Katika maisha tujifunze kuwa watu wa mabadiliko na sio watu wa kukomaa na misimamo isiyo na tija kwakuwa misimamo ya namna hii huwa inagharimu sana
Kuna mzee mmoja ana mabinti watano hakubahatika kupata kijana wa kiume sasa kama unavyojua maisha ikatokea siku ya siku binti yake mmoja akaja kuchumbiwa pale nyumbani kama ilivyo ada ya mila zetu za kiafrika alitumwa mshenga na barua ya posa kuja kuchumbia wazazi wakaipokea vizuri. Babaye wa kijana ikabidi siku aende kumtolea mahari kijana wake akapokewa vizuri kabisa. Katika mazungumzo wazazi wa binti wakafikia kuwa wanataka mahari itoke jumla Milioni 4 hapo ndo mvutano ukaanza mzee ana milioni 3 katika kuongea ongea pale ghafla yule mzee aliekuwa analeta mahari akaanguka kutokana na jazba akapata mshtuko presha ikapanda kumuwahisha hospitali wakaambiwa ameshafariki.
Sasa badala ya kuwaza ndoa ghafla ikaanza mipango ya msiba. Kila mtu aliesimuliwa ule mkasa alichukizwa na kushangazwa ni kwa muda mfupi kiasi gani tamu inaweza geuka chungu, furaha inaweza ikageuka huzuni.
Basi kila mtu akaogopa kwenda kuchumbia mabinti wa yule familia ile kutokana na yalyotokea mwishowe mabinti wake waliishia kutoroshwa na wanaume na kutokomea kusipojulikana na hata hawakutaka mawasiliano na nyumbani kwao
Ukiangalia sababu kubwa ya yule familia ile kudai milion 4 ni kisa jirani yao aliozesha binti kwa milion tatu kwahiyo alitaka amfunike tu. Tazama bint anavyotumika kama bidhaa
Wito wangu ifike mahala haya masuala ya wazazi kupanga mahari yapigwe marufuku kama mzazi usitegemee kupata malipo kwa kumlea bint yako pindi anapoolewa basi ukaanza kumtwisha kijana anaeanza kutafuta maisha gharama asizoziweza. Mahari iwe tu kma ishara ya kuridhia pokea chochote utacholetewa na Mungu atakubariki