Ushauri, Maoni na Msaada: Kwa wanaotaka kujilipua nje ya nchi kusaka maisha, kusoma na kuwekeza

Ushauri, Maoni na Msaada: Kwa wanaotaka kujilipua nje ya nchi kusaka maisha, kusoma na kuwekeza

Wakuu, mie nashukuru nimepata Scholarship Sweden. Nitakuwa Umea University kuanzia sept mwaka huu, naomba mwenye connections na kazi za vibarua ( Non Skilled jobs) ili nikiwa free haswa masomo yanapokuwa hayajachanganya niwe na-make at least SEK 5,000-10,000 kwa mwezi.

Nipo tayari kufanya kazi yoyote halali ikiwamo kulimia bustani, kuvuna mazao, kuosha magari, kufanya usafi, kubeba box n. k. Kiufupi wakuu sitochagua kazi. Elimu yangu nitaweka pembeni na kupambana kusaka krones tu. Umaskini si kitu kizuri wakuu. Nitapambana kwa kila njia halali kuutokomeza umaskini maishani mwangu. Ee Mungu nisaidie.!!

Nimedharirika sana hapa bongo kutokana na ufukara, sasa kwa hii fursa ninaamini japo ni kwa ajili ya kimasomo ila nitapambana hadi tone la mwisho kuhakikisha natusua. Mie naamini majuu ni majuu tu. Hata kama ni kwenda kimasomo, hata kama kamji nakoenda nikadogo ukilinganisha na Stockholm ila nitapambana tu.
Hongera sana man.
Bongo Nyoso sana
Keep your head up Keep pushing
 
