Pre GE2025 Ushauri: Mbowe ajiuzulu mara moja kama Mwenyekiti wa CHADEMA

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Hakuna mkuu, kuna mambo ayahitaji mihemuko, safari ni mwendo au atua moja kwenda nyingine , Maridhiano ilikua sehem ya mwendo , so iyo phase imeisha twende na phase mpya sasa , Uongonzi wa Chadema mpaka sasa wapo sawa kabisa
Ni kweli, ila sio chini ya uenyikiti wa Mbowe.
 
Mimi naongelea CHADEMA mkuu. Sio watu wa serikalini. Mbowe hawezi kuaminika Tena. Katuingiza chaka halafu anadai anajutia kumuamini Samiah.
Yale Yale mbowe au Chadema hawajawahi kukusanya Kodi katika inchi hii tuwalaumu Kwa lipi maliziano ilikua ni jambo jema Kwa pale tulipokua tumefikia hata MH RAIS hayakua madhumni yake kuvuruga maliziano isipokua Kuna wenye vimelea vya mwenda zake ndio wanaompelekesha mpaka hapo ushapata mwanga walaumu kina makonda na kina mwigulu na co yote ya sukuma Gang
 
Mwenyeki wa chama hajiteuwi mwenyewe, anachaguliwa pitia vikao halali vya chama, kwa kujinadi na kuomba kura ,siku ambapo hatapigiwa kura za kutosha basi atakoma kuwa mwenyekiti , mbona kitu simple tu
Alisema ataachia uenyekiti mwaka ulioisha, je ameachia Hadi sasa? Jana aligusia hilo zaidi ya kukiri kuingizwa mjini na bibi mkojani? Ni hatari kuwa na mwenyekiti aisyesimamia anachoongea hadharani.
 
Hata yeye mwenyewe Mbowe analijua Hilo ndio maana aliahidi kustaafu mwaka Jana.
Mbowe hana nguvu tena za kisiasa kuiongoza chadema, anayumbisha watu hana msimamo thabiti.... Chadema inahitaji kiongozi aliye na msimamo na anayesimamia ajenda za chama sio za kwake binafsi!. Chadema ikiwa na kiongozi Kama Lissu au Heche Mimi nakwambia hata isipochukua dola but 70-80 ya wabunge watatoka chadema... Raia wanahitaji kiongozi asiyewayumbisha.
 
Nimesoma hii nikataka nipite tu ila nikaona niandike kitu; naona wengi mnataka Mbowe ajiuzulu na kuomba radhi, tena wengine mnakuja na sababu zilizotoka nje ya mada zisizo na msingi wowote.

- Kumpokea Lowassa, hili hakulifanya mwenyewe, yale yalikuwa ni maamuzi ya KK ya chama chao kumpokea Lowassa, ndio maana siku ilipofika, karibia nusu ya wajumbe wa KK walikuwepo pale kumpokea, sijui kama mnajua maana ya collective responsibility au ni mihemko tu.

- Maridhiano; hivi mmewahi kujiuliza kwanini alitaka maridhiano wakati ule, au mnapiga kelele tu?

Wakati ule wa Magufuli kwa mfano, na aina ya siasa alizokuwa akizifanya Magufuli, mlitegemea Mbowe aende sawa na Magufuli kwa namna ipi? ni ipi kwenu ilikuwa njia sahihi kwa Mbowe kufanya siasa wakati ule badala ya maridhiano? Itajeni hapa, au mlitaka ashindane nguvu na Magufuli ambaye kila mmoja alimjua kwa ukatili wake?

Mbowe kuja na wazo mbadala leo mnamuona mkosefu, mlitaka akachukue wapi jeshi la kumuwezesha kuandamana? mfano yale maandamano yao kule Kinondoni alipokoswa na risasi pamoja na wenzie, mlitaka ile ndio iwe njia yao ya kufanya siasa, wakati wewe una mdomo unashindana na mwenzio anayetumia risasi kuyazuia?

Ajabu Mbowe "kukosea" kama mnavyoona nyie kwa thinking yenu, not me; anatakiwa kujiuzulu, hivi ni malaika yupi atakayekuja kuiongoza Chadema ambaye hatakosea [kama kweli kosa litakuwepo sio haya makosa yenu ya mihemko]?

Nawashauri tu, kama Mbowe hamumtaki kuweni straight kusema hivyo, mtoe na sababu zenu zitakazomuhusu personally, kama mwingine alivyozoea kuimba kiongozi akikaa miaka kumi akili yake inachoka!, hata kama ni sababu ya kuchekesha lakini atleast ametoa sababu.

Lakini sio kuja na sababu za jumla kama kumpokea Lowassa, mnazidi kujipoteza, au kumtaka ajiuzulu kisa "amekosea", huyo malaika wenu yuko wapi aje apewe Chadema leo?! mna tatizo la kukariri siasa za aina moja pekee, akitokea mwingine mwenye plan B kwenu anaonekana hafai! kwani hiyo plan A yenu lini iliwahi kufaulu?!

Mna wenge sana.

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
 
Alisema ataachia uenyekiti mwaka ulioisha, je ameachia Hadi sasa? Jana aligusia hilo zaidi ya kukiri kuingizwa mjini na bibi mkojani? Ni hatari kuwa na mwenyekiti aisyesimamia anachoongea hadharani.
Mwenyekiti akisema ndio tatizo, wakisema wengine wa chini yake sio tatizo...

