Pre GE2025 Ushauri: Mbowe ajiuzulu mara moja kama Mwenyekiti wa CHADEMA

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Misingi haiwezi kutupwa. Aliona mbali beberu kuachiana vijiti. Ikikosekana falsafa, kumbe tunaamini au kusimamia nini? Simple mathematics.
 
Mbowe ndio tatizo pale chadema na wenzake watatu kiukweli chama kimepoteza ata matumaini mdogo waliyokuwa nayo kwa wananchi apo awali ni kama hakuna chama cha upinzani awa jamaa wachie madaraka wamekiangamiza chama wapewe vijana wenye maono ya kisasa na new strategy za kisiasa over [emoji56]
 

1. Beberu aliona mbali sana watu kuachiana vijiti.

2. Kwa hakika kukaa sana kiti kile kile tija hupungua.

3. Ana hitaji likizo anaweza rejea siku za usoni. Tuliyaona Kwa kina Putin, Medvedev na sasa Trump yuko njia moja.

4. Siyo siri bila falsafa ya wazi chama kimepoteza mwelekeo. Hakuna tunachoamini, hakuna msimamo.

5. Tunayoyaona sasa ni matokeo ya #4, ndiyo maana leo hili kesho lile, chawa kuibuka na kushamiri, hoja kujibiwa kwa matusi, kejeli nk.

6. Mwamba kafanya mengi mazuri ya kutosha. Uko sahihi ni binadamu pakunyoosha ni kwenye falsafa, Imani, na misimamo; akipaweza karibu.

7. Kwa hakika alipo he is lost.

8. Siasa haziwezi kwenda kimachale machale, wizi wizi, ujanja ujanja nk ambayo ni matokeo ya kukosa kinachoaminiwa, msimamo yaani falsafa.
 
Sasa kama ametambua hilo na kusahihisha, shida iko wapi? Admitting weaknesses/failures is a positive attribute.
 

1. Ni hatari sana kuongea kama Mungu, Yesu, shweitwani, malaika, jini au nabii kwenye vitu ambavyo haupo 100% ushahidi wa wazi.

2. Sisi ni binadamu tu, haya maanguko yaliyokuwa yanakuja, akatokea superman kuyaepusha yanatoka wapi?

3. Tuachaneni na upigaji ramli na kujitafutia uhalali usiokuwapo.

4. Chama atapewa nani? Haya si yatakuwa yale ya jiwe tukiamnishwa ni yeye tu mwenye kuweza kuimalizia iliyoitwa miradi yake?

5. Hawakukosea waswahili waliosema "wavumao baharini nI papa lakini na wengine wapo!"

6. Hapo #5 misahafu inasema "amelaaniwa yeye amtumainiaye binadamu."

7. Ikumbukwe vyama haviendeshwi na watu kibinafsi bali kwa mujibu wa katiba.

8. Huyu bwana kafanya sehemu yake apumzike akipenda atarudi kama kina Putin, Medvedev, Trump nk.

9. Tujikite kwenye kukinyoosha chama kuwa na falsafa ya wazi; hivyo imani na misimamo thabiti.

10. Bila #9 kama ilivyo sasa, tuna bet kwenye kila jambo. Tuyaonayo haya, wala si ajabu bali matokeo kamili ya siasa za tombola.

11. Hatuwezi kuitoa CCM madarakani kwa siasa za kubahatisha.

12. Leo hii tunaongelea utengano. Tumesahau mafanikio yote ya UKAWA.

13. Tunahitaji mtu kutuongoza panapo majaliwa, kuridhiana na makundi mengine ili kuunganisha nguvu zaidi.

14. Kuwa tuna adui mmoja, kulikoni tusipigane vita moja? Mbona UKAWA ililipa?

15. Umoja ni nguvu, penye nia ipo njia:

Jan 23/24, Maandamano yahusishe wadau wote

16. #15 ni pa kuanzia hii jan 23/24, wala si mbali.

