Ushauri, Maoni na Msaada: Kwa wanaotaka kujilipua nje ya nchi kusaka maisha, kusoma na kuwekeza

Ushauri, Maoni na Msaada: Kwa wanaotaka kujilipua nje ya nchi kusaka maisha, kusoma na kuwekeza

Kocha sizonje ndiye kasababisha yote haya Mkuu. Kuna wengine waliamua kurudi nyumbani sasa hivi wanajuta na wengine wameamua kurudi majuu kwao. Roho mbaya, vitisho, visasi, kujiona yeye ndiye yeye hataki ushauri eti anainyoosha nchi wakati ukweli anaiangamiza nchi si mambo mazuri kwa uchumi wa nchi yoyote ile duniani.

Ni ajabu na kweli!!
Leo hii kubeba boksi kunatafutwa hivi wakati muda sio mrefu wabeba maboksi walikuwa wanatukanwa na kukejeliwa?
Holy mother!!
 
Mkuu, nchi zote za ulaya, Asia na America huendi bila kuwa na English proficiency test...kwa wale wanaoenda kwa ajili ya shule lazima uambatanishe cheti hicho ili uweze ku-qualify. Kuhusu hiyo mitihani, zamani walikuwepo jamaa wa British Council na walikuwa ndo wanatoa mitihani hiyo (TOEFL)...kama uko tz/Dar..jaribu kuwacheki hawo jamaa wa British Council wanaweza saidia kidogo....
Sweden wana scholarship bila hata TOEFL wanakubali Ila uwe Umepata walau B ya kingereza O_LEVEL
 
Me ninandugu yangu, ambae kwasasa ameshakuwa raia wa UK, na anafamilia kabisa kule.
Nimeshajaribu, kumshawishi anipe mbinu za kuingia kule lakini ni muoga balaa, yaan haishi kunikatisha tamaa. Mara utasikia oooh siku hizi Hali ni mbaya Sana.

Halafu inaonekana si mtu wakujichanganya kabisa yan hujui aanzie wapi ili kunirahisishia njia.

Wadau Hebu nipenni mbinu ili nimfundishe Huyu anko wangu maana amelala Sana.
 
Mkuu acha tu mi siku system ikichange naweza Rudi uzuri huku kuna wabongo wengi mpaka wana timu ya mpira wa miguu akina Athuman Machupa na Shekhan Rashid na wenzao nadhani Kama Wangekuwa members humu wangeleta mautundu walivyofanya mpaka kufikia pale walipo . Sweden is the best place.

Machupa na shekhan wote wako hapa,walikuja kucheza mpira shekhan akazamia na kuendelea na maisha baadae kapata mke kaoa na sasa ana watoto 2 na tiyari ni raia wa hapa.lkn walipigana saana kupata karatasi si rais inabidi kukaza buti saana,na maisha ya hapa ni akili saana na kujipanga unaweza kuwa na karatasi lkn ukawa choka mbaya tu kama Joseph kaniki gorota sasa yuko jela
 
Ni kweli mkuu wakati naingia Sweden niliingia kwa lengo la kusoma via scholarship ya shirika fulani lengo lilikuwa Ni after three years nitarudi Bongo kuendelea na mambo mengine according to their principles kumbuka by then nilikuwa nimefukuzwa Chuo na sikuwa na hili wala lile but uncle wangu alinichomeka katika hiyo chance wakati naendelea na masomo nilimpata rafiki wa kike Swedish ambaye tulijaliwa kupata mtoto then ikawa nimepewa uraia wa Sweden ila uraia wa Bongo sijaukana bado but nilichofurahi Ni kwamba Sweden Kuna watanzania wengi Sana I'm feeling like I am in Tabata.
Mkuu Stockholm vipi maisha kwa mtu anayepata 9000 SEK kwa Mwezi? Naweza kusave hata kidogo?
 
Zipo nchi zaidi ya 50 ambazo mtihani wa kingereza si inshu lakini swala la mitihani ya kingereza si swala la nchi kwani nchi ambazo kingereza si Lugha yao kingereza hakitokusaidia chochote swala la kiingereza ni swala la Chuo chenyewe kuamua vyuo vingi vya Ulaya na sehemu nying ambao wanachukua wanafunzi wa kimataifa wanachukulia kiingereza kama lugha muhimu ya kufundishia kwa wanafunzi wa kimataifa
Ungetutajia baadhi ya hizo nchi mkuu ingependeza sana.
 
Mimi nipo Stockholm kwa zaidi ya half decade ntaeleza badae Ni kwa njia gani waweza tumia but briefly Kuna timu ya mpira huku inaitwa Kilimanjaro ipo under Athuman Machupa Na Shekhan Rashid and co wanaweza kusaidia pia kuwaleta wabongo huku. lusungo
Mkuu, kama naweza kupiga danadana mbili tatu au kukimbia na mpora si wanawaweza waka ni recommend na kunichukua hao watindiga wenzetu??
 
