Lord denning
JF-Expert Member
- Jun 3, 2015
- 15,819
- 33,255
Huu ujumbe umwendee Humphrey Polepole, wenye chuki wote na Mama Samia wakiongozwa na kile kikundi kilichotaka kuigeuza Tanzania nchi ya kikabila na kikanda!
Kwanza poleni sana! Naona mnateseka sana pale Mama Samia anapofanikiwa jambo! Mnajaribu kuzua mambo juu ya mambo ili kumtingisha Mama wa watu ila Mungu hajamuacha!
Mlianza kusema anaongozwa na Kikwete, wimbo ukachuja mkaja na ramli kuwa upigaji umerudi, wimbo huo pia umechuja, mkaja na anaondoa watu wa Jiwe, wimbo huu pia ukachuja haraka sana kutokana na watu kuanza kuwashtukia kuwa kumbe kazi yenu ni kum sabotage Mama wa watu!
Mama akiendelea kuupiga mwingi akatoa maagizo wamachinga wapangwe ikiwa ni mwanzo wa kuanza kurekebisha miji mliyoiharibu kwa Sera zenu mfu ili kupanga upya mitaa yetu na kutengeneza jamii ya kistaarabu inayofanya shughuli zake kwa kuzingatia usafi, mipango Bora na Pia kulipa kodi!
Baada ya kuona maeneo kama Dar ambapo kwa miaka 4-5 iliharibiwa kwa uchafu wa vibanda kila kona inaanza kupendeza! Posta pananawiri, Mwenge na Ubungo wanaanza kung’aaa mmeona sasa muhamishe Magoli kujipambanua kuwa ni watetezi wa Wanyonge ili kumtingisha Mama Samia. Nia ni moja tu , kumchonganisha Mama wa watu ila kumbe ndo mnafeli vibaya!
Leo napenda kuwapa ushauri murua kabisa humu
1. Kwanza jitahidini kutofautisha kati ya machinga na ufanyaji biashara holela unaoharibu miji na kuchochea uchafu! Serikali haizuii machinga kufanya biashara, serikali inazuia ufanyaji biashara holela, usiozingatia usafi, mipango miji na unaohamasisha uharibifu wa miondombinu.
Kama mtu anaweza kujenga kibanda barabarani cha mbao chenye mfumo wa duka chenye thamani ya Shs si chini ya Laki 5 huku akiweka bidhaa zenye thamani ya si chini ya Mil 2 Au 3 mpaka 4 huyo mtu anashindwaje kupanga fremu sehemu na kufanya biashara?
Kumbukeni mtaani kuna fremu hadi za elfu 70- 100 kwa mwezi! Sasa huyu mnadhani ni machinga au mkwepa kodi?
2. Jitahidini sana kupata exposure! Jueni uholela mnaotetea ndio unaosababisha nchi kukosa mapato makubwa sana na kila siku kuonekana Kama binadamu tusiowaza vizuri!
Mfano mtu anapanga vyombo barabarani vyenye thamani ya hadi Mil 5. Je huyu ni machinga Kweli? Vyombo vya Mil 5 anauza kila siku na kuingiza faida kubwa bila kulipa hata thumni Kama kodi! Je hiyo ni sahihi? Serikali ikikalia kimya hili siku za mbeleni itakuwaje kila mtu akisema sasa afanye biashara kwa mtindo huo??
3. Kama vijijini watu wanaenda kwenye gulio kununua bidhaa, Kama hapa Tanzania kwa miaka mingi watu wamekuwa wakitembea kwenda kufuata bidhaa sehemu fulani mf. Sokoni Kariakoo, Tandika na Tandale, kwa nini isiwe sawa sasa hivi serikali inaposema hao watu wawe sehemu moja na wanajamii wakafuate bidhaa huko?
Kuna shida gani watu kwenda kufuata bidhaa kwenye hayo maeneo hadi wafanyabiashara watoke kwenye maeneo rasmi na kwenda kuwafuata watu hivyo kufunga barabara, kuongeza msongamano, kusababisha kusambaa kwa uchafu mitaani na kuharibu miundombinu ambayo imejengwa kwa gharama kubwa?
Mbona kwenye smart areas mf maeneo ya majeshi watu wanatoka kwenda kufuata bidhaa sehemu mbalimbali na wanaishi hawafi? Kwa nini isiwezekane kwa watu Wengine? Nendeni Lugalo, Twalipo na maeneo mengine ya Jeshi, Je kuna vibanda vya machinga? Je hakuna watu wanaoishi huko?
Napenda kumaliza kwa kumshauri Polepole na wenzake wote! Ni vizuri mtumie muda wenu kuielimisha jamii ya Watanzania kujifunza kuishi kistaarabu, kwamba sio lazima bidhaa ikufuate, unatakiwa uifuate bidhaa ilipo ili ununue na kuitumia.
Ni vizuri mtumie akili zenu vizuri kujua kuwa hakuna mtu aliyekatazwa kufanya biashara, kinachohimizwa ni kwa namna gani biashara ifanywe huku sheria na taratibu zetu za kutunza mazingira na miji yetu zikizingatiwa na kufuatwa bila shida yeyote.
Ni vizuri mjue kuwa Serikali inataka kodi, na ujanja ujanja hasa kwenye kulipa kodi ni kitu ambacho hakiwezi vumiliwa na serikali yeyote ile makini.
Tulieni jifunzeni Uongozi kwa Mama Samia!