Ushauri, Maoni na Msaada: Kwa wanaotaka kujilipua nje ya nchi kusaka maisha, kusoma na kuwekeza

Mkuu lusungo una moyo wa ajabu sana, siyo wote wana moyo wa namna hii, hiu nia uliyo nayo kusaidia waTz wenzako siyo asili ya watanzania wengi. Nimekuona unavyojitahidi kuwajibu wale wanao hitaji diaspora forum lakini ukweli inaonyesha wala hawana nia wala moyo ulio nao. Muhimu naona uwapuuze tu kwa sasa, wasiposema wao kuna wengine wenye moyo watasema. Zidi kubarikiwa
 
izzo nakusoma kwa utulivu mkubwa, naendelea kusema asante kwa moyo unao uonyesha na wakuu wengine pia. Naamini muda wenu hautapotea bure kuna kitu mmekipanda na lazima kitazaa matunda.
Hapo kwenye Host niko tayari sana.
Siku zote mm napenda sana kama mna kitu mnafanya bhasi matokeo yaonekane japo kidogo tatizo Watanganyika mnapenda story story sana hilo ndio tatizo kubwa sana kwa Dunia ya leo hatuwezi kujaza saver za JF kwa story story tu mpaka leo hakuna hata mrejesho hata wa aliyekwenda ubalozi wa Italy japo kuuliza tu michakato ya visa tu nothing host ni wawili tu walionyesha nia so unadhani tunafanya nini hapa sasa ?????
 
Mkuu izzo naomba usome comment yangu juu hapo
 
izzo nakuelewa sana,mimi natamani nirudi hata leo tz nianze michakato ila nina contract ya kazi imenibana mpaka mwezi wa 7 ntarudi tz.
wabongo wanapenda stori lakini kufanyia kazi ni suala jingine.
Kuna ndugu nmempa mpango mzima wa kwenda Malta kutafuta maisha na nauli ntamuazima kanijibu nisubiri atafikiria wakati anakaa nyumbani hana kazi wala nini,anakaa kwenye tv 25 hours..
 
Ndio maana nasema nitakuwa sitendi haki kwa akili yangu kuweka maproject hapa ambayo hayafanyiwi kazi no siwezi hata kidogo kufanya hvyo
 
naomba kwenye host hapo uniweke npo serious kwa hilo i don't kno km itakuwa issue kwa tulio mikoani.,binafsi npo mwanza muda ukifka ukitaka details nitakupa..,ubarikiwe mkuu izzo..
 
Chief hii kitu nilitaman sana kuifanya ila tatizo tuko kwenye viajira vyetu inakua ngumu kidogo
 
mkuu dr adam.faida ile option yako ya kwenda Botswana November bdo ipo, au umeamua unyoke Malta moja kwa moja?
 
izzo kama umeona comment yangu hili suala nimeliongelea hapo juu. Tunaopewa ushauri tujitahidi tunayoambiwa tuyafanyie kazi la sivyo hizi zitakuwa stori kama za chit-chat.
Sipo perfect kuhusu hili ila jamani tunaoshauriwa ili washauri waendelee kutupigania lazima tuonyeshe efforts japo kidogo. Binafsi sikutaka kuexpose nilipofikia kwasasa ila kwa comment yako hii imenibidi japo nitaelezea kwa ufupi.

Kuna jamaa nilikutana naye na nafikiri nilimwelezea kule nyuma nikasema anayehitaji msaada wake anifuate ila sikuona reponse ya mtu yeyote. Huyu jamaa anadeal na visa za Canada na Europe anakutafutia visa then pia anakutafutia mbongo au mtu yeyote wa kukuhost kwa muda huku ukikamilisha mambo yako. Gharama yake ni usd 2000 ila ukiongea naye kikubwa inapungua.

So binafsi nimeamua kudeal naye ananishughulikia visa ya sweden a process zimeanza. Safari itakuwa before tareh 20 April. Kuhusu kurushwa jamaa sina mashaka naye japo binadamu sio wa kuwaamini.

Changamoto iliyopo kwake:
Ni namna ya kupata makaratasi maana napotoka huku nakuwa na schengen visa so bado nafanya mchakato wa namna ya kupata makaratasi na kuishi muda mrefu. Kuna watu nimekutana nao wananipa ramani ya kupata makaratasi lakini still michakato haijafikia hatua inayostahili ila shukrani kwao saana saana.

Gharama za jamaa ni nyingi maana hizo usd nilizotaja hapo sio kitoto.

Ombi langu kwenu kama kuna mtu anajua machimbo ya kupata papers nikishafika nishaurini ila nimeamua kujilipua April.
Msichoke kutushauri vijana wapo wanafutilia documents ila ni vizuri ndugu zangu muweke updates hapa tuwape moyo kina lusungo na izzo wanayofanya ni zaidi ya tuliyotarajia kuyapata.
 
Nitumie namba ya huyo Agent inbox
 
Haya ndio matatizo ya kukosa uzalendo. nenda Kenya hauhitaji vitu vyote hivyo. bila aibu unalilia upewe na nauli. Yaani kama unamke haushindwi kuomba wanaume wampe ujauzito.
 
Axnte mkuu!!
 
Poa mkuu karibu sana....
Kuhusu Australia aka OZ ni bonge la chimbo kwa watu ambao wameshawahi fika au wako wanafahamu nisemacho,kiukweli sio wabongo wengi wanapazungumzia hata humu kwenye jukwaa sijaona mijadala ya kuhusu kufanya plan za OZ.

Kiufupi ni kuwa OZ ni moja ya nchi za ulimwengu wa kwanza ambapo wazungu wako 90% yawakaazi wote na wana uchumi mzuri. Kiufupi ukifanikiwa kupata PR na citizenship ya hii nchi bwana unakua umeshawin life sio mchezo.... am talking with experience.

Njia rahisi ya kuweza kupenya OZ ni kwa kupitia student visa (visa 572, 573 etc), tatizo linakuja how to rise $25,000 ili utumie kama mtaji wa kupenya. Wanachotaka wao ni rahisi tu utoe one semester ada kama $9,000 (zinachajiwa kwa module yaani kila somo lina bei yake na foreigner lazima usome module 4 kwa semester). Pia uwe na kama 18,100 kwenye A.C yako kuprove unaweza kuishi mwaka mzima bila kufanya kazi (hapa unaweza hata kuazima kwa mtu akaweka kwa ac yako alafu baada ya kupata mapepa unazirudisha) ndio hata majiran wetu huko Kenya ndio wanafanya. Cha mwisho ni bank statement ya mtu wa karibu (next of kin) ya miezi 3 ambayo inaweza kua na flow of income ya 30m-50m basi.

Kazi zinazolipa kwa sasaivi ni kazi za hospitality (nurses, carers,etc) kuna dada analipwa $56/hr na weekend kuna malipo ya penalties yaani kama unalipwa $20/hr siku za kawaida then jumamosi unalipwa (50% more) $30/hr na jumapili unalipwa (100%) $40/hr
Ukiweza tu we ingia Acacia | Immigration Australia uanze process za kujiripua,

Pia ingia hapo hapo utatakiwa kulipia $135 ili kupata consultation ya nusu saa (inalipa kwani unaambiwa option zote kwa ufasaha kabisa kabisa na unapewa na nafasi ya kuuliza maswali utakavyo) na baada ya maongezi utaprintiwa ile convo yote
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…