kwa miaka mitano ni shilingi 990,000,000 (milioni 990).
Bado kila baada ya miaka mitano huyu mbunge analipwa kiinua mgongo milioni Mia mbili (200,000,000).

Vikao vya Bunge

Kikao cha Januari 31 - Feb 10 = siku 11
Kikao cha bajeti April 4 - June 30 = siku za vikao 59
Mkutano wa tisa wa bunge mwaka 2022 Nov 1-11 = siku 10
Mkutano wa nane kuanzia Sept 13-23 = siku 10
Jumla ya siku za vikao vya bunge ni siku 90.

Siku 90 za vikao × 470,000 = 42,300,000
42,300,000 za vikao × miaka 5 = 211,500,000

JUMLA KWA MIAKA MITANO
1,201,500,000 (Bilioni moja na milioni 200) bila kuhusisha posho za kamati.

TUANGALIE MSHAHARA WA MWALIMU KWA MIAKA MITANO

Mwl. mwenye TGTS D1 mshahara wake basic ni shilingi 771,000 kwa mwezi, ukitoa makato, take home ya mwalimu huyu no shilingi 531,000.

Mshahara wa huyu mwalimu kwa mwaka 531,000 × miezi 12 = 6,372,000 mara miaka mitano = 31,860,000 (huu ni mshahara wa Mia I miwili wa mbunge).

Kwa miaka 38 mwalimu analipwa 6,372,000 * 38 = 242,136,000 (sawa na mshahara wa mwaka mmoja wa mbunge).

Huyu mwalimu akidai nyongeza ya mshahara anaambiwa "KUWA MZALENDO." Kama sio wizi huu ni nini????

Wakati mbunge wa Tanzania anaogelea kwenye bwawa la utajiri wa kodi za walala hoi, mtoto wa mtanzania maskini anashindwa kujengewa hata choo cha tundu kwenye shule yake; hata dawati la shilingi elfu 50 tu limeshindikana; hata kitabu cha elfu kumi tu imeshindikana.

IFIKE MAHALI TUACHE HUU UFALA WA KUENDELEA KUFUMBIA MACHO UDHALIMU WAKATI TUNAOUMIA NI SISI NA WATOTO WETU. MABADILIKO YA KWELI YATAKUJA PALE WATU WA CHINI TUTAKAPOSIMAMA KUPINGA UDHALIMU.
 
Wewe bibi kizee utakufa mdomo wazi na chuki zako za kidini. Toka enzi za akina malaria sugu wa jf, sijawahi kusoma andiko lako lisilo na harufu za chuki za kidini. Unazunguuuka ila kinakuuma kwanini taasisi za kikristo zinashamiri na kufanikiwa. Kupanga ni kuchagua, endelea na sonona la moyo wako huku wanaume wakipiga kazi
Kabibi haka Kali tumia ujanja wake pale Magot club Sasa kamechoka kamekimbilia Siasa taka mkasame tu
 
Back
Top Bottom