Uchaguzi 2020 Ushauri muhimu sana kwa Tundu Lissu tukielekea Oktoba 2020

Ni kweli kabisa, kwa muundo wa serikali yetu kile kinachofanywa na serikali kina akisi moja kwa moja msimamo wa rais. Lakini ni vema kuikosoa serikali ya CCM na kuinadi serikali mbadala ya CDM.
Hapana wacha ashambuliwe yeye binafsi,kwa sababu wakati wa kampeni alikua anajinadi kuwa tumchague ajenge serikali mpya serikali ya Magufuli,Tanzania ya Magufuli Hadi Mkapa akamuonya sio serikali yake Ni ya CCm.
Wacha tu aambiwe yeye.
Ni serikali ya Magufuli,Tanzania ya Magufuli kwa sauti yake alisikika.
 
Hahahaha unenikumbusha ya Menbe anaogopa hata kutaja jina wala chama anasema anataka kumtoa bwana yule na chama kile sjui huwa anamaanisha nini
 
😂😂😂😂
Membe anaujua uzito wa mambo haya, kuna maisha baada ya uchaguzi.
 
Hilo hata Mimi nimeliona aache Mara moja kumshambulia Magufuli aje na Sera zake za maana wananchi watamuelewa hasira kejeli hazitamsaidia atawakosesha Chadema mpaka wabunge wakae nae chini wampike kisawa sawa kabla kampeni hazijaanza
 
yule jamaa ni mnafki sana, kazi kutwa kuchwa kupenda sifa

Huyu kajipanga kuwa mtumwa na tegemezi wa mabeberu,
Kupewa misaada ya ukimwi sio kosa letu ni kosa la watoa misaada kwani wao ndio chanzo cha ugonjwa, wasingeuleta tusingepewa hiyo misaada.
Sisi tuna ardhi kubwa na yenye rutuba, kupewa misaada ya chakula kwa uzembe sio sifa,
Ukiona mtu anakuwa na akiri za kijinga kutokana na makosa ya huko nyuma basi ujuwe hatoshi kuwa Raisi wa taifa linalohitaji kusonga mbele.
Aliwahi kuema raisi JK NYERERE Ni muongo alizoea uongo, leo anajifanya kutaka kuwa anamheshimu?
Hatari kabisa.
Arafu kuna wajinga na wengine na elimu zao na wana familia zao wamekaa chini wanamshabikia.
 
sasa akiacha kumchokonoa rais ataongea nini jukwaani[emoji38][emoji38][emoji38].

lissu ana akili sana anajua huko hana anachoweza kusimama akakijengea hoja, anachofanya sasa anampa jima baya mbwa ili achukiwe.

nimemsikiliza sehemu anasema rais anajisifu kwa kujenga bwawa la umeme wakati kuna mtera, nikajisemea doh hapa hamna kazi.
 
#2 kuteswa na kulengwa moja kwa moja na utawala huu hili siliamini mpaka kesho,huyu alilengwa na maadui zake tu wala asitudanganye.

Serikali yoyote duniani ilivyo na mkono mrefu iende ikafanye vitu kitoto namna hiyo wapi na wapi,huyu atakua na maadui zake tu huko ndani ya chama,au aliwahi kumpindishia mtu sheria, au aligongwa na mabeberu moja kwa moja kuchafua taswira ya nchi na wakageuka kumsaidia na kumlazimisha amtukane Rais ambaye sisi wananchi tunaona wazi kua tuna Rais anayetupigania usiku na mchana

NB: inawezekana kabisa mabeberu yamemuwekea hata vinasa sauti na yeye anajua au anahisi, hivyo basi ni lazima kwake kuropoka ropoka ili wamsikie huku yeye pia akilenga mamilioni ya pesa wanayompa yasije yakakata

Tundu ni muhuni tu na siamini kama kuna siku moja MUNGU anaweza kumteua huyu maana hakuna mamlaka inakuja kwa kupiga tu kura isipokua kwa maamuzi ya MUNGU mwenyewe
Huo mkono mrefu umeshindwa kuwajua au kuwakamata hao maadui wa lissu waliopo ndani ya chama au mabeberu wanaoichafua serikal tukufu?

Au hao maadui zake eti "aliwahi kuwapindishia sheria" , lissu ni hakimu au jaji?
 
sasa akiacha kumchokonoa rais ataongea nini jukwaani[emoji38][emoji38][emoji38].

lissu ana akili sana anajua huko hana anachoweza kusimama akakijengea hoja, anachofanya sasa anampa jima baya mbwa ili achukiwe.

nimemsikiliza sehemu anasema rais anajisifu kwa kujenga bwawa la umeme wakati kuna mtera, nikajisemea doh hapa hamna kazi.

