USHAURI: kwa wasioamini maswala ya time travel

Uwesutanzania

JF-Expert Member
Joined
Feb 9, 2019
Posts
1,380
Reaction score
1,686
Naomba niingie kwenye maada mojakwamoja,

Ni baada ya kupitia mijadala kadhaa ya kitu kinachoitwa time travel nimeona watu wengi wakipingana na hii kitu, mimi binafsi bila ya lengo ya kujinufaida na faida yeyote ile napenda nikupe shuhuda na kukuomba pia uamini na ufanyie kazi kuwa hii kitu IPO.

Nakumbuka wakati nikiwa mdogo huko kijijini kwetu (....) Mkoa wa pwani. "Kijiji kimezungukwa na mito, vichaka mabonde na misitu mikubwa.
Kulikuwa na kawaida ya kupotea kwa watu mara kwa mara huku imani ya wengi ikiwa ni wachawi ndo wahusika wa kupotea kwa watu. Na hii nahisi wenda si kijijini kwetu tu bali hata kijijini kwenu wenda kuna haka ka tabia ka kupotea kwa watu ila niseme tuu sio watu wote wanapotelea kwa wachawi ila baadhi yao ni time travel. kwanini nasema ni time tlavel iliwahi nitokea pia ilikuwa hivi;-
(Shuhuda ya kwanza)::;
mimi na vijana wenzangu tulikuwa tunakwaida ya kusaka wanyama wadogowadogo kwa kutumia mbwa. Siku moja shambani kwetu waliingia ngedere kama kawaida nikafungulia mbwa na kuanza kimbiza ngedere (tumbili) kimbiza yangu ikaishia kwenye msitu mdogo ulioko mbali kidogo. Nikafika mahali na kupumzika nakumbuka ilikuwa kama majila ya saa saba mchana kwendea saa nane nikakaa chini ya mti mmoja aina ya mtopetope na kuanza kula matunda ya mti huo. Hada kufika saa 11 jioni ndio safari ikaanza ya kurudi home ile nafika home napata taarifa kuwa nilikuwa nimepotea tena siku mbili na watu walishapiga mpaka nyanga.
nikaanza kuwaelezea na hakuna aliyeniamini kuwa nimetumia kama masaa manne tu hivi kuwa msituni wala sio siku mbili nikaenda shambani kuhakiki baadhi ya mazao waliyokuwa wameharibu ngedere siku ile ni kweli nilikuta ni mazao yaliyoalibiwa kama siku mbili zilizopita nyuma. Kwa wakati ule niliamini kweri wenda ikawa ni wachawi ila baada ya kufika JF na kukutana na hii kitu time travel. Imenifanya niamini kuwa hata hapa dunianibkuna maeneo ukifika ukitoka hapo unaeza ona umetumia dakika mbili ila ukitoka kwenye hilo eneo unakuta hata masaa saba yameahapita. Na hata kama unasaa ya kimwekumweku itakulazimu uilekebishe.
(Shuhuda ya pili)
Wakati nasoma pia shule ya msingi ilikuwa inanilazimu nilekebishe saa yangu kila ninapopita njia flani yaani saa yangu imekuwa imechelewa hata dakika tano na saa wenzie.
HITIMISHO
time travel ni yakweli na ipo na hata kuna baadhi ya maeneo hapa hapa ndani ya dunia.
 
HITIMISHO
time travel ni yakweli na ipo na hata kuna baadhi ya maeneo hapa hapa ndani ya dunia.[/SIZE][/SIZE][/SIZE]
Mate umetoa hitimishi bila hata kuweka facts about how it is possible, mimi ni muumini wa dhana hii ila mada yako na hitimisho lako halijitoshelezi.
No Einstein Rosen-bridge no time Travel...ungeenza kwanza hapo kuona ni jinsi gani tunaweza kutengeneza e.r.Bridge.
Point to ponder. unajua Gravity ndio kitu chenye spidi zaidi kuliko mwanga?
Time Travel: Je, linaweza kuwa suluhisho la kifo?
Time Heist and Time Apocalypse: Jinsi muda unavyoathiri Maisha ya ulimwengu na vilivyomo
 
