Ushauri, Maoni na Msaada: Kwa wanaotaka kujilipua nje ya nchi kusaka maisha, kusoma na kuwekeza

[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Mkuu lusungo asante kwa uzi mzuri,nilikuwa najaribu kupitia maswaibu gani wanayapata wanaopitia libya siliti,kule jangwani hakufai mfano gari ikizingua mnakufa mnakaukia hapo hapo,pia kunyang'anywa pesa ni rahisi,pia wale watu wenye zile gari zinazobeba wanaojilipua(wanaoenda ng'ambo) nasikia ni makatili balaa ukipata tatizo njiani wanakutupa jangwani,pia wanakuwa wamejaa kwenye zile gari kwa hiyo kuna wanaodondoka njiani wanawaacha mfano kwa hili gari hapo chini lilipata hitilafu wote wakafia hapo jangwani
 
Duh mbona wamekaukiana hivyo?
 
Ndio maana tunataka subforum ya diaspora
Hivi kueleza hapa mbinu aliyotumia kupata visa kinazuia nini? Huu ni uzi mahsusi kwa hilo ina maana isubiriwe hiyo forum ya diaspora? Why wabongo tupo hivi?

Nini kinakuzuia kuandika hapa ulichokusudia kukiandika huko sub forum ya diaspora? So watu wanaohitaji huo msaada sasa wasubiri hadi iletwe hiyo sub forum?
 
Ina maana izi safari hawakujipanga na vp kuhusu mawasiliano ya Simu hawakubeba spea kama gari ikizingua hawakubeba misosi je???? Ila wamekufa vibaya sana
 

Australia ni tofauti sana, km unasoma kwa miez18 au zaid ukimaliza unapewa 18months to find a job na visa inakua (bridging visa) so unapata muda wa kusaka job. Most paying jobs ni hospitality mpk $56/hr
 
Denmark ni nchi ya scandinavia... Ni nchi yenye maisha ya raha na amani sana japo ni nchi ndogo... Njia rahisi kwenda huko unaweza kwenda as tourist then ukifika huko unapambana upate wa kumwoa hata kwa makaratasi tu ili upate kibali cha ukaazi.

Mbona husemi ukweli? Kuna ubaguzi wa rangi, kuna ugumu wa lugha, Europe nzima Sasa kuna tension hawataki wageni, pa kufikia wapi, kuowa kwa makakatasi kunataka pesa za kutosha. Nchi nyingine za uralaya kama Uingereza mgeni haruhusiwi kuolewa ama kuowa mpaka ruhusa kutoka immigration, na hata kama ukipata ruhusa, kupata ruhusa ya kuishi inabidi anayekuowa ama unayemuowa lazima awe anafanya kazi na mushahara wake usiwe chine ya £18,000 kwa Mwaka, kwa hiyo kumpata mtu mwenye kipato hicho nawe lazima uwe umejipanga. Lazima usiwe mvivu, Watanzania wanajulikana kwa uvivu. Maisha sasa ni Afrika ndiko kwenye uchumi unakuwa. Kukimbilia sio solution, Europe Wafrika wengi wana kazi haswa wenye kusoma cha chini na lugha shida. Simkatishi yeyote tamaa, mwenye kutaka kujaribu aendelee, lakini ujuwe kuna shida nyingi sana.
 

Nimegundua wengi hawana taarifa vyema khs chimbo la Oz nitadadavua baadae
 
Sijakuelewa ktk hicho ulichoniquote sijasema ukweli kuhusu nini!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…