Ushauri kwa Serikali ya Tanzania, hususan Waziri wa Fedha kuhusu misamaha ya kodi

CCM hakuna kitu cha maana ishawahi kufanya...
 
inamankusweke
unaposema
wanyonyaji,hapo bado wanakula sadaka,zaka,fungu la kumi...hawali kwa jasho

hivi unafikili kuanzisha kanisa mpaka lipate hao waleta zaka nijambo rahisi kunavitu vigumu sana msiwe mnasema wanakula bila jasho
Hata Kama,siyo kunyonya hazina kwa ruzuku na misamaha ya kodi,hata hivyo kazi ya kusaka wafuasi ilifanyika zamani,Sasa hivi mtu anazaliwa anafuata dini ya wazazi,so yeah..hawali kwa jasho
 
Huwa unanisoma kwa uoga tu.
 
We mama unajua kuwa kanisa halifanyi biashara? Usitake kuleta ushauri mbovu kwa serikali wakati unajua serikali haina uwezo wa kutoa huduma kwa jamii peke yake mpaka isaidiwe. Lengo lako hasa unataka kanisa likomolewe, hao wabunge na misikiti umejumuisha tu ili kuficha lengo lako ovu. Kama serikali itafuata ushauri wako na kuutekeleza poa tu, pia irudishe shule na hospitali zote ilizotaifisha zirudi kwa wenyewe wazihudumie kikamilifu
 
Yaaan miaka Ile najiunga JF, nikawa naona wakumention mention, Kwa akili yangu nikawa najua wee ni mtu ambaye una upeo mkubwa wa Akili ,umejaza Kichwa chako Maarifa ya kutosha.
Nasikitika sana kugundua kwamba ,nilifanya matumizi mabaya ya Akili yangu .


Wewe ni Mbumbumbu, ulojawa na udini.
 
Mzee #Kinana anasema “wabunge wetu wanalipwa pesa kidogo sana”[emoji848][emoji848][emoji27][emoji27][emoji3596]

MISHAHARA YA WABUNGE NI WIZI NA UNYANG'ANYI WA HALI YA JUU KABISA TANZANIA.

Suala la Mishahara ya Wabunge analoliongea @HecheJohn linaumiza roho sana.

Mwalimu wa Tanzania mwenye TGTS D1 mwenye mshahara take home 531,000 kwa mwezi, akifanya kazi kwa miaka 38 atalipwa shilingi 242,136,000 (milioni 242).

MBUNGE wa Tanzania kwa mwaka mmoja analipwa shilingi 240,300,000 (milioni 240 bila posho za kamati).

Yani mwalimu wa Tanzania mwenye degree analazimika kufanya kazi kwa miaka 38 ili aweze kupata malipo anayopewa mbunge wake (ANAYETAKIWA KUJUA KUSOMA NA KUANDIKA TU) kwa mwaka mmoja tu. Ndio uzalendo huu?????? @SuluhuSamia

YANI IPO HIVI,
Mbunge anayelala tu bungeni @bunge_tz analipwa;

Posho za vikao kwa mwaka ni sh. 42,300,000 (milioni 42.3)
Mshahara na marupurupu kila mwezi 16,500,000 × miezi 12 = 198,000,000 (milioni 198).
Jumla kwa mwaka mmoja ni sh. 240,300,000 (milioni 240, hii haihusishi posho za kamati za kudumu).

Kwa miaka mitano, mbunge wa Tanzania analipwa 1,201,500,000 (Bilioni moja na milioni 200) bila kuhusisha posho za kamati.

TUCHANGANUE MALIPO YA MBUNGE VIZURI.

Sitting Allowance - 220,000
Per Diem - 250,000
Jumla kila siku mbunge analipwa 470,000/= (haijalishi ameongea au lah).
Mshahara na marupurupu kwa mwezi - 16,500,000/=

Mshahara wa mbunge kwa mwaka mmoja ni shilingi 198,000,000 (milioni 198).
Mshahara wa mbunge kwa miaka mitano ni shilingi 990,000,000 (milioni 990).
Bado kila baada ya miaka mitano huyu mbunge analipwa kiinua mgongo milioni Mia mbili (200,000,000).

Vikao vya Bunge

Kikao cha Januari 31 - Feb 10 = siku 11
Kikao cha bajeti April 4 - June 30 = siku za vikao 59
Mkutano wa tisa wa bunge mwaka 2022 Nov 1-11 = siku 10
Mkutano wa nane kuanzia Sept 13-23 = siku 10
Jumla ya siku za vikao vya bunge ni siku 90.

Siku 90 za vikao × 470,000 = 42,300,000
42,300,000 za vikao × miaka 5 = 211,500,000

JUMLA KWA MIAKA MITANO
1,201,500,000 (Bilioni moja na milioni 200) bila kuhusisha posho za kamati.

TUANGALIE MSHAHARA WA MWALIMU KWA MIAKA MITANO

Mwl. mwenye TGTS D1 mshahara wake basic ni shilingi 771,000 kwa mwezi, ukitoa makato, take home ya mwalimu huyu no shilingi 531,000.

Mshahara wa huyu mwalimu kwa mwaka 531,000 × miezi 12 = 6,372,000 mara miaka mitano = 31,860,000 (huu ni mshahara wa Mia I miwili wa mbunge).

Kwa miaka 38 mwalimu analipwa 6,372,000 * 38 = 242,136,000 (sawa na mshahara wa mwaka mmoja wa mbunge).

Huyu mwalimu akidai nyongeza ya mshahara anaambiwa "KUWA MZALENDO." Kama sio wizi huu ni nini????

Wakati mbunge wa Tanzania anaogelea kwenye bwawa la utajiri wa kodi za walala hoi, mtoto wa mtanzania maskini anashindwa kujengewa hata choo cha tundu kwenye shule yake; hata dawati la shilingi elfu 50 tu limeshindikana; hata kitabu cha elfu kumi tu imeshindikana.

IFIKE MAHALI TUACHE HUU UFALA WA KUENDELEA KUFUMBIA MACHO UDHALIMU WAKATI TUNAOUMIA NI SISI NA WATOTO WETU. MABADILIKO YA KWELI YATAKUJA PALE WATU WA CHINI TUTAKAPOSIMAMA KUPINGA UDHALIMU.
 
Kabibi haka Kali tumia ujanja wake pale Magot club Sasa kamechoka kamekimbilia Siasa taka mkasame tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…