Ushauri, Maoni na Msaada: Kwa wanaotaka kujilipua nje ya nchi kusaka maisha, kusoma na kuwekeza


wakuu wazoefu kuna link hyo ni utapeli au kwel!?? maana ukiapply wanataka mpunga!!
 
Wakuu wa jukwaa letu pendwa tulikuwa tupo sambamba sana kupeana info za maaana ila kwa siku ya leo kuna kiumbe cha ajabu sijui kimedondoka hapa kutokea wapi? ID yake Mgaka12 I tried to argue with him earlier.


muhimu

TUSIMJIBU CHOCHOTE, WALA KUMJADILI HATA AKIPOSTI AU REPLYING COMMENTS YA MTU TUMWACHE AROPOKE UPUUZI WAKE, SISI TUFOCUS KWENYE MAMBO YETU.

kuna ishu ya udereva unahitajika nchi ya newzealand na uyaya wa ndani kama ilivyotolewa na mkuu Izzo jamani tuombeni mwongozo wa hizi kazi na mwenye nia aombe haraka.




cc Dr Adam
Stunterr
Daby
Wisegal
Kirikou
Na wengine wote, kwani Nina yetu ni moja kutafuta maisha nje ya tz huyu fala asitupotezee direction tukawaste kurasa zetu hapa kwenye nyuzi kupashana naye.
 
Nikweli huyu tumpotezee tuangalie mbele zaidi na malengo yetu kwani wajanja wanasema mpuuzi mpuuzee so huyu pia tumpuuze jaman kwa wale wenye sifa tajwa hapo juu wajitokeze japo niliona kuna mkuu mmoja ni mwenzetu alishaomba udereva nadhani hapo ni ya uyaya ndio bado lakini najua mpka kesho watajitokeza wahitaji zaidi Inshaa Allah.
 
Akipatikana wa Dom namie ntupie mmoja aseee...
 
Mkuu IZZO nakukumbusha tena ndg yangu naomba unisaidie jinsi ya kupata hio kazi ya driving in New Zea land ntakushukuru saana mkuu, vigezo vyote ulivotaja ninavyo. Ntakushukuru saana Mkuu.
 
Mkuu lusungo shukrani kwa kuleta huu uzi. izzo mkuu endelea na moyo huo huo pamoja na wadau wote mliochangia humu.

Kuna mambo nimejifunza mengi sana na kwa huu uzi nimefufua ndoto ya kwenda ulaya. Nakumbuka wakati nipo sekondari kuna wazungu walikua wanakuja shule, kipindi hicho nina upako wa kiingereza yes no what when zilikuwepo kwa wingi. Mimi sikujua kwamba ile ilikua ni fursa ya kwenda ulaya. Nimesoma huu uzi nikakumbuka kama ningejiongeza ningekua nipo huko.

Kwa kupitia nondo za huku kuna mambo nimeyagundua, kwanza ukiwa na nia utafanikiwa. Pia kwenda ulaya sio jambo kubwa sana ila mikakati ya nguvu inatakiwa.

Mkuu izzo kaleta plan za kwenda huko, kwa kupitia Malta na ku_host wageni toka ulaya. Ila kwa upande wangu nimejiwekea mpango mkakati wa miaka 2 ili nifanikiwe.. [HASHTAG]#RoadtoEurope[/HASHTAG]..!!

1. Naanza kwa kutafuta Passport, ikae tuu ndani maana ndio kitu cha muhimu. Wadau wameshaatoa njia ya kuipata naamini nitaipata.
2. Nauli, hapa ndio mziki ulipo. Nauli ndio kila kitu, lazima niitafute. Japo sina kazi ila ndani ya miaka hiyo 2 najua itaeleweka
3. Kiingereza, japo cha kuombea maji kipo ila kukiongeza zaidi inanipasa. Sio unaongea na mtu unaanza kusearch vocabulary mojamoja kichwani.
4. Scholarship, japo kwa sisi wenye diploma zinakua ngumu na chache ila nitaanza kuzitafuta kwa udi na uvumba. Zile mb za kuangalia Messi's skills au Ronaldo's skills youtube nitazitumia kutafutia scholarship.
5. Kutafuta demu mzungu aliyepo Ulaya kwa kupitia online dating sites. Najua wazungu akikupenda anakupenda kweli, akijilengesha mmoja hana bahati. Namng'ang'ania kama kupe hata kwa ndumba itabidi 😛.

Naamini Mwenyenzi Mungu atasaidia na mimi niende Ulaya siku moja, aliyewezesha wengine wawepo na mimi atanisaidia.

Wakuu msisite kutoa miongozo, mbinu, nafasi ya kutusaidia na sisi tuweze kwenda huko wanapopaita Ulaya.

[HASHTAG]#RoadtoUlaya[/HASHTAG]......🙂🙂🙂🙂
 
Britannica kaja kivingine humu naona anavokatisha watu tamaa
 
Hao warembo wa kizungu uliwapata kupitia website gani?
 

Mkuu Prishaz hao wako wachache Lakini kelele nyingi.Kitu nilicho penda kaandika kwa wale ambao watapata hizi fursa Halafu wawaharibie watanzania wakarimu Na Wazalendo.
Bila ya kutoa povu nawaomba tu wale watakao fanikiwa katika fursa hizi wakumbuke michango ya Lusungo,Izzo Na wengi walio tufungulia hii milango ya kheri Na wao wakafanya mazuri Kwa wengine.
 

Mkuu Daby
Nimekuelewa sanaaaaa tu.
Itakuwa vizuri kuandika mazuri Kwa watu wanao jitolea kutuonyesha njia ili wengi wetu tufanikiwe.Tafadhali usipoteze muda wako muhimu Kwa huyo jamaa.Anacho taka usimpe
 
South si huwa tunaruhusiwa kukaa week tatu kama skosei, sasa wewe umechukua permit ya kazi au ?
Mkuu kuhusu kipindi wanachoruhusu kukaa hata wakikuruhusu wiki mbili ww kama umeamua kwenda kutafuta maisha usijali mm nilikuwa na viza ya mwezi 1 miaka hiyo unachofanya ukifika unaenda kujilipua home affair kuomba asylum seeker usiende na passport utapata hiyo permit utakayokuwa unaenda kurenew kila baada ya miezi kadhaa kwa wakati ule unaruhusiwa kufanya kazi na kusoma unaweza kuchukua hata miaka 4 ndio uje usikilizwe kesi yako kwa ajili ya kupata status ila mara nyingine watz huwa hatupati utapewa siku za kurudi kwenu au kuapili kupinga hiyo hukumu kwa cape town tulikuwa tunaenda UCT pale kuna mawakili wanaosaidia nakumbuka baada ya kuapili nilikaa mpaka 2010 nilipoamua kuondoka mwenyewe, nadhani nitakuwa nimesaidia kidogo kama ndicho ulichotaka kujua
 
Kujikwaa siyo mwisho wa safari. Don't take it generally.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…