17. Pascal Mayalla kwa upekee sana niheshimu impartiality yako tokea chama mboga mboga; hii nchi ni yetu sote.

18. CHADEMA imara ni kwa maslahi yetu wote bila kujali vyama!
 
Yoyote, ambaye kwa sasa sio Mbowe. Hatuhitaji malaika maana hata Mbowe hakuwa malaika. Labda kwako alikuwa malaika, hivyo kwakuwa mawazo yako ni ya nje ya box, na sisi tunapaswa kumtafuta malaika wetu Ili tuwaze nje ya box kama ww.
Ndio mkimtafuta huyo malaika wenu sasa muwe na sababu za msingi kumkataa Mbowe, sio kila mmoja anakuja na lake mnasahau Mbowe hakuwa malaika, kama hamumtaki nendeni straight Mbowe ondoka, tena muwe na hayo mabango siku hiyo ya maandamano, sioni sababu kwenu ya kulia lia kila siku kama vile Mbowe ndie anaizuia Chadema kwenda ikulu, mkijitia upofu msizione sababu nyingine.

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
 
Suala la kuachiana vijiti sio kesi, lakini tukubaliane hivyo vijiti vya kuachiana kuna taratibu zake, sasa kama wale wanaohusika wako tayari kuendelea kuongozwa na yule msiyemtaka mnakuwa na maana na nia gani? hamjioni kama nyie ndio mnataka kuleta vurugu huko chamani?

Kwa nini hamtaki kuheshimu maamuzi ya wale wanaompigia kura Mbowe? kwanini mnajiona nyie ndio wenye hati miliki ya kuamua nani awe mwenyekiti wa Chadema? kwanini hamtaki kufuata taratibu?

Kama mna mtu wenu mnaamini ni mzuri zaidi ya Mbowe, huwa mnakuwa wapi kumwambia akachukue form ya kugombea, ili nanyi mkamfanyie kampeni apate ushindi dhidi ya Mbowe?

Hapa zisiwepo sababu za uchaguzi huwa sio huru, hizi ni sababu za waliokata tamaa na kile wanachotaka wasio na lakujitetea, huwezi kusema uchaguzi sio huru ikiwa kura hupigwa kwa uwazi, kuhesabiwa kwa uwazi, na matokeo kutangazwa wazi, pasiwepo mjumbe yeyote anayelalamikia zoezi isipokuwa wajumbe nyie wa JF!.

Kama issue ni kukaa sana, wenye uamuzi wa kumuondoa ni wapiga kura wakiona kuna haja ya kufanya hivyo, lakini msitake kulazimisha mawazo yenu na matakwa yenu ndio yawe juu ya wengine, huu ni udikteta, mnaleta vurugu, nyie ni kama vile mnaandaa mapinduzi part 2 ya kina Zitto, Mwigamba, na Kitilla yaliyofeli, sijui kama mnaiona hiyo tafsiri yenu kwa nje!.

- Msijiite wafuasi wa chama cha demokrasia huku mkitaka kumuondoa Mbowe kwa mawazo yenu binafsi.

Chadema ina taratibu zake, ziheshimiwe na kufuatwa, sio kulazimisha mambo kama vile kile ni chama cha barabarani, msikishushie heshima yake, mmekipenda kwa sababu hiyo, na muendelee kuishi hivyo, muda ukifika pelekeni mgombea wenu mfanyieni kampeni ashinde, asiposhinda; mjue hiyo ndio demokrasia, sio kulazimisha mambo yawe vile mtakavyo nje ya taratibu.

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
 
Sijui kwann watu huwa wakali na hawapendi kuukubali huu ukwel.

Sikatai, mbadala wa Mbowe hata mimi naona itachukua muda kumpata ila kwa sasa Freeman hana jipya tena. Ndio yale yale ya Mrema na lipumba yanaenda kumpata wakat angeweza kuacha kwa heshima.

Mbowe hana jipya kwasasa na ameanza kuonekana kama mjanja janja tu..Nothing more
 
Economist, Chadema ikifuata maoni na mawazo ya aina hii itaangamia. Nilipi kosa la Mbowe kufanya maridhiano? Kwa nini hasilaumiwe Samia na CCM yake walioeshidwa kutekeleza maridhiano badala yake unamlaumu Mbowe, je, ulitaka Mbowe achukue bunduki aingie msituni badala ya kukaa meza moja kutafuta muafaka wa kisiasa?
 
