Ushauri, Maoni, Mapendekezo na Pongezi kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar, Paul Makonda

Ushauri, Maoni, Mapendekezo na Pongezi kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar, Paul Makonda

Mheshimiwa RC Makonda wewe ni Governor. Unajukumu kubwa sana la kuking'arisha kioo chetu cha mji wetu wa Dar es salaam kipendeze. Jiji la Dar es salaam ni himaya yako ya utawala na ni mategemeo yangu kuona kuwa unalifanya jiji letu liwe safi na la mfano nchini na Afrika mashariki na kati.

Natambua jitihada zako ambazo mpaka sasa umezionyesha kwa wananchi wako wa Dar es salaam na napenda kwa dhati kabisa kukupa pongezi kubwa sana kwa hayo. Zaidi ya hayo yote Mh. RC Makonda mimi binafsi bado naona una fursa kubwa sana ya kuliboresha jiji letu.

Dar es salaam ni mji ambao una kabiliana na changamoto kubwa sana. Changamoto ya kwanza ambayo inatakiwa ipewe kipao mbele ni kupanuka kwa mji. Kulingana na idadi ya wakazi inavyo ongezea kila mwaka exponentially naona serikali na wewe mwenyewe Mh. RC Makonda ukiwa mtawala na msimamizi wa miradi yote ya maendeleo katika jiji lako ufanisi wake siku hizi kidogo unatia utata. Speed na njia zinazo tumika katika kukabiliana na hili tatizo naona bado ni ndogo. Tunako kwenda tutakuwa na shida kubwa sana ya kukabiliana na tatizo la ajira kwa vijana wetu kwa speed hii nasikitika kukuambia kuwa hatuta weza fanikiwa kipindi hiki cha Rais Magufuli.

Mheshimia umekuwa mzungumzaji sana badala ya kuwa mtendaji. Ndiyo nakubali umesaidia sana katika kujaribu kuwaletea wakazi wa Dar es salaam ahueni wa maisha lakini jitihada hizo peke yake hazitoshi kiongozi wangu. Jiji la Dar es salaam ambalo lina wakazi wengi kuliko miji mingibe Tanazania linahitaji Dynamic kubwa ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo. Tunahitaji turbo Speed kuweza kuikabili changamoto hii.

Ili kukabiliana na hali ya kupanuka kwa jiji kulingana na idadi ya watu wanao ongezeka exponantially inabidi radical measures zichukuliwe kwa haraka sana. Biashara ya kuuza viwanja bila maeneo kuwa na infrastructure nzuri ya mitaa/barabara, energy (umeme/natural Gas pipes), fresh water pipes na sewerage system ya uhakika, ningeshauri istopishwe badala yake serikali i-concetrate na kuboresha mji kwa kujenga nyumba nyingi za gorofa na kuwauzia au kuwapangisha wakazi wa Dar es salaam kama, Rais Magufuli alivyo fanya kwenye Magorofa ya Magomeni Quarters, ili pia kutoa nafasi kubwa za Parks ambazo wakazi wa Dar wanaweza wakawa wanazitumia kwa mapunziko na vijana kufanya michezo mbali mbali kama mpira na kadhalika kama Central Park in New York au Volks Garten in Berlin in Germany.

Challenge ya pili ni ajira. Ajira ni changamoto ambayo nchi nyingi inamatatizo nayo makubwa na utatuaji wake hapa ina hitaji ubunifu mkubwa wa miradi mbali mbali mikubwa na kusimamia utekelezaji wake, kwa kutoa mfano tu hapa sewarage system na taka.

Dar es salaam Mh. Makonda unahitaji mabadiliko makubwa na usimamizi wa hali ya juu wa Systems. Mambo ya uchimbaji wa vyoo au kutumia vyoo vya mashimo na kuyaacha maji machafu yaende baharini bila kusafishwa tuachane nao. Hizi systems mbili zikichukuliwa umakini na kuzijengea utaratibu vijana wengi sana watapata ajira. Mh. Makonda katika kukabiliana na changamoto hii dhamira kubwa na mpango wa mda mrefu unahitajika. Hizi ni projects kubwa na ambazo zinahitaji pesa nyingi kidogo, lakini faida yake ni kukabiliana na swala la ajira na mabadiliko ya jiji.