Kumbe na wewe umeliona hilo?
Sasa tunasubili sera zake yeye ataleta vitu vipi ambavyo havijaanzishwa hapa TZ
 
Huyu kajipanga kuwa mtumwa na tegemezi wa mabeberu,
Kupewa misaada ya ukimwi sio kosa letu ni kosa la watoa misaada kwani wao ndio chanzo cha ugonjwa, wasingeuleta tusingepewa hiyo misaada.
Sisi tuna ardhi kubwa na yenye rutuba, kupewa misaa ya chakula kwa uzembe sio sifa,
Ukiona mtu anakuwa na akiri za kijinga kutokana na makosa ya huko nyuma basi ujuwe hatoshi kuwa Raisi wa taifa linalohitaji kusonga mbele.
Aliwahi kuema raisi JK NYERERE Ni muingo alizoea ungo, leo anajifanya kumtaka kuwa anamheshimu?
Hatari kabisa.
Arafu kuna wajinga na wengine na elimu zao na wana familia zao wamekaa chini wanamshabikia.
hueleweki
 
Ni wazi kuwa Lissu amekuwa mwanaharakati wa kutetea haki za wananchi kwa miaka mingi, pia ni wazi kuwa kwa sasa yeye ndiye mwanasiasa pekee wa upinzani mwenye uwezo wa kumtikisa Magufuli.

Lakini kuna mambo machache ningependa kumshauri ayazingatie atakavyoendelea na kampeni zake kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka huu.

1. Aache kumshambulia Magufuli binafsi
Naamini kuna watu wengi tu wamemshauri juu ya hili, ni muhimu sana kulizingatia hili. Ni vema kuielekezea mashambulizi serikali kwa ujumla na chama cha CCM badala ya kumshambulia Magufuli.

Hata Magufuli akitaka kurusha vijembe upande wa pili mara nyingi hua hataji majina ya watu. Anaepusha mgongano wa hoja kugeuka kuwa ugomvi binafsi.

2. Ajikite kwenye matatizo yanayowagusa wananchi wengi
Japo kiubinadamu ni ngumu sana kufanya hili ukizingatia yeye binafsi alivyoteswa na kulengwa moja kwa moja na utawala huu lakini ajitahidi kuachana na 'personal vendetta' dhidi ya serikali akiwa jukwaani.

Watu hawakuchagui ili ukatimize hasira zako bali ili ukatatue changamoto zao. Kuna mengi ya kuongelea kila sehemu, watumishi, wakulima, wafanya biashara, wahitimu wa vyuo n.k

Lakini pia kuna ukatili wa polisi na kuminywa kwa demokrasia na uhuru, bila kusahau sheria na kanuni za kishenzi za awamu ya 5.

3. Ajizuei kutumia lugha kali
Najua Lissu ni bingwa wa kutibua nyongo za wapinzani wake, namshauri sasa kwakua anawania ofisi ya juu kabisa hapa nchini basi ajitahidi kuongea kama rais mtarajiwa. Lugha za kejeli na kukashifu hazifai kutolewa na kiongozi mkuu wa nchi.

Ni hayo tu machache, natumaini ujumbe umefika.

Ushauri wako ni mzuri sana na ninategemea utafanyiwa kazi. Ila ninapenda kuboresha sehemu kadhaa kwenye ushauri wako.
  1. Ni kweli aishambulie zaidi ccm na serikali. Lakini itakuwa ngumu moja kwa moja kwa kutomahambulia Magufuli, maana Magufuli yeye binafsi kajigeuza ndio ccm na ndio serikali. Kama yeye binafsi anajitahidi kujiweka kuwa juu ya hizo taasisi na anataka sifa ziwe kwake kwanza,kisha taasisi, unamtengaje hapo na mashambulizi direct?
  2. Ushauri wako hapa uko sahihi kwa 100%
  3. Lugha kali kwa sasa zinatisha watu, kutokana na saikolojia ya hofu iliyojengwa na awamu hii ya tano. Kuna aina fulani ya ukondoo watanzania wamejengewa kimfumo wa kutaka kuonyeshwa utawala uliopo uko sahihi, na wala hakuna haja ya kuhoji wala kukosoa, na iwapo utafanya hayo, basi iwe kwa lugha ya kubembeleza. Enzi za kina Mtikila waliongea lugha kali zaidi ya hizi na hakukuwa na tatizo lolote. Unapotaka kushindana na mtu kama Magufuli, hupaswi kutumia lugha laini kama unatongoza, lazima utumie lugha ya kupandisha saikolojia ya watu wako kuwa unajiamini. Pepo huwa anakemewa, sio mambo ya " na ww pepo si utoke jamani, mbona uko hivyo?"
 
