Ujenzi ni mgumu sana na unahitaji kujitoa sana na uvumilivu mkubwa . Jenga nyumba ambayo unaweza Kwa kipato chako.
View attachment 2486913
View attachment 2486914
View attachment 2486916
Narudia kipato chako sio kiwango cha pesa ulizokopa au ulizosave kwenye bank account yako maana kwenye ujenzi sio kitu cha ajabu Kwa bajeti kuisha huku kazi bado sana sasa hapo kinachofuata ni kipato chako ndio kimalizie mjengo .
Sasa kama ulikopa 100 mil ukaamua kujenga ghorofa alafu pesa inakata utajikuta pabaya sana maana benk wanakudai payment na nyumba inahitaji pesa kuendelea. Mimi wakati naanza kujenga nilikuwa na milioni 150 yote ili kwisha na nyumba bado sana sasa hivi natumia mshahara wangu kujenga .
It’s not easy lakini na make progress kubwa kila mwezi . Nondo ni hatari sana especially Kwa ghorofa . So jenga kulingana na kipato sio saving amount. Hapo ndio nimefikia sasa nilianza miezi mitano nyuma . Na natarajia kumwaga zege ya mwisho weekend ijayo.