Ushauri, Maoni na Msaada: Kwa wanaotaka kujilipua nje ya nchi kusaka maisha, kusoma na kuwekeza

Ushauri, Maoni na Msaada: Kwa wanaotaka kujilipua nje ya nchi kusaka maisha, kusoma na kuwekeza

Mkuu usiwaze Sana hayo Mambo yapogo Sana ..Kama wewe unataka kuja nnje basi pambana tu kwa namna yako unavyojua wewe ..sisi wengine tulitapeliwa lakini hatukukata tamaa tulipambana Hadi Sasa tupo hapa tulipo, ivyo wewe pigania maisha yako ..huku arabuni pesa ipo Tena Kama siyo mvivu na mtu wa Bata basi utajenga nyumba hapo bongo hata tatu kwa mwaka.
naomba unipe A,B,C za Uarabuni kaka
 
Scandinavia ni pazuri lakin kuna changamoto zake lazima ujifunze lugha yao,mie niko sweden hapa,lugha na kupata permanent residence ni mziki,kabla ya kuja unatakiwa kujipanga sana,ujue wapi unafikia ukiwa na mwenyejj mzuri unatoboa maisha kilaini saana,lkn wabongo ulaya ni shidaa sio wote lkn tuna mambo ya ajabu saana kusaindiana,lkn sometime naelewa unaweza kumsaidia mtu kumbe akili yake ni kuuza drugs end of the day anakuweka matatani ,wabongo wengj wako jela kwa hiyo kitu hapa Europe.
Huko Scandinavian naona kila mtu anapataja tunapataje mchongo huko
 
Chotera upo sahihi unachoongea mimi nishaenda ila nilibeba nywere na viatu tripu moja vipo bei chini kweli ila nilishuka navyo SA maana pale soko la vitu brand hizi Nike,Adidas, puma hapo SA unauza sana na kodi haumizi ili mradi visiwe copy tuu hata kuingia haviingii SA...Waganda na Wakenya wanatumia hiyo fursa ndio maana huko kwao vipo vitu vingi na vizuri..
Ndio maana viatu vya mtumba Kenya ni grade nzur kumbe
 
Mkuu hiyo usiwaze si binadamu wote wako fair kumpa njia mwenzake afanikiwe ni wachache sana wenye hiyo sacrifice.
Lakini kingine pia inategemea huyo classmate wako mliishi naye vipi na mnaaminiana vipi.
Wako baadhi ya watu pia wakisaidiwa baadae hugeuka na kuwa masnitch.
Kwa mfano unakuta kuna mtu mwingine yuko nje ya nchi lakini kuna dili za ujanja ujanja anazipiga ili kutoboa sasa anaogopa akiziweka wazi unaweza baadae ukawasanua watu dili zake zikabuma.
Kwa hiyo unapokuwa unasaka details kwa mtu fulani ukazikosa usimaind tafuta alternative way ya kupata hizo information.
Penye nia pana njia.

Sent from my SM-C7000 using JamiiForums mobile app
Ni kweli mimi napambana ila mshkaji ali nirusha tu ila madhari bado nipo hai na afya njema nta pambana
 
Canada
Application fee $75
Tuition fee $12,000 per year
Visa Application fee $150
Biometric fee $85
Medical check up Tshs 400,000
Tuition deposit $1,000 Non Refundable
Ticket cost $1,800
Insuarance $1,000

Msc or Diploma
Boss hio tuition fee unatakiwa kuonekana bank kwenye visa interview???
 
Kuna tetesi kwamba baada ya Uingereza kuondoka rasmi kwenye umoja wa Ulaya wataigeukia Jumuiya ya Madola na kuanza kushirikiana na nchi za Jumuiya hiyo ikiwemo Tanzania.

Ni hapo utakapofika huo muda tutafahamu zaidi.
Dah lini sijui ndg zangu
 
Back
Top Bottom