Mbona husemi ukweli? Kuna ubaguzi wa rangi, kuna ugumu wa lugha, Europe nzima Sasa kuna tension hawataki wageni, pa kufikia wapi, kuowa kwa makakatasi kunataka pesa za kutosha. Nchi nyingine za uralaya kama Uingereza mgeni haruhusiwi kuolewa ama kuowa mpaka ruhusa kutoka immigration, na hata kama ukipata ruhusa, kupata ruhusa ya kuishi inabidi anayekuowa ama unayemuowa lazima awe anafanya kazi na mushahara wake usiwe chine ya £18,000 kwa Mwaka, kwa hiyo kumpata mtu mwenye kipato hicho nawe lazima uwe umejipanga. Lazima usiwe mvivu, Watanzania wanajulikana kwa uvivu. Maisha sasa ni Afrika ndiko kwenye uchumi unakuwa. Kukimbilia sio solution, Europe Wafrika wengi wana kazi haswa wenye kusoma cha chini na lugha shida. Simkatishi yeyote tamaa, mwenye kutaka kujaribu aendelee, lakini ujuwe kuna shida nyingi sana.