Kwanini unaona kutetea machinga ni jambo baya? Si machinga tu bali mtu yeyote kama ikionekana anaonewa ni vizuri kupata watetezi.
Umeweka mambo kadhaa ya kujadilika kiweledi na kwa uzoefu, kama ambavyo umetaja thamani ya bidhaa ambazo machinga wanatandaza barabarani.- hoja ipo"
Pia umeeleza serikali hatua ilizochukua ikiwemo kuwatafutia machinga maeneo mengine ya kufanyia biashara.- hoja ipo"
Idadi kubwa ya machinga siyo wa mitaji hiyo uliyoisema. Kumbuka kuna mama ntilie humo na wale wauza Mo energy pale buguruni stand.
Lakini mbona hata serikali yenyewe inawatetea machinga akiwemo rais mwenyewe? Kwanini uweke mipasho kama vile machinga ni watu wa kukataliwa?
Mimi binafsi napenda kutetea watu wanaotaabika lakini simo kwenye hizo songombingo zenu na akina polepole.
Wengine hii ni nature yetu kumtetea au kumsaidia yeyote anayetaabika.
Edit huu uzi, ondoa machinga waweke watu wako halafu wapige mawe unayotaka.