Mkuu naandaa mfumo mzuri wa kufanya swala hili kwani project ni mwezi wa 6 namba nilisema nianze kutumiwa mwezi wa 4 bt mpaka sasa nimepata namba kama saba tu bt ktk watu 7 niliopata namba zao watu watatu hawafai kutokana na sababu za usalama wa wageni bt kwenye project ya mwezi wa 6 tutaitaji host kama 20 hv
kavel kavel vp mbona kimya toka juzi maneno 400 bado????? duh
Kuna misemo 2 ambayo huwa inanifanya kujihisi niko hai
1."To be a leader is to suffer for the other's "
2. As you're trying to light a candle for others to see the bright future ahead, your also brighten your own future.
Huu Uzi umenikumbusha mbali sana mwaka 2007 nakumbuka nilienda ubalozi wa marekani mara 2 bila mafanikio, kipindi hicho kuomba visa nilikua ni dola 100 so nilipoteza dola 200 ziliniuma sana japo sikua nimezitoa mimi.
Kipindi icho nilikua najiandaa kufanya mtihani duuu nilijihisi kukosa amani kwani sikuamini kabisa kilichonitokea mara 2 kunyimwa visa, ikumbukwe nilikua under 18 na nina mashetani ya kwenda mbele kwa George W.Bush.
Mpaka naenda chuo akili yangu ilikua haikubaliani na kitendo cha kukosa visa lakini nitafanyaje na ndio ishatokea, niliumia zaidi baada ya mfadhili wangu tokea primary nae alipopata mtoto akiwa na miaka 58 mke na mume 60 huo ni mwaka 2010.
Kwao ilikua furaha nami nilifurah mwanzoni lakini furaha ikatoweka baada ya kunijulisha kuwa hawataweza kuendelea kunizamini masomo ya udaktari katika chuo cha IMTU.
Ndoto zangu za kuwa njia katika kitongoji changu zikazidi kufifia ilinilazimu lubadili course na kuhama chuo ikumbukwe TCU imeanza kutumika mwaka 2010.
Huwezi amini nilibidi kwenda ofisini kwao na kujifanya chizi ili nihamishwe chuo. Vingine ni kama masihara nakumbuka ilikua majira ya sa 8 mchana ndio niliruhusiwa kuingia ndani kumwona anaehusika na data base, kabla ya kumwona nikakutana na mama 1 akanihoji sana, ikabidi nijitoe ufahamu, niigize wa vijijini chuo nilisaidiwa kuapply na shangazi na hakujua kama zile 4500$ ni dola..Asee usiombee, ila akili ni Mali. Basi ofisi nzima wakaanza kunicheka na kushangaa, mimi wala siogopi KAMA ZOMBIE tu nilikua. Basi mama akanichukua mpaka kwa jamaa wa database then wakanibadilisha kwenda vyuo vya watoto wa wakulima aka vya TSH.
Ikumbukwe waliokua wananidhamini na kunifadhili naenda USA ni professors mke na Mme wrote ni profs mwenye sekta ya Afya, hivyo nilikua nina imani kwamba pesa ya kuendelea kunifadhili ilikuepo lakini wamegoma baada ya kupata mtoto tena wa uzeeni hata ivyo bahati haikua upande wangu mwaka 2007.
Baada ya mambo mengi nimekua nikipambana kuhama hii nchi kwa kutumia mipango hafifu lakini kupitia huu uzi nimejikuta najihisi bado niko hai tena. BIGUP wrote mnaozidi kutoa mlicho nacho. THROUGH SHARING KNOWLEDGE & SKILLS WE ARE SHARING LIFE.
Kupoteza na kupata ni kama 1_2, ukweli kufatilia kila comments mwenye huu Uzi kisha unakaa kimya bila kuchukua hatua yeyote sio jambo LA kiungwana kabisa, natamani kila atakaesoma huu Uzi abadilike ama abadilishe wengine kwa namna ingine.
MREJESHO.
NIlifungia accounts couch surfing na air bnb pia kujiunga home stays, hivi vitu ni kweli vinaganya kazi yaani ukiwa na nauli ya tickets go & return kuna host wana kupata offer ya kukupokea airport na free meals & accommodation in exchange of 0.00 coins kwa miezi 1-12 hapa ni wewe tu. Huwafanyii kazi yeyote.
Nimejaribu Leo kutumia host stays nchi za China 3, Japan 3, korea, Finland, Malta.
Pia kuna host unachangia dola MF. 500$ kwa mwez wanakupa chakula na malazi kwa mwezi, kwa walioko serious na nauli mkononi jipange then jua kwanini unaenda uko, utapataje RP, kisha jisogeze mbele. Muhimu ni kujipanga tusiende tu kisa umesikia kuna green pasture, lazima uwe na ramani na Dira ya unakotegemea pia PLAN B
MWISHO.
Naomba kuwa coordinator wa host kwa Tz, sio kazi nyepesi lakini naimani, nina uwezo wa kufanya kwa kiwango kinachotakikana#izzo
Ila kama unaenda south njia salama ni ya ndege tu... Kata return ticket... Ingia booking.com book room then print booking conformation ibebe ukifika huko unawaonesha tuuu unapita!!
Njia ya boda si nzuri sana
Isanga family