Da'vinci mdogo wangu unapotelea gizani bila hata kujijua...kanuni au theory ya Albert Eistern ni maoni yake tu juu ya ufaham ya jambo hili.Jambo hili la kusafiri katika Muda ni jambo halisi na lina njia zake ambazo binaadamu hatujazivumbua..hapa ukumbuke ili tuupate muda ni lazima kuwe na mwanga(jua), kuna baadhi ya sehemu ndani ya sayari yetu hii speed ya jua hua ni zero.na maaneo hayo ndio hole za kutembea katika muda..jambo moja tu ambalo bado limefichwa na alieumba Dunia hii ni kwamba anaeingia katika sehem hizo hua hajui mpaka atakapotoka na kurudi eneo sahihi la asili la mwili..Najua wewe si muumin wa maisha baada ya kifo.ila time travel ni kionjo kidogo cha Paradise..hufi wala huzeeki na wala muda hausongi mbele....bi maana muda husimama. Na maana wanaoamini juu ya malipo huita siku ya "Mwisho",
 
Mwaka 2002 mjomba wngu alikuw anaendesha magari makubwa, akiwa ametoka kukusanya mzigo wa kahawa akiwa na konda wake, walifika sehemu akaegesha gari pembeni ilikuwa usiku akaenda chimba dawa. Kwenye gari alikuwa kaambatana na tingo wake. Tingo alisubiri jamaa hakurejea. Ikabidi aanze kumtafuta akamtafuta sana vichakani akaita lakini jamaa hakuwepo. Yani ni kama vile e just vanished into thin air without a trace.
Kesho yake habari zikafika nyumbani, na kwa mke wake kazini na kwa marafiki pamoja na vyombo vya dola. Alitafutwa sana lakini hakuwahi kupatikana kabisa mpaka baadae msako ukakoma maana hakukuwa na habari yake kabisa.
Ikapita miaka 3, ndipo habari ikaja kuwa kapatikana. Ajabu alikuwa kavaa nguo zile zile alizopotea kavaa na hazijachakaa, ni kama vile yuko vile vile, kuanzia nywele zake ziko kama zilivyokuwa yuko kama alivyokuwa wakati anapotea.
Jambo la kushangaza yeye alikuwa anadai kapaki gari kaenda chimba dawa karudi hakulikuta ndipo akaanza tembea tembea barabarani kulitafuta mpaka alipokutana na wananchi wakamsaidia kumfikisha serikali ya kijiji. Kwake ilikuwa ni tukio la muda mchache hakujua kama kapotea miaka mitatu.
Hakuna aliyeweza kuelewa nini kinaendelea, watu wakahusisha na ushirikina. Na bahati mbaya alifariki kwa kuugua baad ya miaka miwili toka apatikane.
Sijui nini kilitokea mpaka leo hakuna anayeelewa.
 
Sijui nini kilitokea mpaka leo hakuna anayeelewa
Labda ulimwengu tuliopo ni simulation, na time inaexist ndani ya hii simulation only. hivyo kuna sehemu ambazo zina glitch inapelekea ukifika hapo unakuwa kama upo nje ya simulation bila kujua. Na kama nje ya simulation hakuna time hivyo kila kitu hubaki kama kilivyo, ukirudi ndani ya simulation utakuta time inaendelea kama ilivyo.
 
Ndiyo commet niliyo comment kwa jamaa juzi, ni kamwambia ni kama vile movie ya matrix
 
mttupolli kwa mujibu wa maelezo yako ni kwamba ulifungulia mbwa sasa wakati unarudi ulirudi na mbwa au ulikuwa peke yako..?
Hebu toa ufafanuzi kuhusu hao mbwa au wenyewe walifukuza kisha wakarudi je,hukuwaona wakiwa wanarudi..? Nataka useme kuhusu hao mbwa.
 
