Ushauri: Niende Serikalini au nibaki private sector

Kwanini usifanye kazi zote mbili sababu wewe ni 2in1
Anyway sijawahi fanya kazi serikalini na suitokuja kufanya japo niliwahi pata nafasi ya kwenda kufundisha DIT nikaamua kubaki zangu private sector
Hahaha we jamaa umewaza nje ya box
 
1.Niliomba taasisi kubwa ya serikali mzee na ningepata huko nisingejishauri kwa chochote ningeenda sema nilikosa nafasi jina likabaki kwenye database ndio wamenipangia huko halmashauri sahv ambapo sikuombea ajira nimepangiwa tu
2.Mechanical Engineer
 
ni ngumu kukushauri, because hatujui terms za huko private Vs public!
 
1.Niliomba taasisi kubwa ya serikali mzee na ningepata huko nisingejishauri kwa chochote ningeenda sema nilikosa nafasi jina likabaki kwenye database ndio wamenipangia huko halmashauri sahv ambapo sikuombea ajira nimepangiwa tu
2.Mechanical Engineer
Ndio umepangwa halmashauri ya nzega mkuu
 
Mwenye jibu ni wewe mwenyewe.Kwa sababu ni wewe uliyeomba hiyo kazi huko serikalini huku ukiwa muajiriwa wa private sector.Je ulilenga nini kuomba kazi wakati una kazi?mbona umezuia nafasi za wenzako.
Hana budi kuachia kijiwe aendee huko serikalini aliko kutaka
 
fuata huu ushauri utakuja kushukuru baadaye.
 
Nenda serikalini mkuuu awamu hii serikalini kuna pesa acha kuwaza
 
Mkuu baki private sector ila jitahidi uwe unawekeza pesa kama kununua Viwanja na kufungua Biashara za kukuingizia extra income.Dar es salaam kuna opportunities nyingi kuliko Tabora na pia serikalini utakacho ambulia labda job security compared to private sector.
 
Dj niletee watu wa "take it from me, utakuja kunishukuru baadae"
 
1.Niliomba taasisi kubwa ya serikali mzee na ningepata huko nisingejishauri kwa chochote ningeenda sema nilikosa nafasi jina likabaki kwenye database ndio wamenipangia huko halmashauri sahv ambapo sikuombea ajira nimepangiwa tu
2.Mechanical Engineer
OK.
1. Hapo na. moja umeipiga chenga (umekwepa) hoja yangu kwenye post #55. Lakini hiyo itoshe tu kukuhakikishia Serikali ni MOJA Tanzania hiyo kuitwa H/W au Central Gvt. au Taasisi haijalishi kitu alimradi ni ndani ya Serikali na ndo mana wakakupanga kule ambako ww kwa imani yako unasema hukuomba. Iko hv; Ukiomba Serikalini wao kama Serikali huangalia ni wapi pana upungufu na uhitaji mkubwa wa Taaluma yako na huko ndiko watakupanga.
2. Hongera sana kuwa umebobea katika Mechanical Engineer. Kwenye Halmashauri ndiko hasa Taaluma yako inahitajika - unless useme hupendi kuwa chini ya DED. Halmashauri ndizo ziko frontline tena karibu zaidi na wananchi na ndiko miradi yote hutekelezwa. Ukiwa Fundi mitambo na umeajiriwa Serikalini e.g. kiwandani n.k. bado wanaweza kukuhamishia Halmashauri au kukushikiza (on secondment basis) katika Taasisi nyingine hata zile za kutoka nje ya nchi na huwezi kataa. Kumbuka ukiomba kazi Serkalini hauombi kituo cha kazi. Utapangiwa popote Tz. Ndo mana wakakupanga Tabora.
 
πš–πš£πšŽπšŽ πš”πš’πš–πš‹πš’πšŠ πš‘πšŠπš›πšŠπš”πšŠ 𝚐𝚟𝚝, πšœπš‘πšŠπšžπš›πš’ πš’πšŠπš”πš˜ πš˜πšπšπš’πšŒπšŽ πš£πš’πš”πš’πšžπš—πšπšžπšŠ πš‘πšžπš”πš˜ πšžπš•πš’πš™πš˜ πš—πšπš’πš˜ πš‹πšŠπšŠπšŠπšŠπšŠπšœπšœπšœ πš—πšπš’πš˜ πš‹πšŠπšœ πšπšŽπš—πšŠ.
πš‚πšŠπšœπšŠ 𝚠𝚎𝚠𝚎 πš“πš’πšŒπš‘πšŠπš—πšπšŠπš—πš’πš’πšœπš‘πšŽ 𝚝𝚞 πš™πš›πš’πšŸπšŠπšπšŽ (πšžπšœπš’πš›πš’πš—πš’)
 
Private kuna majungu na fitna mkataba mpaka umnyenyekee mtu hapana private hata wanipe million 10 kuna jamaa aliacha kazi private licha ya kulipwa hela nyingi kwasababu ya majungu na fitna mkuu nenda serikalini kuna siku utakuwa na familia.
 
Kama siyo competent wahi serekalini kule hata uwe mbabaishaji unaenda kazini hufanyi kazi unazurura tu kutoka ofisi hii kwenda ofisi ile hadi jua linazama mshahara utapata wakikuchoka na ubabaishaji wako wanakuhamisha tu
Ila huo ujanja ujanja usiujaribu private sector wanakutumbua kabla hujavuta pumzi ya pili
 
Private kuna majungu na fitna mkataba mpaka umnyenyekee mtu hapana private hata wanipe million 10 kuna jamaa aliacha kazi private licha ya kulipwa hela nyingi kwasababu ya majungu na fitna mkuu nenda serikalini kuna siku utakuwa na familia.
Hapo kuwa na familia sijaelewa point yako mkuu
 
Hapo kuwa na familia sijaelewa point yako mkuu
Mimi nimefanya kazi private company tena international walikuwa wanalipa vizuri sana ila kwa fitna zile kuna siku watakupiga tukio hutaamini nina visa vingi ila nakushauri nenda serikalini ukithibitishwa chukua mkopo kama million 12 fanya bussness endelea kupiga kazi usiwe kama wale washamba anachukua mkopo wa kwanza kijana mdogo ananunua gari mwingine anajenga tena nyumba ya kukaa mbali na anapofanyia kazi nenda serikalini chukua mkopo fanya bussness sasa huo mkataba wa miaka mitatu ni bank gani itakupa mkopo labda oya microfinance siku ukija kuwa na familia kama hauna utakuja kunielewa vizuri.
 
Wee bhana usimdanganye mwenzio. Unasema eti "Kama siyo competent wahi serekalini kule hata uwe mbabaishaji unaenda kazini hufanyi kazi unazurura tu kutoka ofisi hii kwenda ofisi ile hadi jua linazama mshahara utapata wakikuchoka na ubabaishaji wako wanakuhamisha tu....." sio kweli. Cjui kwa siku hIzi lakini siku za nyuma kulikuwa na fomu za kujaza almaarufu kama OPRAS.
 
Sasa sijui unabisha nini
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…