Ndugu wanajukwaa,
Awali niwapongeze CHADEMA kuruka kiunzi hiki, Maamuzi yeyote kinyume na haya yasingeeleweka kwa Wanachama.
Nikirejea kwenye mada, Kumekuwa na mijadala mingi ya namna kina Mdee na wenzake wanavyoweza kusalia bungeni. Katika mijadala hii tegemeo pekee linaloonekana ni kwa kutumia mahakama.
Ikiwa watafungua shauri mahakamani, na kama inavyoonekana kwamba waligushi saini ya Katibu mkuu Mnyika na kwamba Katibu hakuwahi kupeleka majina Tume, na kama haitoshi CHADEMA wamewahi kuiandikia Tume ya uchaguzi kukanusha wao kuwateua hao wabunge, Basi jambo hilo litakuwa kutafuta kuona nyeti za kuku.
Wakienda mahakamani itabidi waseme jinsi walivyoteuliwa, Jambo hili mahakamani litamuhusisha Katibu mkuu wa CHADEMA, Watu wa Tume ya Uchaguzi.