Mwaka 2002 mjomba wngu alikuw anaendesha magari makubwa, akiwa ametoka kukusanya mzigo wa kahawa akiwa na konda wake, walifika sehemu akaegesha gari pembeni ilikuwa usiku akaenda chimba dawa. Kwenye gari alikuwa kaambatana na tingo wake. Tingo alisubiri jamaa hakurejea. Ikabidi aanze kumtafuta akamtafuta sana vichakani akaita lakini jamaa hakuwepo. Yani ni kama vile e just vanished into thin air without a trace.
Kesho yake habari zikafika nyumbani, na kwa mke wake kazini na kwa marafiki pamoja na vyombo vya dola. Alitafutwa sana lakini hakuwahi kupatikana kabisa mpaka baadae msako ukakoma maana hakukuwa na habari yake kabisa.
Ikapita miaka 3, ndipo habari ikaja kuwa kapatikana. Ajabu alikuwa kavaa nguo zile zile alizopotea kavaa na hazijachakaa, ni kama vile yuko vile vile, kuanzia nywele zake ziko kama zilivyokuwa yuko kama alivyokuwa wakati anapotea.
Jambo la kushangaza yeye alikuwa anadai kapaki gari kaenda chimba dawa karudi hakulikuta ndipo akaanza tembea tembea barabarani kulitafuta mpaka alipokutana na wananchi wakamsaidia kumfikisha serikali ya kijiji. Kwake ilikuwa ni tukio la muda mchache hakujua kama kapotea miaka mitatu.
Hakuna aliyeweza kuelewa nini kinaendelea, watu wakahusisha na ushirikina. Na bahati mbaya alifariki kwa kuugua baad ya miaka miwili toka apatikane.
Sijui nini kilitokea mpaka leo hakuna anayeelewa.
Tukio lilitukia usiku wakati ye anarudi kutoka kuchimba dawa alisimulia ilikuwa ni usiku uleule au ilikuwaje..?
Hakusimulia tofauti yoyote aliyoiona..?
 
Na hapa ndo maajabu ya hii kitu yanapoanzia yaani wewe muhisika mwenyewe unajikuta umetumia kama dakika 3 tu hivi ila walimwengu wengine ni zaidi ya hizo dakika tatu.
 
mttupolli kwa mujibu wa maelezo yako ni kwamba ulifungulia mbwa sasa wakati unarudi ulirudi na mbwa au ulikuwa peke yako..?
Hebu toa ufafanuzi kuhusu hao mbwa au wenyewe walifukuza kisha wakarudi je,hukuwaona wakiwa wanarudi..? Nataka useme kuhusu hao mbwa.
Nilirudi na dogs wangu wote watatu tena kama tulivyoenda
 
Tukio lilitukia usiku wakati ye anarudi kutoka kuchimba dawa alisimulia ilikuwa ni usiku uleule au ilikuwaje..?
Hakusimulia tofauti yoyote aliyoiona..?
Mkuu ukisoma vizuri nimeeleza kuwa yeye alipopatiakana alikuwa anaona kama vile tingo aliondoka na gari baada ya yeye kwenda kuchimba dawa, kwake yeye lilikuwa ni tukio la masaa kadhaa mpaka kupatikana kwake. Alipopotea tingo hakuwa na uwezo wakuendesha lile scania alimtafuta, akalala pale mpaka asubuhi aktoa taarifa kijiji walipokuwa akasaidiwa kumtafuta na habari ikatumwa ofisini na kwa familia pamoja na polisi, wakatuma dereva aende chukua gari, ndugu na askari wakaenda kusaidia kumtafuta.
Hakupatikana na hakukuwa na habari juu yake.
Baada ya muda basi tuka assume alikufa labda alibebwa na mnyama mkali tukatoa sadaka ikaisha. Then baada ya miaka mitatu anapatikana eneo karibia na alikopotea akiwa vile vile anahangaika akiwa anadhani tingo akakimbia na gari tena alikuwa yeey hofu yake ni kwamba akiliangusha gari la kazini kibarua kitaota nyasi.
 
Nachotaka kujua alitoka kuchimba dawa ikiwa ni mazingira ya usiku au..??
Mkuu hakuwasimulia kuwa aidha alipata walakini wowote ule..?
 
Kutoka 2020 uende kuishi maisha ya 2050 hapa ndipo utata unapokuja..
Au utoke 2020 uende kuishi maisha ya mwaka 1990 hapa ndipo utata unapokuja.