Mbinu nyepesi sana ya kufanikisha ndoto zenu coz naona wengi mnatamani kuja au kwenda Ulaya na US lakini njia mnayotumia ni ndefu ikiwamo ya ndoa za usanii siku hz wanafatilia sana na njia hii siku hz ni ngumu kwa sasa hv kwani siasa za sasa ni siasa za utengano na kufunga mipaka dhidi ya wageni
Ok njia ya kwanza ni kuingia nchi ya Malta ,Malta ndio nchi inayomkaribisha mgeni yeyote na yenye sheria nyepesi sana za uhamiaji kwa wananchi wanaotoka nchi za Commonwealth ( British colonisation)
So ukishafika Malta ukiweza kukaa ndani ya Malta ndani ya mwaka mmoja bila ya kufanya jinai huna haki ya kuomba uraia so kama utakuwa umekwenda kusoma , kufanya kazi, kutembea au kwenda kufanya kazi ya kujitolea (kazi za bila ya malipo)
Ukishapata uraia wa Malta unakuwa na uwezo wa kwenda kufanya kazi nchi yeyote ya Ulaya kwani Malta ni nchi iliyo kwenye jumuhiya ya Ulaya
So kama unabahati unaweza kupata lakini nchi nying za ulaya au nchi za dunia ya kwanza kupata kazi kwa elimu uliyosomea Africa ni ngumu sana mpaka usome kwao ndio wanakuamini
Owk kama utakuwa uko vizuri kiafya unaweza kwenda Jeshini ,nchi nyingi za ulaya zinachukua raia wa nchi za ulaya kama wanajeshi au kama umetoka nje ya jumuhiya ya ulaya ni lazima upate parmanent resident kitu ambacho ni kigumu sana kukipata kwa nyinyi mnaokuja huku kiujanja janja
Nchi zinazochukua raia wa nchi nyingine kwenye majeshi yao nitakuja na list yao muda si mrefu
lakini ni nchi ambazo zipo kwenye kundi la A list duniani zikiwamo nchi zote za Scandinavian
Ushaingia jeshini ,majeshi mengi ya Ulaya wanapaga watu ambao si raia wa nchi hyo mkataba miaka mitano mitano ndani ya hyo miaka mitano unaruhusiwa kusoma chochote utakachopenda gharama ni za jeshi so utachagua cha kusoma kama umetoka bongo na ka degree chako utasoma masters kama umetoka manyoya utatafuta cha kusoma ndani ya miaka mitano ni mingi sana na unapata faida mbili moja kulipwa mshahara ,huduma za Afya na uhakika wa kupata uraia kama utaitaji
So ukimaliza miaka mitano tu usiongeze tena mkataba ongeza tena kama umeipenda kazi ya jeshi so kama umeona ni manyoya unaiacha so unalipwa mafao yako na unakwenda kuomba uraia na unapata hata bila ya kufanya mtihani wa kuomba uraia na hii kuna nchi hawataki uraia pacha kama Germany au Norway so kama nchi hawataki uraia pacha basi unachagua mmoja ukishamaliza kupata uraia wa nchi hyo uliyoichagua ww from there unatafuta kazi kwa vyeti ulivyosomea jeshini na tena wakijua ulikuwa mwanajeshi wanakuheshimu sana kwani unaonekana umejitoa kwa nchi so unapata kazi na maisha yanaendelea ndani ya miaka 6 tu mission inakuwa imekwisha ukipita Airport ukionyesha gamba la mzungu unapita tu hupekuliwi pekuliwi kama mwenye passport ya Bongo
Kuna website ambazo watu kutoka sehemu zote za dunia wanatafuta watu wa kuja kumfanyia kazi ya kujitolea ambapo yeye atakupa chakula na sehemu ya kukaa bure kipindi chote utakachokuwa pale kwake mwaka mmoja tu ndani ya Malta bhasi
Lakini leo kunambia sijui mnapanga kuondoka kwenda nchi ambayo huna mwenyeji naona mnacheza nyinyi na mnadanganyana Ulaya na US ya sasa si kama ya zamani utaishia jela au kufa tena na balozi zenu zilivyo ngumu kwa raia wake utakoma na kujuta kuja tena mkuu wenu amesema muachwe njia nyepesi kabsa ndani ya miaka 6 tu umefanikisha mwaka mmoja Malta miaka 5 jeshini mwaka wa sita unapassport ya mzungu
Na hii ni kwa wanawake na wanaume sehemu pekee ni kufika Malta tu mwaka mmoja tatizo nililogundua Waafrica wengi akili yetu tunawaza ulaya tena zile nchi tajiri tu lakini mmeshindwa kujua dunia nzima wanawaza hvyo hvyo njia hii ya malta bado wengi awajaijua then tafuta mtu wa malta kafanye kazi ya kujitolea kwa mwaka mmoja kwanza unapata pa kukaa kula na mwenyeji lakini kwenda sehemu kwa mipango mipango mtakuwa mnadanganyana tu wanawake hasa wa Tanganyika wamekuwa wanaogapa sana kuchukua maamuzi ya kuondoka lakini nataka kuwambia tena wanawake ndio njia nyepesi sana kwani wazungu wanawaheshimu sana wanawake cha kwanza kwa heshima kwa wazungu
1 Wanawake
2 Mbwa au wanyama
3 Mwanaume
So kwa dada zangu kwa njia hii ya Jeshi ni bora sana kwao tena sana naongea hv kwa kujua ninachosem

Ningependa kuwambia ndugu zangu Watanganyika kwamba dunia ya sasa maendeleo yamehama kutoka kwenye nchi zinazoongea kingereza na kuhamia kwenye nchi ambazo haziongei kingereza kwani dunia nzima robo tatu wanajifunza au wanajua kingereza na target yao ni kwenda kukaa nchi zinazoogea kingereza sasa utakuta nchi zinazoongea kingereza zimeshajaa wahamiaji kibao lakini niwape siri kubwa kuwa nchi zisizo ongea kingereza zinaitaji sana watu kwani watu wamekuwa wakienda kwenye nchi zinazoongea kingereza

MALCOM LUMUMBA

Hili bandiko lako linafurahisha na kutia moyo mno chief,hasa kwa wale kwenye mpango wa kwenda kusaka tonge abroad..!
Lakini bahati mbaya mengi uliyoandika katika bandiko hili hayana ukweli,hivyo kama msaka tonge atafuata haya uliyoyaandika bila kufanya research basi atakuwa ameumia vibaya sana..!
Ila bandiko lako linatia moyo sana,shukrani kwa hilo..!
 
