Ushauri: Mahari ifutwe?

Ushauri: Mahari ifutwe?

Katika maisha tujifunze kuwa watu wa mabadiliko na sio watu wa kukomaa na misimamo isiyo na tija kwakuwa misimamo ya namna hii huwa inagharimu sana

Kuna mzee mmoja ana mabinti watano hakubahatika kupata kijana wa kiume sasa kama unavyojua maisha ikatokea siku ya siku binti yake mmoja akaja kuchumbiwa pale nyumbani kama ilivyo ada ya mila zetu za kiafrika alitumwa mshenga na barua ya posa kuja kuchumbia wazazi wakaipokea vizuri. Babaye wa kijana ikabidi siku aende kumtolea mahari kijana wake akapokewa vizuri kabisa. Katika mazungumzo wazazi wa binti wakafikia kuwa wanataka mahari itoke jumla Milioni 4 hapo ndo mvutano ukaanza mzee ana milioni 3 katika kuongea ongea pale ghafla yule mzee aliekuwa analeta mahari akaanguka kutokana na jazba akapata mshtuko presha ikapanda kumuwahisha hospitali wakaambiwa ameshafariki.

Sasa badala ya kuwaza ndoa ghafla ikaanza mipango ya msiba. Kila mtu aliesimuliwa ule mkasa alichukizwa na kushangazwa ni kwa muda mfupi kiasi gani tamu inaweza geuka chungu, furaha inaweza ikageuka huzuni.

Basi kila mtu akaogopa kwenda kuchumbia mabinti wa yule familia ile kutokana na yalyotokea mwishowe mabinti wake waliishia kutoroshwa na wanaume na kutokomea kusipojulikana na hata hawakutaka mawasiliano na nyumbani kwao

Ukiangalia sababu kubwa ya yule familia ile kudai milion 4 ni kisa jirani yao aliozesha binti kwa milion tatu kwahiyo alitaka amfunike tu. Tazama bint anavyotumika kama bidhaa

Wito wangu ifike mahala haya masuala ya wazazi kupanga mahari yapigwe marufuku kama mzazi usitegemee kupata malipo kwa kumlea bint yako pindi anapoolewa basi ukaanza kumtwisha kijana anaeanza kutafuta maisha gharama asizoziweza. Mahari iwe tu kma ishara ya kuridhia pokea chochote utacholetewa na Mungu atakubariki
 
Kuna watu sijui mmeokotwa hamjazaliwa yaani kwa mfano kama mimi mdogo wangu wa kike nimsomeshe halafu kamaliza anataka kuolewa aende bure jamaa linamzalisha watoto watatu linamuacha anarudi tena mzigo wa kulea unakuwa tena kwetu mtoa mada una dada au ndugu wa kike kweli.
 
Kwahiyo kwa akili zako kusomesha ndio kibari cha mzazi kuomba Mahari?
 
Habari!
Hii mada imejadiliwa mara nyingi na sehemu nyingi.
Je, Mahari inayotolewa ili kijana aozeshwe ifutwe?
Kama ifutwe toa sababu, kama uendelee toa sababu.
Mbona haujatoka sababu za kwanini huo utaratibu ufutwe?? Kinyume chake unataka sababu za kwanini uendelee??? Shusha hoja zako ili ueleweke na kama hauna uwezo WA kulipa mahar sema usaidiwe
 
Kuna watu sijui mmeokotwa hamjazaliwa yaani kwa mfano kama mimi mdogo wangu wa kike nimsomeshe halafu kamaliza anataka kuolewa aende bure jamaa linamzalisha watoto watatu linamuacha anarudi tena mzigo wa kulea unakuwa tena kwetu mtoa mada una dada au ndugu wa kike kweli.
Tukimtia mimba hapo kwako utatupa bure tu
 
Mbona haujatoka sababu za kwanini huo utaratibu ufutwe?? Kinyume chake unataka sababu za kwanini uendelee??? Shusha hoja zako ili ueleweke na kama hauna uwezo WA kulipa mahar sema usaidiwe
Mahari ifutwe, hata waliotuletea huo utaratibu ambao ni Wazungu wameuacha.
 
Mahari ifutwe na wanawake wakishaolewa no kuzaa.mmechukuana Ili mlane
 
Habari!

Hii mada imejadiliwa mara nyingi na sehemu nyingi.

Je, Mahari inayotolewa ili kijana aozeshwe ifutwe?

Kama ifutwe toa sababu, kama uendelee toa sababu.
Mahali iongezwe. Vijana wajitume kufanya kazi, wajue kabisa bila chambi chambi hawapati jiko 😁😁
 
Kuna watu sijui mmeokotwa hamjazaliwa yaani kwa mfano kama mimi mdogo wangu wa kike nimsomeshe halafu kamaliza anataka kuolewa aende bure jamaa linamzalisha watoto watatu linamuacha anarudi tena mzigo wa kulea unakuwa tena kwetu mtoa mada una dada au ndugu wa kike kweli.
Ulilazimishwa kumsomesha? Hata mzazi hategemei malipo yeyote kuanzia kumleta na kumsomesha mwanae kwa sababu ni wajibu kwani Kuna ulazima gani wa kumzaa mtoto dunia kama huna uwezo wa kumuhudumia?
 
Kuna watu sijui mmeokotwa hamjazaliwa yaani kwa mfano kama mimi mdogo wangu wa kike nimsomeshe halafu kamaliza anataka kuolewa aende bure jamaa linamzalisha watoto watatu linamuacha anarudi tena mzigo wa kulea unakuwa tena kwetu mtoa mada una dada au ndugu wa kike kweli.
Huu utetezi wako wa hovyo Sana.
 
Mimi naona huo utaratibu uendelee kuwepo ili wajinga waendelee kupigwa.

Yaan umempa heshima mwanamke na bado umewaondolea mzigo bado unamtunza tena ulipe hela za kumchukua huo ni ujinga.

Nasema hivi mahali isizidi laki 3,ikizidi hapo ni wizi mtupu.
 
Ni Mila na Desturi tu kuonyesha heshima fulani....!
Huko India hasa ya Kusini familia ya binti ndo hutoa mahari..!
Hivyo iendelee Lkn hakuna haja kuifanya Kubwa.
 
Back
Top Bottom