Sent from my SM-G928F using JamiiForums mobile app
Tunayoyafahamu katika dunia ni machache mno ukilinganisha na tusiyoyafahamu. Vitabu vya dini vinasibitisha hilo.
Na hata katika qur-ani kuna kisa cha swaaba mmoja aliwahi pia enda sehemu nahisi ni mbinguni ila sikumbuki vizuri yeye alitumia siku moja ila alirudi na kukuta watu wameishi miaka 70
 
Nachotaka kujua alitoka kuchimba dawa ikiwa ni mazingira ya usiku au..??
Mkuu hakuwasimulia kuwa aidha alipata walakini wowote ule..?
Alipotea usiku. Hakuna, yeye anachokumbuka ni kwamba alienda chimba dawa akamaliza akarudi akakuta gari hakuna akaanza tembea anahangaika kulitafuta akidani tingo kajikuta dereva
 
Naomba niingie kwenye maada mojakwamoja,

Ni baada ya kupitia mijadala kadhaa ya kitu kinachoitwa time travel nimeona watu wengi wakipingana na hii kitu, mimi binafsi bila ya lengo ya kujinufaida na faida yeyote ile napenda nikupe shuhuda na kukuomba pia uamini na ufanyie kazi kuwa hii kitu IPO.

Nakumbuka wakati nikiwa mdogo huko kijijini kwetu (....) Mkoa wa pwani. "Kijiji kimezungukwa na mito, vichaka mabonde na misitu mikubwa.
Kulikuwa na kawaida ya kupotea kwa watu mara kwa mara huku imani ya wengi ikiwa ni wachawi ndo wahusika wa kupotea kwa watu. Na hii nahisi wenda si kijijini kwetu tu bali hata kijijini kwenu wenda kuna haka ka tabia ka kupotea kwa watu ila niseme tuu sio watu wote wanapotelea kwa wachawi ila baadhi yao ni time travel. kwanini nasema ni time tlavel iliwahi nitokea pia ilikuwa hivi;-
(Shuhuda ya kwanza)::;
mimi na vijana wenzangu tulikuwa tunakwaida ya kusaka wanyama wadogowadogo kwa kutumia mbwa. Siku moja shambani kwetu waliingia ngedere kama kawaida nikafungulia mbwa na kuanza kimbiza ngedere (tumbili) kimbiza yangu ikaishia kwenye msitu mdogo ulioko mbali kidogo. Nikafika mahali na kupumzika nakumbuka ilikuwa kama majila ya saa saba mchana kwendea saa nane nikakaa chini ya mti mmoja aina ya mtopetope na kuanza kula matunda ya mti huo. Hada kufika saa 11 jioni ndio safari ikaanza ya kurudi home ile nafika home napata taarifa kuwa nilikuwa nimepotea tena siku mbili na watu walishapiga mpaka nyanga.
nikaanza kuwaelezea na hakuna aliyeniamini kuwa nimetumia kama masaa manne tu hivi kuwa msituni wala sio siku mbili nikaenda shambani kuhakiki baadhi ya mazao waliyokuwa wameharibu ngedere siku ile ni kweli nilikuta ni mazao yaliyoalibiwa kama siku mbili zilizopita nyuma. Kwa wakati ule niliamini kweri wenda ikawa ni wachawi ila baada ya kufika JF na kukutana na hii kitu time travel. Imenifanya niamini kuwa hata hapa dunianibkuna maeneo ukifika ukitoka hapo unaeza ona umetumia dakika mbili ila ukitoka kwenye hilo eneo unakuta hata masaa saba yameahapita. Na hata kama unasaa ya kimwekumweku itakulazimu uilekebishe.
(Shuhuda ya pili)
Wakati nasoma pia shule ya msingi ilikuwa inanilazimu nilekebishe saa yangu kila ninapopita njia flani yaani saa yangu imekuwa imechelewa hata dakika tano na saa wenzie.
HITIMISHO
time travel ni yakweli na ipo na hata kuna baadhi ya maeneo hapa hapa ndani ya dunia.
Hiyo ya kwenda kuwinda wanyama na kuchelewa kurudi nyumbani haiwezi kuwa time travel wewe sema ulikuwa umesinzia vichakani ulivyoamka ukapata wazo la kurudi nyumbani.
 
Back
Top Bottom