Ushauri: NEMC fanyeni haya ili kupunguza kelele za muziki mtaani

Ushauri: NEMC fanyeni haya ili kupunguza kelele za muziki mtaani

Hii nchi ngumu sana, kuna wale wanauza dawa za mende sijui panya yaaani wana spika zao zinazingua sana, na mabodaboda yanawekz miziki kwa sauti ya juu na wenye convenient stores, ana uza beers, ana mteja mmoja anafungulia mziki sauti mpaka mtaa wa tatu. Nchi ngumu sana, washamba ni wengi sana
Ama kweli msemo wa mtaa mada " Bongo wanaona ni haki yao kukera wengine "
 
WABONGO unawajuwa lakini wewe? Wataomba kibari cha piano! Lakini huko ndani watafunga busta za sebene!
Ndomboro ya yesu itapigwa kama kawa! Na watatoa ushuhuda kwamba yesu katenda miujiza ya busta
Kuna stika nimesema zinabandikwa seal
 
Kuna haya makanisa uchwara yanapiga kelele unakuta wamekodi nyumba kwenye makazi ya watu, usiku wanatumia speaker usiku kucha waweza usilale na wao hawajali waanze kupigwa fine
Ndo changamoto hiyo
 
Nafaham upo ugumu mkubwa wa kushughulika na watu wanaoamini KERO ni haki yao!

Yaani kuna watu wanajimilikisha haki ya kuwakera wengine!
Na wanaoamini wako sahihi!

Zamani kukuta spika ya disco kanisani ilikuwa HAKUNA! Na watu waliogopa kucheza sebene kanisani lakini hivi Leo ni kawaida sana!

Miziki mikubwa kwenye bar, makanisa na misikiti imekuwa kawaida na wanaamini ni HAKI YAO!

NEMC FANYENI HIVI KUONDOA TATIZO!
1. Wekeni viwango elekezi vya decibel's ya chombo cha mziki kwa kuzingatia uwiano wa chumba/jengo (Volume ratio) ya chumba na muwape vibari!

Fomu za vibari NEMC zijazwe kupitia serikali ya mtaa na mtendaji wa mtaa (hii itakuwa bure kwa vyombo vyote vidogo vya mziki mfano! Koni spika, na vinanda vidogo (piano)

2. Spika zote kubwa kuanzia decibels elekezi mtakazopanga na kuendelea kutokana na uwiano wa jengo.
Hakikisheni Zinapatiwa kibali maalum kutoka NEMC

MFANO! spika moja kubwa kwa mwaka ilipiwe 10MIL na hakikisheni nakala ya stika ya vibari vyenu vinabandikwa inje ya jengo husika
Vikionesha tarehe, muda wa matumizi, na ukomo!
(Hakikisheni na mkague vibari vyenu VALID kama vimebandikwa inje)

Asilimia 30% ya malipo wapeni mtaa husika kwa maendeleo ya mtaa!

HAKIKISHENI HAKUNA MTU ANAYETUMIA SPIKA KUBWA YENYE DECIBEL'S kinyume na kiwango elekezi pasipo USAJILI!

NA MJIPAMBANUE KWAMBA HAMUWAKATAZI KUTUMIA BALI MNAWASAJILI NA KUWAPA MATUMIZI ELEKEZI! Anaeshindwa aaache!

Nahilo lifanyike kitaifa!
Nani wa kumfunga paka kengele wakati wa kampeni miziki kila kona hata mbio za mwenge nazo kelo mwenge unapo lala mtaa huo watu wote watakesha kwa kelele na vibaka na uzinzi matangazo ya makampuni ya simu pombe kelo bado makanisa kitu kibaya zaidi jafo ajiwezi kabisa wizara ilisha mshinda yupo yupo tu
 
Research sheria za serikali za mitaa (municipalities )zipo sheria zinazohusu mambo haya including maduka ya kiti moto,utekelezaji ni zero
Kanisa lipige kelele ulipeleke serikali ya mtaa kwanza wakiitwa awaendi chezea kanisa wewe
 
Kanisa lipige kelele ulipeleke serikali ya mtaa kwanza wakiitwa awaendi chezea kanisa wewe
Sisi tulikwenda serikali ya mtaa, tukawaelezea kero yetu ya mziki mkubwa wa kanisani, wakaitwa wakasema wana kibali kipindi mwenyekiti wa serikali ya mtaa alikuwa anatokea Chadema na sasa ni CCM hivyo hawana uwezo wa kuwakatalia. Wanasali Mala 5 kwa week, Jumapili saa moja asubuhi ni lazima muamke. Mziki mkubwa kama uko nao ndani.
 
