Ushauri, Maoni na Msaada: Kwa wanaotaka kujilipua nje ya nchi kusaka maisha, kusoma na kuwekeza

Poa mkuu karibu sana....
Kuhusu Australia aka OZ ni bonge la chimbo kwa watu ambao wameshawahi fika au wako wanafahamu nisemacho,kiukweli sio wabongo wengi wanapazungumzia hata humu kwenye jukwaa sijaona mijadala ya kuhusu kufanya plan za OZ.

Kiufupi ni kuwa OZ ni moja ya nchi za ulimwengu wa kwanza ambapo wazungu wako 90% yawakaazi wote na wana uchumi mzuri. Kiufupi ukifanikiwa kupata PR na citizenship ya hii nchi bwana unakua umeshawin life sio mchezo.... am talking with experience.

Njia rahisi ya kuweza kupenya OZ ni kwa kupitia student visa (visa 572, 573 etc), tatizo linakuja how to rise $25,000 ili utumie kama mtaji wa kupenya. Wanachotaka wao ni rahisi tu utoe one semester ada kama $9,000 (zinachajiwa kwa module yaani kila somo lina bei yake na foreigner lazima usome module 4 kwa semester). Pia uwe na kama 18,100 kwenye A.C yako kuprove unaweza kuishi mwaka mzima bila kufanya kazi (hapa unaweza hata kuazima kwa mtu akaweka kwa ac yako alafu baada ya kupata mapepa unazirudisha) ndio hata majiran wetu huko Kenya ndio wanafanya. Cha mwisho ni bank statement ya mtu wa karibu (next of kin) ya miezi 3 ambayo inaweza kua na flow of income ya 30m-50m basi.

Kazi zinazolipa kwa sasaivi ni kazi za hospitality (nurses, carers,etc) kuna dada analipwa $56/hr na weekend kuna malipo ya penalties yaani kama unalipwa $20/hr siku za kawaida then jumamosi unalipwa (50% more) $30/hr na jumapili unalipwa (100%) $40/hr
Ukiweza tu we ingia Acacia | Immigration Australia uanze process za kujiripua,

Pia ingia hapo hapo utatakiwa kulipia $135 ili kupata consultation ya nusu saa (inalipa kwani unaambiwa option zote kwa ufasaha kabisa kabisa na unapewa na nafasi ya kuuliza maswali utakavyo) na baada ya maongezi utaprintiwa ile convo yote
 
na mimi pia nilinyimwa.niliambiwa hadi huyo mchunba aje hapa Tanzania,tufunge ndoa,na tena awe ameishi zaidi ya siku 21 ndio anaruhusiwa kunioa.yani ni process ndefu sana na uwezekano wa kunyimwa visa ni 90%
 
Kwa wewe uliye na ajira na una degree moja, opportunity hii hapa ya kusoma masters organised na waswisi. Kuna module utakwenda Geneva, apply sasa maana deadline ni trh 15.03 yaani kesho kutwa. Bahati uliyo nayo ni kuwa Tanzania imewekwa kama priority country so unaweza pata scholarship. Unachotakiwa kuraise kwa upande wa huku ni 3,500 CHF tu. Hizi unaweza tafuta namna ya kupambana ukapata.

Kwa maelezo zaidi pitia hii link Executive Master in Development Policies and Practices (DPP) - The Graduate Institute, Geneva
 
Mkuu kuhusu mwitikio wa kuhost naona ni mkubwa tangu utoe utaratibu huo naona watu waliitikia vyema kila mmoja aliomba apate nafasi hiyo kwenye thread hii lakini pia kuna changamoto ambazo nafikiri watu wengi watakuwa wanazifikiria mfano kwa wale ambao wapo mikoani je watawapokea wageni wao kisha kuwatembeza mikoani au wanaotakiwa kuhost kunatakiwa mwenyeji awe yupo dsm tu?.
Mi natambua kuna watu ambao wapo serious na ninawasiliana nao wapo wanapambana mpaka sasa wafanikishe safari zao mimi binafsi najifunza kupitia kwao lakini pia ingekuwa vyema watu hawa wakawa wanatuletea mrejesho hapa kwenye uzi huu wapi wamefikia na wanakutana na changamoto zipi?.