Hii ndio mindset ya hawa jamaa, wanataka Chadema wasio na silaha wakashindane na CCM yenye silaha physically, na wameikariri hii njia moja miaka yote!.

Swali dogo tu nimewauliza; kama maridhiano hawayataki wao walitaka itumike njia gani mbadala? ajabu hakuna hata mmoja wao aliyenijibu!

Simply wanataka kitu wasichokijua.

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
 
Nyie wanachama wa chadema acheni kulalamika mtimueni mzee mbowe kwenye chama
 

1. Wapi unapoisoma unayoiita kesi? Kulikoni kutokujikita kujibu hoja kwa hoja?

2. Wanaohusika ni kina nani ndugu? Aghalabu na sisi unaothubutu kutuita tusiohusika labda nasi pia ni nani?

3. Kwanini neno demokrasia kwenu ni shida? Kwanini mnaotaka kuleta vurugu msiwe ni ninyi?

4. Kwanini hudhani tuliompigia kura Mbowe ni sisi? Na pia kwanini mnataka kujimilikisha chama? Kwanini mnadhani mna haki zaidi kuliko wengine?

5. Kwanini hamdhani chamani tuna haki sawa? Kwanini hamuoni kuwa mnahangaika kupinga demokrasia tunayoipigania nchini na vyamani?

6. Umeandika mengi ambayo kwa hakika hayana msingi wowote!

7. Hakuna tunapolazimisha lolote wala popote, zaidi ya kuwa tunaona mnataka kutulazimisha misimamo yenu mipya isiyokuwapo. Kilichokuwa chama cha haki, uhuru na demokrasia leo kimekuwa na siasa za tombola.

8. Ustaarabu ni kuwa, kukitokea kukengeuka, demokrasia huchukua mkondo wake. Ni Hilo tu tunalolitaka kurejelewa sasa.

9. Tumesema huyu bwana ana uchaguzi mmoja, ku retreat kwenye misimamo ya chama inayoeleweka au kupumzika?

10. Kulikoni #9, ni chungu mno kwenu? Kwamba mnataka kutulazimisha na siasa za ku bet? Hiki chama ni cha umma, si mali binafsi.

11. Kulikoni ninyi kutaka kuleta vurugu hivi? Ni watu wa namna gani ninyi msioweza kuona wanachama wanataka nini?

12. Waziwazi siasa hizi za kulamba sumu hatuzitaki.

CHADEMA, ACT, CUF na wengine, na hofu ya kuonja sumu

13. Ninakazia:

hiyo #12 hatutaki
 
Chama ni chama mbowe alichorithishwa na mkwe wake,.kwa hiyo ni mali yake binafsi na siyo mali ya chama.kama unataka wewe ondoka muachie mbowe kitega uchumi chake.
 

1. Hoja iliyopo ni kuwa chama kimekosa mwelekeo, hakuna tunachoamini, hatuna msimamo.

2. Leo hili kesho lile. Imekuwa mwendo wa kimang'amu ng'amu.

3. Tunasema CCM haitatoka madarakani kwa siasa hizi.

4. Tunataka falsafa, Imani na misimamo ya wazi tujue Kwa uwazi tunasimamia nini

5. Kulikoni kuanza kuandika vitu vyako kuwawekea wengine mdomoni?

6. Kama hujui kinachoongelewa ustaarabu ni kuuliza.

7. Bottom line demokrasia ndiyo mwamuzi si mtu mmoja.

8. Kama wanachama tuna haki sawa.
 
Chama ni chama mbowe alichorithishwa na mkwe wake,.kwa hiyo ni mali yake binafsi na siyo mali ya chama.kama unataka wewe ondoka muachie mbowe kitega uchumi chake.

1. Umesharudi kutoka mapokezi, Gamboshi?



2. Usisahau huku huwa tuko macho kwa maana mwenye msafara wa mamba tunajua kenge nao huwa mko kazini.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…