Nchi ipi ya kwenda ipi si ya kwenda
Tofauti ya fikra za watu kuwa Ulaya ni Ulaya, kuna nchi za Ulaya ambazo hazifai kwenda kama unatafuta maisha. Jiepushe na nchi za Ulaya mashariki kama Czech, Estonia, Hungary, Latvia, Lithuania, Poland, Slovakia, Slovenia, Bulgaria, Croatia, Romania, Ukraine na Urusi. Nchi hizi hamna kazi na mishahara yake ni midogo mno ambayo haitaweza kukusaidia kwa lolote. Watu wengi wa nchi hizi huwa wanakimbilia nchi za Ulaya magharibi. Pia ubaguzi umekithiri sana Ulaya mashariki.
Nchi nyingine za kujiepusha nazo ni nchi ambazo zilikuwa na uchumi mkubwa lakini zimeanguka kiuchumi. Nchi hizi ni Ugiriki, Italia, Ureno na Hispania. Waafrika wengi katika nchi hizi ni wauza unga au wamachinga. Raia wa nchi hizo pia wanakimbilia nchi nyingine za Ulaya.
Pia, ukienda nchi wasiyotumia Kiingereza jiepushe na kuishi miji midogo. Kwa wale wanaotaka kuja nchi za Nordic (Sweden, Denmark, Finland, Norway na Iceland) mjiepushe na kwenda kuishi miji midogo mbali na miji mikuu. Ukiishi mji mkubwa angalau unaweza ukasukuma maisha kwa Kiingereza na kazi pia zipo. Ukienda vijijini huko hamna kazi na kuishi bila kuongea lugha ya hapo ni ngumu. Vijijini pia ubaguzi upo kwa kiwango cha juu ukilinganisha na mijini.