Ushauri kwa vijana: Kubeti siyo kazi

Ushauri kwa vijana: Kubeti siyo kazi

Wapenda mafanikio ya haraka utawajua tu na hao ndiyo wanaopapatikia michezo ya kamari na betting. Sina haja ya kumpangia mtu katika maisha yake lakini kitu ninchoona kinaangamizi vijana ni wajibu kuzungumza.
 
Hongera sana mkuu umetoa ushauri mzuri, katika uhalisia kamali ni dhambi mbele za mungu na haina maana yoyote.
Kuna mwamba alikua ana matatizo ya kifamilia yaan watoto wote wamerudishwa ada shuleni na mfukoni hana kitu mwamba anakwambia ndio ilikua ni mara ya kwanza kuanza kubet na ilivyo maajabu alitusua pesa ya kulisha familia miezi isiyopungua 6 kulipia mahitaji yote ya nyumba kuwavesha mke na watoto na kulipia ada za watoto mwaka mzima bila kugusa mshahara wake kwa pesa aliyoipata, unaambiwa mpaka leo jamaa hajaacha kubet kila siku memory inamwambia atatusua km vile na baada ya hapo mkewe alimwambia km hizi hela umepata kwenye betting usiache kubet kwa hio sasa hivi wote wanaishi kwa kubet juzi hapa walimwekea JKT Queens aliifunga Yanga Princess wakavuna kibunda cha kutosha
 
Mtoa mada mbona umeukimbia uzi wako? Njoo uone majibu ya ulichokileta.

Kazi sio lazima uonekane mtaani unajishuhurisha
🤣 mmemsengenya mpk ameenda kulia sahivi analia kwa kwikwi!,akirudi kusoma tena ataanza kulia kile kilio cha kugalagala kabisa!
 
Fanya Yako yaliokuleta duniani usijifanye mshauri kwenye mambo yasiyokuhusu kama umepigwa kwenye betting ni wewe wenzio tunakula pesa na tumefanikiwa haujaja na mtu duniani ishi maisha Yako halafu mwisho kabisa acha utapeli naona umeweka namba Ili upige wajinga.
ww mwenyewe hujaja na mtu vilevile kwa hiyo ungejijibu kimoyo moyo pasina kuandika🙄
 
Wewe usiebet mafanikio yako ni yepi? Mbona bado unaogelea katika umasikini
 
ww mwenyewe hujaja na mtu vilevile kwa hiyo ungejijibu kimoyo moyo pasina kuandika🙄
Nimemjibu sababu anataka kazi ambayo haimuhusu kwanini aangaike na jambo ambalo halimuhusu si shobo Mimi betting nahusika nayo ndio maana nimemjibu ukitaja betting Kwa kuiponda lazima nikujibu sababu umegusa kazi yangu inayonifanya niishi mjini
 
Wanasema Hivi watu wa gambling.

BETI kiasi ambacho upo tayari kukipoteza.

Kitu kibaya hapo ni Kuwa addicts .
 
Nilipogundua maisha ni betting nikaingia kwenye kubeti rasmi...nimewahi lima hekari mbili za mahindi nikapata debe 3 Za mahindi..nimewahi lima hekari moja ya maharagwe nikapata nusu ndoo...nimewahi fanyakazi kwenye taasisi X kwa mikataba mifupi kipindi cha miaka 6 nikatengenezewa zengwe nikatolewa kama mbwa aliyeiba mayai hadi niliokuwa nafanya nao kazi walibaki kushangaa na kuuzunika natena bila malipo yoyote ya kuanzia mtaani...nimekaa darasani mpaka sasa matumaini ya kupata ajira rasmi hayapo nimeomba kazi serikalini lakini wapi sijapata.. Nikaamini maisha ni kubahatisha kwa sasa mfariji wangu ni Betting anayenifanya niishi kwa matumaini...wewe unayetaka kuniondoa huku unakazi kubwa ya kunishawishi.
 
Back
Top Bottom