Mh. Makonda wewe ndiyo kiongozi na wewe ndiyo msimamizi and people gonna hold you accountable for that. Kwa hiyo ili ujenge legacy nzuri inabidi kazi kubwa ifanyike katika ku impliment hii miradi ambayo itabadilisha sura ya jiji letu na kuwa mfano kwa miji mingine. Katika kutatua tatizo la maji machafu sewarage system kubwa inabidi itengenezwe na kazi ifanyike na matokeo yaonekane na sio tu kutuonyesha sisi Computer Animation ya wishes ambazo unazo. Watu wanataka Action.

Mh. Makonda katika kujadili miradi kama hii piga tarumbeta ya kukutana na wataalam wote ambao wako jijini na agenda kubwa iwe kupata mawazo tofauti ya vijana kwa wazee jinsi ya kuboresha sura ya mji na kukabiliana na swala la ajira. Nina uhakika tutapata mengi ya kusikia, haya na mengine kutoka kwa Diaspora yatatuwezesha sisi kuwa na msimamo wa kupata mahali pa kuanzia.

Mimi nashangaa sana, Mh. mwenye majukumu na uwezo mkubwa kama wewe RC Makonda unapoteza mda na nguvu nyingi ku deal na wasanii na viongozi wa dini ambao hawasaidii jamii kwa kiasi kikubwa sana cha kutatua tatizo la ajira la vijana wetu mbali na kutaka hela kwa ajili ya binafsi zao upande wa wasanii na viongozi wa dini kutoa faraja za kiroho, zaidi ya hayo hakuna. Hawana vision ya kukabiliana na challenge ya ajira zaidi ya kukusifu tu. Sasa wewe Mh. Makonda sifa zitakupa nini? Challenge ya kukabiliana na ajira ni ku-finance miradi mikubwa ambayo in the long run italipa kwa kubadilisha sura ya jiji letu na watu kuwa na kipato cha uhakika cha maisha.

Mh. Makonda kuwa pioneer katika kubuni na kutekeleza na sio kuwa champion katika siasa. Hayo waachie wengine, wewe tekeleza wajibu wako ambao Rais Magufuli amekukabidhi. Usi shangilie tu kujengwa kwa Standard gauge bali kuwa mwenyewe active katika kuhakikisha mji wako unakwenda sambamba na mahitaji ya leo mji au jiji linavyotakiwa liwe.

Shirikiana na mawaziri wano husika na wadau wengine ambao wanaweza kutoa pesa zao na kuwekeza katika miradi wakiwa kama share Holders, kama Mo Dewji na wengineo.

Elb Philharmoniker ya Hamburg ujerumani, serikali na matajiri wa huo mji kama Happag Lloyd na wengine walihusika kulijenga hilo jengo lao la concert kwa kutoa michango yao. Hivi sasa limekuwa Tourist Attraction kwa ma-tuorist wengi kutoka nchi mbali mbali za ulimwengu. Kwa mda mfupi baada ya hilo jengo kwisha gharama zilirudi na hivi sasa wanapata faida tu. Kwa hiyo utaona investiments zao zimelipa na vile vile sura ya mji wao imebadilika na kupitia Tourist Business watu wamepata ajira na maisha kuendelea.

Na sisi Mh. Makonda tunatakiwa tuwe wabunifu na kuwa tayari kuingia risk ya kugharamia miradi ambayo itabadili sura ya mji wetu na vile vile kuboresha manzingira ya kufanya biashara na kuishi.

Unachofanya kuwasaidia wasanii kwa mikopo ya bila riba na kujenga ukumbi au Sport Center kwa ajili ya jamii ni kitu kizuri sana, lakini peke yake nasikitika hakitatosha. Mh. Makonda una nafasi nzuri na kubwa sana ya kubadilisha Dar es salaam yetu na sio tu kwa majengo bali pia kwa vitu ambavyo vita wa attract tourists. Hofu yangu kubwa ni kwamba wewe mda mrefu huna wa kuanza na projects hizo. Mh. Makonda uko slow sana katika ku-impliment projects na uzalishaji wa ajira. Usipo fanya wewe hivi sasa sina uhakika kama Dar es salaam itampata kiongozi mwingine kama wewe na Rais ambaye yuko tayari kwa mawazo mengi kama Magufuli, haraka.