Lissu aliwahi kutoa kauli kumhusu Lowassa akadai asiaminiwe popote, umewahi kumtaka Lissu nae ajiuzulu u makamu mwenyekiti?!

Politics haitaki mihemko kama hii mliyonayo, kuwa mwanasiasa hasa kiongozi wa chama lazima uendane na mazingira yaliyopo kwa wakati husika, ujue njia ya kukabiliana na mpinzani wako, sio kukariri njia moja uitumie miaka yote, mtafeli.

Lissu aliwahi kusema akiibiwa kura 2020 hapatakalika, ikawaje baada ya pale hapakukalika? au alizuiwa na Mbowe kuitisha maandamano?! maana kwenu Mbowe hana jema!.

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
 

Ile blunder ya Lowassa ilitakiwa iwe fundisho kwake. Na baada ya ule uchaguzi ilitakiwa ajiuzulu ila ndio hivyo, bado anaona CHADEMA haiwezi bila yeye.
 

Kitendo Cha Mbowe kuamua kufanya maridhiano na Samiah lilipunguza harakati za kisiasa na kuonekana CHADEMA imecompromise na CCM. Na hata watu kupelekea utani wa kuilamba asali. Hata Mbowe mwenyewe anakiri kwenye chama alipata upinzani mkali Sana.

Hoja yangu sio kumkataza Mbowe, hoja yangu ipo kwenye position aliyonayo Mbowe.

1. Kwanza, Kama mwenyekiti alikiri hadharani kwamba hatamsema vibaya Samiah.

2. Pili, hayo maridhiano alivyokuwa anayapigania Mbowe hayajazaa matunda zaidi ya kulipa CCM nafasi ya kuretreat na Kuja na scheme nyingine.

3. Tatu, Mh Mbowe kakiri hadharani kwamba anajuta kumwamini Samiah. Hilo ni tusi kubwa Sana, Yani unakubali kurubuniwa kijinga halafu unakuja kulalamika mwishoni, when the damage has already been done, itasaidia Nini?.

Niseme tu kwa kauli ya Mbowe kuwa anaajuta kumwamini Samiah, ilitosha kuwajibika mara moja.
 

Kuhusu uchaguzi wa 2020, ule haukuwa uchaguzi. Ulikuwa uwanja wa vita. Ndio maana nature took its cause 5 months later.
 

Sawa mkuu
 

Kweli mkuu, mwenyekiti Hana msimamo.
 
Reactions: Exy
Usiniwekee maneno, Mbowe ana mazuri yake, Sina popota ninaposema Hana jema, lakini wakati ukuta. Team ikikosa mafanikio kocha huondoka, na hata wakati mwingine kocha msaidizi hubaki.

Kama Mbowe anajua Lisu aliitisha maandamano na hayakupata watu, haya anayoitisha Sasa ni ya Nini wakati inafahamika watu hawana udhubutu wa kuandamana kudai matakwa yao yatimizwe?
 
- Kwanini Mbowe amseme vibaya Samia wakati walikuwa wote kwenye meza ya maridhiano? unataka wakati anajenga, awe tena anabomoa hapo hapo?! haiingii akilini.

- Ukisema maridhiano hayajazaa matunda, utakuwa na tatizo la kupoteza kumbukumbu, hukumbuki hata hii mikutano ya siasa inayofanywa na Heche maeneo tofauti kwa sasa nchini ni matunda ya maridhiano.

• Labda wewe usiyetaka maridhiano utuambie, njia ipi unayoipenda iliyowahi kufanikisha jambo lolote kisiasa ambayo ulitaka Mbowe aifuate? sio kelele tu.

- Mbowe kujuta kumuamini Samia hilo sio kosa kwake, ni ubinadamu; yule sio jini aijue dhamira ya Samia kuanzia mwanzo, hoja zako nyingi hazina mantiki.

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
 
Kuhusu uchaguzi wa 2020, ule haukuwa uchaguzi. Ulikuwa uwanja wa vita. Ndio maana nature took its cause 5 months later.
Kumbe unakiri ule ulikuwa uwanja wa vita, ajabu unataka Mbowe aende kwenye uwanja wa vita bila silaha, wake up dude!.

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
 
Leo machawa wa mbowe wanamnanga mwenyekiti wao? ni jambo la kushangaza Mimi naendelea kuwaambia msipende kuamini hivi vyama mnapoteza muda wenu hakuna Chama chenye nia ya dhati kukomboa hapo ulipo wanawatumieni kutimiza maslahi yao
Kama kina rostam wanawaamlisha mkate umeme wanufaike na bado mnakubali.matajiri wa Mabasi wanawatongoza mpaka leo reli dar moro dodoma haifunguliwi wajipigie pesa za mazwazwa.
 
Sijakuwekea maneno, nimeupanua ubongo wako, umezoea kufikiria ndani ya box kuamini njia moja tu kisiasa ndio sahihi miaka yote!.

Sio tu timu ikikosa mafanikio kocha huondoka, hata na wachezaji nao wapo wanaoondoshwa, think outside the box.

Ukishapata jibu mtuambie jina la huyo malaika wenu atakayekuja kuiongoza Chadema asikosee...



Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
 
Yoyote, ambaye kwa sasa sio Mbowe. Hatuhitaji malaika maana hata Mbowe hakuwa malaika. Labda kwako alikuwa malaika, hivyo kwakuwa mawazo yako ni ya nje ya box, na sisi tunapaswa kumtafuta malaika wetu Ili tuwaze nje ya box kama ww.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…