#2 kuteswa na kulengwa moja kwa moja na utawala huu hili siliamini mpaka kesho,huyu alilengwa na maadui zake tu wala asitudanganye.

Serikali yoyote duniani ilivyo na mkono mrefu iende ikafanye vitu kitoto namna hiyo wapi na wapi,huyu atakua na maadui zake tu huko ndani ya chama,au aliwahi kumpindishia mtu sheria, au aligongwa na mabeberu moja kwa moja kuchafua taswira ya nchi na wakageuka kumsaidia na kumlazimisha amtukane Rais ambaye sisi wananchi tunaona wazi kua tuna Rais anayetupigania usiku na mchana

NB: inawezekana kabisa mabeberu yamemuwekea hata vinasa sauti na yeye anajua au anahisi, hivyo basi ni lazima kwake kuropoka ropoka ili wamsikie huku yeye pia akilenga mamilioni ya pesa wanayompa yasije yakakata

Tundu ni muhuni tu na siamini kama kuna siku moja MUNGU anaweza kumteua huyu maana hakuna mamlaka inakuja kwa kupiga tu kura isipokua kwa maamuzi ya MUNGU mwenyewe

Beberu gani ana shida na Tanzania? Sisi bado tuko kwenye hatua ya kunawa mikono baada ya kutoka chooni, ndio wa kuwasumbua hao mabeberu? Mabeberu waache kudeal na nchi ziliko kwenye hatua ya kutengeneza nyuklia, ndio waje wahangaike na watu wanaoshangilia kwa vifijo kuwa rais kapewa jogoo huko porini?

Ni kweli serikali ina mkono mrefu, lakini ni mkono ulioopoza au huo urefu wake ni wa kuwakomoa wasiomsujidia jiwe. Hayo anayosema Lisu kuhusu shambulio lake yako hivyo hivyo mpaka uchunguzi ufanyike na ukweli uwe hadharani.
 
Ni wazi kuwa Lissu amekuwa mwanaharakati wa kutetea haki za wananchi kwa miaka mingi, pia ni wazi kuwa kwa sasa yeye ndiye mwanasiasa pekee wa upinzani mwenye uwezo wa kumtikisa Magufuli.

Lakini kuna mambo machache ningependa kumshauri ayazingatie atakavyoendelea na kampeni zake kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka huu.

1. Aache kumshambulia Magufuli binafsi
Naamini kuna watu wengi tu wamemshauri juu ya hili, ni muhimu sana kulizingatia hili. Ni vema kuielekezea mashambulizi serikali kwa ujumla na chama cha CCM badala ya kumshambulia Magufuli.

Hata Magufuli akitaka kurusha vijembe upande wa pili mara nyingi hua hataji majina ya watu. Anaepusha mgongano wa hoja kugeuka kuwa ugomvi binafsi.

2. Ajikite kwenye matatizo yanayowagusa wananchi wengi
Japo kiubinadamu ni ngumu sana kufanya hili ukizingatia yeye binafsi alivyoteswa na kulengwa moja kwa moja na utawala huu lakini ajitahidi kuachana na 'personal vendetta' dhidi ya serikali akiwa jukwaani.

Watu hawakuchagui ili ukatimize hasira zako bali ili ukatatue changamoto zao. Kuna mengi ya kuongelea kila sehemu, watumishi, wakulima, wafanya biashara, wahitimu wa vyuo n.k

Lakini pia kuna ukatili wa polisi na kuminywa kwa demokrasia na uhuru, bila kusahau sheria na kanuni za kishenzi za awamu ya 5.

3. Ajizuei kutumia lugha kali
Najua Lissu ni bingwa wa kutibua nyongo za wapinzani wake, namshauri sasa kwakua anawania ofisi ya juu kabisa hapa nchini basi ajitahidi kuongea kama rais mtarajiwa. Lugha za kejeli na kukashifu hazifai kutolewa na kiongozi mkuu wa nchi.

Ni hayo tu machache, natumaini ujumbe umefika.
Nani kati ya Lissu na Magufuli ana lugha ngumu yenye kuudhi isiyo na staha?
 
Back
Top Bottom