Mkuu izzo mi navyofahamu kwa nchi yetu hii kuzungushwa kwenye vitu kama viza ni swala la kawaida ikumbukwe pia kuna watu wameamuka kupitia huu uzi hivyo walikuwa hawajajiandaa mfano kuandaa PASS,YELLOW FEVER CARD na vitu vingine vingi mtu huyu inambidi avumilie avipate ndo aanze mchakato.
Mimi binafsi nakamilisha mambo ya kiserikali safari yangu kuiva ni mpaka november pia nawasubilia hawa wageni unaotuletea.
Lakini pia mkuu tunaomba usikate tamaa kutusaidia bado tunahitaji sana msaada wako japo umetusaidia vya kutosha tunachoomba uendelee kutupa mbinu na njia tofautitofauti zitakazofanisha ndoto za wengi.
 
mkuu dr adam.faida ile option yako ya kwenda Botswana November bdo ipo, au umeamua unyoke Malta moja kwa moja?
Jiwe moja ndege wawili mkuu naona wadau wengi walinishauri ninyooke mojakwamoja ughaibuni lakini pia njia ya kufika botswana ndo ilikuwa lengo la kuweza kufika ughaibuni kiufupi nacheza kotekote ili mradi tu njia ifunguke.
 
Unatumia njia gani ndugu?? a) masomo b) ndoa c) nyingine ..........taja!! asante kwa update ol the best road to sweden....april.!!
 
Mkuu naamin wengi wangependa kuhost lakini hofu inakuja kutokana na mazingira yetu ambayo wengi wetu tunaishi uswazi au sehemu yenye watu wa kipato cha kati sasa unajiuliza mzungu na mazingira haya, mm ni mkazi wa Moro na ningependa uniweke kwenye list ya waliotsyari kuhost
 
Mkuu hii option ya pili kama nilovyochangia hapo kwanza naona ni bora zaidi kwakuanzia kupata exposure kwa watu kama sisi tunaoanza Mimi nipo tayari kuwa host mkuu naimani utaniweka kwenye list yako nipate mgen mmoja.
 
Mkuu Niko tayari kabisa hata kesho tutawasiliana vipi au hapa hapa kwenye jukwaa letu pendwa
 
Mkuu ni kweli... Uhamiaji hawatoi passport bila reason.... Nafikiri tungebadili huu utaratibu tuwe kama wenzetu ambao passport kwao ni haki ya msingi na unaweza miliki tu.
Ninachojua Tanzania kila mtu anapaswa kuwa na passport! bado haijulikani ni muongozo toka wapi walionao watumishi wa uhamiaji wanaotaka mpaka uwe na sababu ya kumiliki passport ya nchi yako. Tabia hii ndiyo inayofanya watu wengi kuhusisha idara hii na rushwa maana mambo hayawekwi wazi kila mtu akajua.
 
Mkuu naomba unisaidie kuelewa "working permit ya USA" unaichukulie huku kwetu au mpaka ufike Marekani kwanza na unaweza kuipata kwa Tzs au USA dollar ngapi
 
Nakubaliana na wewe 100% kwa upande wa afya Australia ni sehemu nzuri sana sema inahitaji uwe na mtaji kama ulivyosema kuna jamaa anaitwa Ivindo mwaka jana alianzisha uzi naamini alifanikisha safari yake kwa kupitia Acacia | Immigration Australia yeye alidai anaenda kusoma nursing then afanye mchakato apate RP mpaka sasa sina mawasiliano nae anayemfahamu huyu bwana atujuze.
Uzi wake ulikuwa
Nataka kwenda Australia kutafuta maisha pitia hapo pia utajifunza kitu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…