Mkuu umeandika points sana sana tatizo ni hawa wahusika NEMC wapo maofisini tu kusubiri mishahara na kwenda kupiga 'deal' kwa watu wanaoingiza mifuko ya plastics!
 
Sisi tulikwenda serikali ya mtaa, tukawaelezea kero yetu ya mziki mkubwa wa kanisani, wakaitwa wakasema wana kibali kipindi mwenyekiti wa serikali ya mtaa alikuwa anatokea Chadema na sasa ni CCM hivyo hawana uwezo wa kuwakatalia. Wanasali Mala 5 kwa week, Jumapili saa moja asubuhi ni lazima muamke. Mziki mkubwa kama uko nao ndani.
Kuna pesa za bure kwenye hivi vyombo vya mziki serikali kusanyeni pesa za maendeleo jamani! Mkajenge madaraja!
Tokomezeni kero kwa faida!
 
Kuna haya makanisa uchwara yanapiga kelele unakuta wamekodi nyumba kwenye makazi ya watu, usiku wanatumia speaker usiku kucha waweza usilale na wao hawajali waanze kupigwa fine
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] wee dear
 
Wameshindwa kucontrol vituo vya mafuta ile sheria hawaifuati, wataweza kwenye miziki kweli, haya njoo mipango miji kila nyumba ina fremu ya biashara ndio maana hata sipermarket au malls kwa Tanzania hazina deal, wangeweka wazi makazi ya watu hapatakiwi kuwe na viduka au vifremu tungekua na makazi bora yenye utulivu lakini sasa ni balaa
 
HAKIKISHENI HAKUNA MTU ANAYETUMIA SPIKA KUBWA YENYE DECIBEL'S kinyume na kiwango elekezi pasipo USAJILI!
Sijui Kama unaelewa ulichoandika

Yani ninunue speaker yenye sentivity ndogo eg 100w 78Db Chinese one niache candy 100w 98db?

Hapa enyewe tuna repair coil za candy 18inch double bass 2000w RMS jpil tuna kiwasha Ni kusifu na kuabudu
 
Bahati nzuri bidhaa zote zinajulikana sokoni! Za kubumba zinajulikana!

Na mbali na specification! NEMC wanaweza kutumia mashine maalum ya kupimia kiwango cha mtetemo (DECIBEL'S METER au SOUND METER)
Hili zoezi NEMC wakiamua hamtoboi popote na janja janja! Wakishindwa wabinafisishe hilo zoezi la USAJILI wa spika! Halafu NEMC wabakie kuratibu na kuhakiki na kusikiliza kesi
 
Kwa upande wa misikiti ni swalah tu ya asubuhi mchana na njion kwa muda wote wanaotumia haizidi hata dakika 15 kwa siku nzima. Wakatholiku ni kengere ya asubuhi mchana na jion . Lakini Kuna wale walokole ukweli wanakera
Siku hizi baadhi ya makanisa kama vilabu vya pombe za kyenyeji
Swala unamuwekea Nani speaker nje tafuteni spika nzuri frequency za zile horn speaker zenu zinakera Sana

Sa 5:30am nasikia swala Ni kelele tu ambazo sielewi wanaongea nini
 
Swala unamuwekea Nani speaker nje tafuteni spika nzuri frequency za zile horn speaker zenu zinakera Sana

Sa 5:30am nasikia swala Ni kelele tu ambazo sielewi wanaongea nini
Wasibague Bali zoezi liwe la kitaifa na liguse kila mtumiaji wa mziki mkubwa mtaani lazima awe na kibali!
 
Back
Top Bottom