Mapendekezo yangu ya kufanya Mkuu wa mkoa wetu ili kulikabili hili janga ambalo linatishia amani yetu in the near future ni kama ifuatavyo ;

1. Tekeleza na kusimamia miradi yote uliyo kusidia mpaka sasa, kama Stand ya mabasi ya kwenda mikoani Ubungo, masoko yote yaboreshwe na soko la Kariakoo ndio kabisa ili kuondoa msongamano wa watu na magari. Usimamizi wa hii miradi uwe wa makini sana kama mradi wa Standard Gauge.

2. Himiza usambazaji wa energy umeme na mabomba ya Gas asilia jijini ili wananchi waache kabisa utegemeaji wa kuni na mkaa ambao kwa namna moja au nyingine kuharibu manzingira yetu kwa haraka kwa kushirikiana na wizara husika na ikibidi mvae Rais mwenyewe. Katika usambazaji wa pipe lines za gas asilia kuna ajira zitatengenezwa katika usambazaji, Monitoring na mounting.

3. Finance ya mitalo mikubwa ya maji machafu ya chini ya ardhi na waste water treatment plants za kusafisha maji machafu kabla ya kwenda baharini. Angalia clips please;


Hapa pia wafanya kazi waajiriwe kwa ajili ya kusafisha beach zetu. Watumie vyombo vya kisasa. Mpaka waturuki wanatuonyesha jinsi ya kusafisha fukwe zetu jamani hata haibu hatuna? Mh. Makonda na wengine mko wapi? Na mnafanya nini? Kazi kuimba nyimbo za ajira tu wakati hizo ndiyo ajira zenyewe.

Waste water kutoka nyumba za watu ndiyo hufanya fuko za bahari yetu kuwa chafu na kunuka. Tukisafisha maji yanayo pitia Jangwani, Ananasif, Mbagara mtoni na Mbezi Beach, fukwe zetu hazitakuwa chafu wala kunuka tena.

4. Pale Kivukoni iwekwe Nembo yetu ya Taifa kubwa sana ya mataa kama Tourist Attraction

Kwa hili vijana mbali waalikwe na Fantasy zao ili the best ashinde.

5. Kustopisha uuzaji wa viwanja bila mpangilio wa infrastructure Dar es salaam. Serikali ijitahidi kwa kushirikiana na matajiri wetu wa nchini kujenga nyumba za gorofa kuondoa au kupunguza upanukaji wa mji kwa haraka. Nyumba zetu zinajengwa kiholela holela tu bila kufuata mpangilio.

6. Kutoka Bagamoyo mpaka City Center na kutoka Mkuranga mpaka City Center tutengeneze sisi wenyewe streets trains za umeme. Hivi ndivyo tunaweza kujenga kizazi ambacho kinajiamini na kufanya mambo chenyewe. Hatugundui Train na wala vifaa. Tunanunua tu na kuvitumia, sasa kwa nini iwe tatizo? Tupuyange tu hivyo hivyo hujajifunza I am sure!

Kwa hili tuchukue mfano kutoka kwa waziri Jaffo. Waziri Jaffo yuko safi sana. Nimesikiliza kwa makini sana maelezo yake juu ya ujenzi wa Wizara ya temisemi Dodoma. Waziri Jaffo katika ujenzi wa jengo la wizara hiyo ya gorofa tatu anatumia malighafi kutoka nchini na wajenzi ni vijana wa University of Mbeya. Nilifurahi sana nilivyosikia waziri wetu anawapa majukumu vijana wetu. Hivyo ndiyo tutajenga taifa la watu wanao jiamini kufanya mambo wenyewe baadae.

Waziri Jaffo hata kama hilo jengo li ki-cost zaidi, acha li cost tu ni hela yetu inatumika katika kuwaendeleza vijana wetu na ni watanzania ndiyo wanao nufaika. Kwa hiyo sio mbaya kabisa waziri. Hongera sana! Mungu atakubariki. Endelea hivyo hivyo waziri wetu. Wewe ni Role Model wa vizazi vyetu vya baadae waziri. Asante sana!


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Najua unapenda sana Kushughulika na kuhakikisha kuwa Jambo fulani linatendeka na linaenda unavyotaka Wewe ila kuna maeneo mengine unatakiwa upime au ujipime Kwanza hasa ukizingatia Usalama wako na jinsi Jamii Kubwa ya Watu hasa ' Maadui ' zako ulionao hapa Mkoani Dar es Salaam.

