USHAURI: Nataka kuacha kazi ila nina mkopo Benki

USHAURI: Nataka kuacha kazi ila nina mkopo Benki

Huu ni ujinga!! Badala ya kutumia kazi kulipa mkopo na pia kuendeleza biashara unataka kuacha kazi?
 
Habari za asubuhi?

Kama kichwa cha Habari kinavyojieleza nimeajiriwa na serikali taaluma yangu ni Daktari wa binadamu (medical doctor) kuna mkopo nimechukua wa thamani ya mil 35. Nimefungua pharmacy pamoja na maabara.

Nataka niache kazi nisimamie biashara zangu. Je, nikikimbia serikali haiwezi kunitafuta kunipeleka mahakamani ili nilipe deni lao?

Je, hata wakinipeleka mahakamani wakitaka nilipe deni nitalipa vipi wakati kazi sina?

Au watanifungulia kesi ya uhujumu uchumi?

Naombeni ushauri katika hili?

NB: Lengo la kupata ajira serikalini ili nipate mkopo na kufungua miradi yangu kwa haraka na si kufanya kazi na serikali
Kwa utaratibu wa kuacha kazi kama ulivyosema ni lazima ulipe mkopo hivyo utapoteza ajira na fedha.

USHAURI:
1.Subiri mpaka utakapomaliza mkopo wako au kama una kiasi cha pesa cha kulipa sasa lipa kiasi kilichobaki(ukilipa kiasi kilichobaki benki sasa huwa ni kidogo ukilinganisha na kiasi utakacholipa mpaka mkopo kuisha).
2. Simamia mradi wako ukiwa kazini,kumbuka kuwa mwezi July,2022 mshahara utaongezeka.
3. Panga kufanya jambo la kiutumishi na siyo kitaaluma(ili ulinde cheti cha taaluma) ambalo litakuondoa kazini haraka(yaani termination of contract) mwajiri akuondoe kazini yeye.

N.B. USHAURI NAMBA MBILI UZINGATIWE.
 
Ndugu, ukiacha kazi mwenyewe utalipa mkopo huo. Bima ya mikopo haijumuishi kuacha kazi kwa hiari hivyo kama utaacha kwa hiari utadaiwa bila shida.
Ila ikitokea umepoteza kazi kwa njia yoyote ile ya bila kupanga mwenyewe either kufukuzwa, kupunguzwa, kuugua, ulemavu, kifo na mengine kama hayo hakika hawawezi kukudai kwa sababu mdhamini ilikuwa kazi yako.
Ukiacha kwa hiara wanatafasiri kwamba una njia nyingine ya kulipa mkopo huo hivyo mwajiri atajitoa kwenye udhamini.
Hivyo kama unataka kutodaiwa baada ya kuacha kazi tafuta namna yoyote ya kuondolewa kazini ambayo haitatafisiriwa kwamba umeamua kuacha kwa hiari.
 
Kama biashara yako inalipa; itumie hiyo biashara kukopa ili kurejesha mkopo, wa awali.
 
Usimdanganye kumbuka amedhaminiwa na Serikali so akiacha kuna mengi atapoteza hadi alipe ikiwepo Leseni ya Udaktari
Hawez nyanganywa Lesen. Mkopo na Lesen wapi na wapi. Të amedhaminiwa na serikal, so benk wataenda serikal Kwa mdhamini kujua wapi alipo na serikal ndo imtafute. Usumbufu anaweza pata pata Hasa akiwa jiran maeneo ya kaz ya zaman
 
Hawez nyanganywa Lesen. Mkopo na Lesen wapi na wapi. Të amedhaminiwa na serikal, so benk wataenda serikal Kwa mdhamini kujua wapi alipo na serikal ndo imtafute. Usumbufu anaweza pata pata Hasa akiwa jiran maeneo ya kaz ya zaman
So wakikupata na ukasema huna hela nini kinafuata
 