Binafsi uzi huu nauunga mkono 100% Lakin pamoja na hayo bado kuna changamoto nyingi kufikia hatua ya kuondoka nchini, kuna mambo mengi ambayo niya msingi hasa upande wa Serikali yetu tukufu hasa upande wa Idara ya uhamiaji. Tz yetu mtu kupata the tu cheti cha kuzaliwa ambacho ni haki ya Mzawa mpaka jasho likutoke, na ikiwezekana na rushwa juu utoe. Ukienda Migiration ili kuanza mchakato wa passport utahenya vibaya,

Kupata card ya chanjo ya homa ya manjano mpaka utahenya.

Lakini pia changamoto nyingine ni mtu kupata Nauli kamili ya kukufikisha mahari unako taka kwenda.
Binafsi ninacho elewa wakirahisisha hayo mambo ya juu, naona Tanzania inaweza kubaki na wazee tu,
Sasa nchi gani hii isiyo toa ajira, Mali asili ni nyingi lakini hatujui wala hatuoni uthamani wake, Vyeo vya juu wanapeana wao kwa wao

HAKI YA MUNGU MIMI SIKU NIKIONDOKA NDO BASI TENA. BORA NIKAFIE KWA FARAO KULIKO KANANI AMBAKO SIJAWAHI FIKA.

Kadi ya manjano sio kazi nikulipa tu na upata chanjo tena wanakuuliza unataka chanjo kabisa au cheti tu?cheti cha kuzaliwa RITA ni wiki moja tu unapata.Pasport ndio tatizo may be,kadi ya manjono europe hawaitaji uwe nayo wala hawakuulizi kabisa
 
Uzi mzuri sana,

kuna njia ya kuvolunteer kufanya kazi katika sehemu mbali mbali duniani hii ni njia nyepesi ila inahitaji pesa kidogo.

kuna web ya workaway.info inaungaisha katika ya worakway na host,unatakiwa kujisajili inacost 29 usd unalipia bank au kwa paylal.

Uzuri wake hii ni njia ya uhakika na mara nyingi host inakua juu yake malazi na makazi juu yako wengine wanakupa access ya kufanya kazi manake kujitolea inakua mara nyingi katika ya masaa 3-6 per day mda mwingine unakua free kufanya mambo yako.
pia unaweza kuongeza muda huku ukisoma ramani ufanye vipi utoke.

vitu unavyohitaji kujilipia ni ticket yako ya ndege go and return,visa fees ambayo inategemea na nchi ila sio ghali.

nauli ya ndege ni ghali kama umechagua nchi za mbali kwenda kama Canada,Australia,Japan and Nordic countries.

Nakutakieni mafanikio mema katika kutafuta maisha nje kila kitu kinawezekana.
 
Mambo ya scholarship jamani mtuwekee, mm hadi naona kero, ukijipanga kuomba vyuo kama 10 duuu utazuguka kwenda kuchukua barua za reference kwa malecturer hadi ukome. Mm nilitaabika sana, kila siku nipo chuo kuomba reference letter, jamaa hawapatikani, email zao kama za maroboti hazijibiwe.

Nikaamua kujilipua kwa kuchonga muhuri wa department, logo yao ipo kwanet, recommendation najifanyia mwenyewe sitaki ujinga kabisa.

Mwaka juzi nikapata admission Coventry University - MSc Oil and Gas Management, scholarship zinapitia wizara ya elimu, natimba mjengoni wananiuliza wewe umejuaje kama kuna scholarahip, nikawafungulia pc nikawaonyesha tangazo kwenye website yao. Daaaa nilijua tu hapa sina changu. Nilikosa scholarship ile.

Bongo nihatari sana, inawezekana leo hio tungekuwa mbali sana na kuwa na wataalamu wa kila aina, lakini wapiiii.
Aisee hakuna kitu kinasumbua Kama reference letter hapa kwetu. Yaani lecturers hawana muda kabisa wa kukuandikia barua. Akikuonea huruma sana anakwambia umpelekee draft then yeye arekebishe na kusaini
 
Machupa na shekhan wote wako hapa,walikuja kucheza mpira shekhan akazamia na kuendelea na maisha baadae kapata mke kaoa na sasa ana watoto 2 na tiyari ni raia wa hapa.lkn walipigana saana kupata karatasi si rais inabidi kukaza buti saana,na maisha ya hapa ni akili saana na kujipanga unaweza kuwa na karatasi lkn ukawa choka mbaya tu kama Joseph kaniki gorota sasa yuko jela
Du KANIKI kawekwa ndani tangu lini mkuu kosa lilikuwa nini?
 
Back
Top Bottom