Binafsi nilishangaa sana ile Jana tena ukiwa barabarani na kuna Watu wengi wa kila aina ' ukijiachia ' kwa kutoka katika Gari yako na Kujumuika nao huku ukizunguka huku na kule pasipo na hata Wewe kuwa na jicho la pili kwa ' Usalama ' wako.

Najua unalindwa tena pengine kuliko hata wanavyolindwa ' VIP's ' wengine nchini ila binafsi nadhani kwa hali iliyopo na hasa ' Chuki ' za Watu dhidi yako ( nikimaanisha Maadui ) zako uliowatengeneza hukupashwa ' Kujiachia ' vile kwani lolote lingeweza kutokea Kwako na pengine leo tungekuwa na habari nyingine mbaya.

Mpaka sasa nawaza RC Makonda unajiamini vipi hadi unapenda ' Kujichanganya ' na Watu tena wale ' Changanyikeni Clan ' ambamo ndani yao humo kuna ambao wanakupenda na wasiokupenda pengine kama nia mbaya ingekuwepo dhidi yako jana basi ingekuwa rahisi Kwao ' Kutekeleza ' jambo lao.

Ushauri wangu Kwako Siku zingine kabla ya kwenda mahala hebu jaribu kupima ' Upepo ' Kwanza na ' Kutafakari ' kwa marefu na mapana hasa hasa ukizingatia suala zima la ' Usalama ' wako. Ila ningekuwa ni Mimi GENTAMYCINE jana ile nipo nawe kama sehemu ya ' Ulinzi ' wako kamwe nisingekuruhusu uwe unatokatoka vile katika Gari yako na kuja ' Kujichanganya ' na Watu ambao Kwanza huwajui vyema, akili zao wengine wanazijua wenyewe na wenye kuwa tayari pia kufanya lolote na kuja ' Kujutia ' baadae huku pengine Wewe ukiwa ' Mwaisela ' au ' ICU ' au umeshaungana na ' Mtani ' wangu katika ' Identity ' mpya ya Marehemu fulani.

Acha kujiamini sana na kuwa makini tafadhali. Yangu ni haya tu kwa leo na ukiona nakuambia hivi jua nakupenda na nakutakia maisha marefu na mema pia. Bado wale ' Maadui ' zako hawajalala usingizi na pia huwezi jua sasa wanajipangaje dhidi yako hivyo nawe pia yakupasha muda mwingi kuwa makini na ' Kujilinda ' huku pia ukipunguza sana kupenda ' Kuonekana ' mbele mbele. Kwani ile jana ambapo nawe ulikuwa ' Msafarani ' ungekuwa tu unatoa ' Maelekezo ' wa Watendaji wako hasa wa Kiusalama / Kiitifaki waliokuwepo pale au uliokuwa nao wasingefanya kile ulichokuwa unataka Kifanyike?

Yafanyie Kazi haya maelezo yangu ila ukiona hayakufai basi niachie tu mwenyewe.

Nawasilisha.
 
Kila siku tunakwambia una kiherehere Sana we Jamaa unaandika ili uonekane much know.kama ulitaka umpe huu ujumbe ungeonana naye.sasa umejuaje Kama yupo humu JF?sijaelewa unatuambia sisi tufanyaje wakati hatujui hata alichokifanya..wajinga wanaamini gentacymine Ni mwanausalama wa taifa kwa sababu tu mabandiko yake...najua utakuja TU kutema nyongo kwenye hi comment yangu kwa upupu uliotukuka.unatuchosha akili kwa lengo gani
 
Najua unapenda sana Kushughulika na kuhakikisha kuwa Jambo fulani linatendeka na linaenda unavyotaka Wewe ila kuna maeneo mengine unatakiwa upime au ujipime Kwanza hasa ukizingatia Usalama wako na jinsi Jamii Kubwa ya Watu hasa ' Maadui ' zako ulionao hapa Mkoani Dar es Salaam.
Sasa mtu anajiamini hana tatizo na mtu.labda watu ndo wana tatizo na yeye.

Ya nini aishi kwa mashaka mashaka na kufa mara moja tu?
 