Kesi lazima Ukutane Haitokuwa Ya Uhujumu uchumi bali Ya Madai Ambayo inaweza simama pia kama jinai.. Na kama isemavyo sheria ya madai inatoa Haki ya Mahakama kukamata mali za Mdaawa Ili kulipa Deni Hivyo Mkopo utalipwa kwa mali zako kukamatwa mafano wa mali zinazoweza kukumatwa ni hyo phamacy uliyonayo.
Sio kweli
Dhamana yake ilikua ni ajira, ajira ikiisha na mkopo umeisha.japo bank watakuwa wanampigia simu kumbembeleza alipe, narudia tena watakua wanambembeleza Ila ikipita muda wakiona kimya basi atakuwa defaulter tu na hawana Cha kufanya Tena
 
Dhamana ya mkopo wako ilikuwa ni nini?

Kama ilikuwa ni Asset zako binafsi,upo huru kuacha kazi ila kama ni kazi yako kupitia mshahara wako basi huwezi kuacha kazi kwa namna yoyote ile mpk pale mkopo wako utakapoisha
Mnacomment huku mkiwa hamjui kitu, hii ndio shida ya watanzania.
Dhamama hapo ni mshahara wake, aliacha kazi, akifukuzwa au akiwa retrenched basi na mkopo unakua ndio umeisha hivyo landa itategemea na yeye akiamua kuendelea kulipa kwa anavyojua yeye.
Bank watakuwa wanampigia simu kumuuliza kuhusu Hilo deni lake na hawatakua na cha kufanya zaidi ya kumsubiri alipe Ila baada ya muda wataachana nae na ataingizwa Kama defaulter.
 
ingekua enzi za Kikwete ungeacha kazi tena bila taarifa, na hilo deni lingeendelea kukatwa ktk mshahara wako (ungekua huupati)
Ila kwasasa hiv usijaribu kufanya upuuzi wowote utafia jela unajiona, utafilisiwa na utaona maisha machungu... Sasa hivi serikal haijumuwi watch out
Ni heri uvumilie
 
Process ya kuacha kazi ni pamoja na kukabidhi ofisi na wakati anafanya clearance ndio atakutana na deni lake, dhamana muhimu ni leseni ya Udaktari wakirevoke inakula kwake
Huenda wengi humu hamjui chochote. Kuacha kazi sio lazima ukabidhi ofisi, japo kiungwana inapaswa kuwa hivyo.
Unaweza kuwapa 24hrs na ukaachana nao
 
Acha kutufanya ma mburura daktari kashavuka level yako ya kufikiri hayo maswali ni ya la sita D
 
Mnacomment huku mkiwa hamjui kitu, hii ndio shida ya watanzania.
Dhamama hapo ni mshahara wake, aliacha kazi, akifukuzwa au akiwa retrenched basi na mkopo unakua ndio umeisha hivyo landa itategemea na yeye akiamua kuendelea kulipa kwa anavyojua yeye.
Bank watakuwa wanampigia simu kumuuliza kuhusu Hilo deni lake na hawatakua na cha kufanya zaidi ya kumsubiri alipe Ila baada ya muda wataachana nae na ataingizwa Kama defaulter.
Sawa Manager wa NMB Bank tawi la Makumbusho
 
Huenda wengi humu hamjui chochote. Kuacha kazi sio lazima ukabidhi ofisi, japo kiungwana inapaswa kuwa hivyo.
Unaweza kuwapa 24hrs na ukaachana nao
Huenda na wewe kuna kitu hujui kutoa notice ya saa24 unatakiwa kulipa gross salary ya mwezi m1 kwa mwajiri na atazuia michango yako ya Pspf, na atahakikisha unalipa
 
Umesoma, unaelewa, deni lazima lilipwe.

Piga hesabu ya mafao yako kama yatatosha kulipa deni, kabidhi kistaarabu ukafanye yako,

Unless hakikisha kuwa mradi wako unaweza kulipa mkopo, resign from employment hama na deni lako uendelee kulipa,

Ukiona vipi ajiri.

Nothing to hide, una tin nida no where to sepa,
 
Back
Top Bottom