Nimeona wale wanaokwenda ulaya kupitia pwani ya Libya hadi Italy jamaa ni wababe watu wenye roho ngumu sana,(wasudan,Ethiopia,Eritrea)jamaa wakifika Italy wanaunga kwa mguu mpaka ufaransa.
Ufaransa wanaishi barabarani,chini ya madaraja,wanazagaa ovyo mitaani wengine wanaishi kwenye vichaka halafu wanatoroka makambini kwa kuruka fensi baadhi yao wanakufa wamejazana kwenye mpaka wa France na UK eneo LA Calais sasa hapa wanatega kudandia malori kuingia UK ni shida sana kila wakati wanakimabizana na polisi,wakiulizwa na wafaransa shida yenu nini? Wanasema sisi tunaka kwenda UK kwa sababu UK ndio ulaya kuna job nyingi na ni pazuri kuliko hapa France na Italy, halafu ni madogo wa miaka 16-19. Da ni hatari sana inahitaji roho ngumu sana nahisi kama wanawaharibia watu wanaotaka kwenda kihali wanafanya vurugu kila wakati.
 
Passport nime pata mwez wa kumi na mbili mwaka jana kuhus barua ya mwaliko tafua ndug au rafiki anae ishi hata kenya aku email barua ya mwaliko na akutumie photocopy ya ID yke. Ila pale nje migration kuna stationary wanawez kukusaidia ukiwapoza kidogo. Kama una ndoto zaku safiri fight upate passport ukiwa na full documents huongi hata mia

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu hebu nisaidie hiyo sample ya barua ninae mtu yupo nje nataka anisaidie hiyo barua
Please
 
Mkuu hii ni thread maalumu kwa kupeana uzoefu wa majuu na namna ya kwenda.... Ni maalumu kwa wenzetu wanaohitaji kwenda huko... Sio mimi ninayehitaji nimeweka kwa niaba ya wengine. Nimeshaishi USA for 8 years na Denmark.
So ili kupunguza wimbi la thread za ushauri ni vizuri tutiririke hapa ili wengine wajifunze.
[/QUOTE]
 
Mkuu hii ni thread maalumu kwa kupeana uzoefu wa majuu na namna ya kwenda.... Ni maalumu kwa wenzetu wanaohitaji kwenda huko... Sio mimi ninayehitaji nimeweka kwa niaba ya wengine. Nimeshaishi USA for 8 years na Denmark.
So ili kupunguza wimbi la thread za ushauri ni vizuri tutiririke hapa ili wengine wajifunze.
[/QUOTE]Mkuu nipe kwanza japo intro ya hizo nchii au fungua thread kidogo uelezee jinsi ya hizo nchini na uzoefu wako ulio kaa huko.

Usisahau kuni tag
 
Wanajf naombeni namna na jinsi ya kutoka TZ kwenda nchini kuwait kwani ni nchi ambayo naipenda sana naitaji sana kufika uko.

Ni nchi nzuri sana ila ina masharti sana kama ukienda kwenye website yao ya visa ni baadhi ya nchi wanapewa E visa online lakini kwa pass ya Tz naona ukaombe ubalozini kama wapo DAR
 
Wakuu, mie nashukuru nimepata Scholarship Sweden. Nitakuwa Umea University kuanzia sept mwaka huu, naomba mwenye connections na kazi za vibarua ( Non Skilled jobs) ili nikiwa free haswa masomo yanapokuwa hayajachanganya niwe na-make at least SEK 5,000-10,000 kwa mwezi.

Nipo tayari kufanya kazi yoyote halali ikiwamo kulimia bustani, kuvuna mazao, kuosha magari, kufanya usafi, kubeba box n. k. Kiufupi wakuu sitochagua kazi. Elimu yangu nitaweka pembeni na kupambana kusaka krones tu. Umaskini si kitu kizuri wakuu. Nitapambana kwa kila njia halali kuutokomeza umaskini maishani mwangu. Ee Mungu nisaidie.!!

Nimedharirika sana hapa bongo kutokana na ufukara, sasa kwa hii fursa ninaamini japo ni kwa ajili ya kimasomo ila nitapambana hadi tone la mwisho kuhakikisha natusua. Mie naamini majuu ni majuu tu. Hata kama ni kwenda kimasomo, hata kama kamji nakoenda nikadogo ukilinganisha na Stockholm ila nitapambana tu.
Mkuu tusaidie ulipataje scholarship na sisi wa mavumbini uku tupambane?
 
Back
Top Bottom