Najua unapenda sana Kushughulika na kuhakikisha kuwa Jambo fulani linatendeka na linaenda unavyotaka Wewe ila kuna maeneo mengine unatakiwa upime au ujipime Kwanza hasa ukizingatia Usalama wako na jinsi Jamii Kubwa ya Watu hasa ' Maadui ' zako ulionao hapa Mkoani Dar es Salaam.
nilishangaa sana kuona bashite anafanya majukumu ya Askari polisi au ndo kusema anajitakatisha?
 
Jazia nyama mkuu, wengine hatukuona hilo tukio la mpendwa rc wetu
 
Kiazi sana wewe unadhani ungefanya lolote au angefanya lolote mtu yeyote pale angetoka? Hakuwa mwenyewe kama unavyozani ule msafara si wakisiasa kwamba zilihitajika nguvu ili kuwaondoa wananzengo pale zilihitajika busara tu.
 
Najua unapenda sana Kushughulika na kuhakikisha kuwa Jambo fulani linatendeka na linaenda unavyotaka Wewe ila kuna maeneo mengine unatakiwa upime au ujipime Kwanza hasa ukizingatia Usalama wako na jinsi Jamii Kubwa ya Watu hasa ' Maadui ' zako ulionao hapa Mkoani Dar es Salaam.

Binafsi nilishangaa sana ile Jana tena ukiwa barabarani na kuna Watu wengi wa kila aina ' ukijiachia ' kwa kutoka katika Gari yako na Kujumuika nao huku ukizunguka huku na kule pasipo na hata Wewe kuwa na jicho la pili kwa ' Usalama ' wako.

Najua unalindwa tena pengine kuliko hata wanavyolindwa ' VIP's ' wengine nchini ila binafsi nadhani kwa hali iliyopo na hasa ' Chuki ' za Watu dhidi yako ( nikimaanisha Maadui ) zako uliowatengeneza hukupashwa ' Kujiachia ' vile kwani lolote lingeweza kutokea Kwako na pengine leo tungekuwa na habari nyingine mbaya.

Mpaka sasa nawaza RC Makonda unajiamini vipi hadi unapenda ' Kujichanganya ' na Watu tena wale ' Changanyikeni Clan ' ambamo ndani yao humo kuna ambao wanakupenda na wasiokupenda pengine kama nia mbaya ingekuwepo dhidi yako jana basi ingekuwa rahisi Kwao ' Kutekeleza ' jambo lao.

Ushauri wangu Kwako Siku zingine kabla ya kwenda mahala hebu jaribu kupima ' Upepo ' Kwanza na ' Kutafakari ' kwa marefu na mapana hasa hasa ukizingatia suala zima la ' Usalama ' wako. Ila ningekuwa ni Mimi GENTAMYCINE jana ile nipo nawe kama sehemu ya ' Ulinzi ' wako kamwe nisingekuruhusu uwe unatokatoka vile katika Gari yako na kuja ' Kujichanganya ' na Watu ambao Kwanza huwajui vyema, akili zao wengine wanazijua wenyewe na wenye kuwa tayari pia kufanya lolote na kuja ' Kujutia ' baadae huku pengine Wewe ukiwa ' Mwaisela ' au ' ICU ' au umeshaungana na ' Mtani ' wangu katika ' Identity ' mpya ya Marehemu fulani.

Acha kujiamini sana na kuwa makini tafadhali. Yangu ni haya tu kwa leo na ukiona nakuambia hivi jua nakupenda na nakutakia maisha marefu na mema pia. Bado wale ' Maadui ' zako hawajalala usingizi na pia huwezi jua sasa wanajipangaje dhidi yako hivyo nawe pia yakupasha muda mwingi kuwa makini na ' Kujilinda ' huku pia ukipunguza sana kupenda ' Kuonekana ' mbele mbele. Kwani ile jana ambapo nawe ulikuwa ' Msafarani ' ungekuwa tu unatoa ' Maelekezo ' wa Watendaji wako hasa wa Kiusalama / Kiitifaki waliokuwepo pale au uliokuwa nao wasingefanya kile ulichokuwa unataka Kifanyike?

Yafanyie Kazi haya maelezo yangu ila ukiona hayakufai basi niachie tu mwenyewe.

Nawasilisha.
Nchi Yetu sio kama kwenu burundi
 
Back
Top Bottom