Ushauri, Maoni na Msaada: Kwa wanaotaka kujilipua nje ya nchi kusaka maisha, kusoma na kuwekeza

Upo sawa mkuu ila swala la makazi si la kuumiza kichwa sana kama unalengo unaweza kumtafutia hoteli nzuri ya kati au ukalipia chumba kwa muda ambachoa atakitumia mgeni wako mtakapokuwa naye.
Pia swala la chakula mgeni hachagui na hata akichagua pia nae anachangia kiasi kidogo cha pesa hivyo hilo lisikupe taabu.
 
Mkuu hapo nafikiri ni vyema sana tumsikilizie Mkuu Izzo kwanza akija hapa
 
Australia ni tofauti sana, km unasoma kwa miez18 au zaid ukimaliza unapewa 18months to find a job na visa inakua (bridging visa) so unapata muda wa kusaka job. Most paying jobs ni hospitality mpk $56/hr
Shida naona kupata scholarship za Australia ni kizigo sana. Wana complication unaweza kuugua makengeza ghafla
 
Kamanda shaka ondoa kabisa. Wengi humu hawana hata passport, si rahisi waendr ubalozi kuulizia process zikoje. Nina hakika watu wanafuatia na wameshaanza kuchukua hatua za awali kuandaa mipango.

Zoezi hili tutegemee matunda mazuri baada ya mwaka au miaka miwili kwani wengi haeakuwa wamejiandaa vizuri, walikuwa na idea ila hawajui lakufanya. Usichoke kamanda.
 
Kuhusu host mkuu tunaitaji kuwa host lakini ao wazungu watakaa uswahilini nyumba ipo je kuna vigezo nyumba iweje???
 
Mkuu izzo kweli upo serious yaan transformation ndio shidah
 
Ndio maana nasema nitakuwa sitendi haki kwa akili yangu kuweka maproject hapa ambayo hayafanyiwi kazi no siwezi hata kidogo kufanya hvyo
Mkuu vuta subra hili swala wapo wanaohangaika kulifanyia kazi. Wengine hawapo dar ningumu fastafasta kuruka dsm kufuatilia mambo haya. Ina watu wanachukua hatua na jitihada zenu hazitapotea bure
 
Sana ni mziki mnene ila ukipata nafasi hiyo uhakika wa kusonga mbele kimaisha ni mkubwa.
Wenye fedha kama US$50,000 benki na wamesoma chuo UDSM au nje, (business management, finance, MBA, chini ya miaka 40, njia ya kupata PR visa ya Australia au Kanada ipo hapo hapo Bongo.

Pia, uwe na uzoefu wa fani yako sio chini ya miaka mitano.

Hio ni fedha unayohitaji kuanza maisha na familia ya watu wanne kihalali na bila msaada wa serikali yao.

Ukiwa peke yako, ni $30,000.
 
Hapo parefuuu...
Wenye nazo njia rahisi hii hapa
 
Mkuu izzo na waasisi wa thread hii msivunjike moyo harakati zinaendelea kwa sisi potential migrants.
Binafsi mimi nilianzaga hizi harakati nyuma kidogo lakini nilikwama kwa changamoto kidogo na inaniuma mpaka leo ni hivi niliomba scholarship Belgium ya Msc, vyote nilikamilisha ilibaki kutuma hardcopy ya application yangu nikachelewa ikawa ndo imenipita.

Baada ya kuona bandiko hili ile hali kutaka ku migrate imezidi kuongezeka tunaomba ninyi wazoefu msichoke kutupa mpango mkakati lengo kuu wote tunaoamini kupitia hii ndoto ya kuondoka tutoboe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…