Ushauri: Nifanyeje juu ya hali hii ya maisha yangu?

Kusema kweli naona makelele tu ,sioni solution ya kumsaidia mtoa mada
 
Inasikitisha. Hii serikali badala ya kuendelea kunyonya nguvukazi ya vijana kama wewe ningeshauri waweke utaratibu wa kuwaajiri vijana waliyojitolea mfululizo japo kwa miaka minne. Hua navyojua wanatoa mikataba mifupifupi ili kuepa sheria inayosema mtu akiajiriwa kwa muda fulani mfululizo kama kibarua inabidi spewe ajira kwa kudumu. Sio vyema serikali kutumia mbinu za waajiri binafsi kunyonya nguvukazi ya vijana wake.
 
Kuwa na malengo mengi kwa wakati 1 it means unakimbiza vipepeo wengi kwa wakati mmoja mwisho wa siku wote wanaruka na kuwakosa ushauri wangu chagua jambo moja unaloliamini sana kukuvusha komaa nalo la sivyo ukitaka kukamaa na yote mwisho wa siku hautafanikiw hata moja tumia 10000 save 5000 walinzi wanalipwa laki 1.5 hadi laki mbili na wanabalance matumizi yao kwa mwezi
 
Ajira ni ngumu sana siku hizi, unajitolea miaka kadhaa mahala na wakitoa ajira wanaajairi vijana wengine tuu maana wanachojali wao ni ufaulu wa kwenye usaili tuu. Mtihani utokane na kada yenu halafu wewe mwenyewe mwenye uzoefu na hapo, na mtihani umejibu vizuri ila unafeli, vijana wasiofanya kazi hapo wanafaulu kwa viwango vya juu, nadhani kuna suala la anakujua nani au rushwa huko juu. Mungu atusaidie sana vijana tunapitia wakati mgumu sana.
 
Sawa.
 
Ahaaah, ngoja ntajaribu nione. Tatizo huwa wanakataa kutupatia kazi ya ualimu maana hatujasoma masomo ya ualimu, na Wapo sahihi kwa kigezo chao cha kuhitaji mwalimu aliyesomea hiyo kazi. Japo ninaweza kufundisha na nimefundisha sana wanafunzi.
Nenda hapo ,uje ulete mrejesho
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…