Ushauri: Nimepewa RB kwa kosa la kufanya fujo kanisani

-Polisi hawakumkomalia, ndio maana wakampa dhamana maana ni haki ya mtuhumiwa.
-Polisi ni kazi yao kupokea kila taarifa itolewayo kituoni na kuichukulia hatua na ndio maana kwa uzito wa kosa walitumia busara ya wito na sio kwenda kumfuata.
Polisi hakuepo eneo la tukio, kimpasacho ni kupokea taarifa na kuifanyia kazi, yaani kuchunguza namna kosa lilivyo tokea, na kwavile chanzo hapo ni mgogoro wa kifamila, na polisi wanajua kua kosa la shambuli anaetakiwa kulalamika mi mke na sio mchungaji wa kanisa, pia polisi sio wajinga wakapeleke kosa hilo mahakamani wakati wanajua kua ndoa itakua na mpasuko na tabu itakua kwa watoto, na Polisi ndie mlinzi wa watoto kisheria.
Pia kwa kosa la shambulio ni mahakama ya mwanzo na hukumu yake ni faini, na faini ni pesa ya serekali na sio ya alie lalamika, kosa hilo hafungwi.
Kosa la kufanya fujo pia nalo sana, hata kanisa wafanyeje, hawawezi kulifanya kua kubwa, na hukumu itategemea na thamani ya uharibifu wa mali, tofauti na hapo kama hakuna thamani nayo ni kupigwa faini, kwa kwa makosa yote hayo faini haivuki laki 2 hata kama kuna uharibifu wa mali. Hiyo ndio kisheria.
Polisi wanajua fika kua ili udhaminiwe unatakiwa ktk wadhamini kuwe na mwanaume, na kama ni mdhamini ni mmoja basi awe mwanaume, lakini polisi walimdhaminisha kwa mama mkwe yani mwanamke, hio ni dalili kua hapo hakuna kesi.
Pia hapo kanisani mchungaji sio msemaji wa mwisho na iko wazi kabisa kua kanisa ndio linaiharibu hiyo ndoa, mzee wa kanisa hawezi kutia aibu kanisa lake kwa kwenda mahakamani kuaibika kwa kusimamia kukosa haki ya msingi ya watoto wa miezi minne kunyonya. Atakosa waumini.
Na polisi hawataacha kuuliza swali la msingi kwa mchungaji ktk maelezo yake ya kua, je! Huoni kwamba wewe utakua chanzo cha ndoa hii kufa?
 
Umeeleza vizuri Kwa uelewa wako mdogo wa sheria hapo Kuna kesi nyingi tu Kuna trespass unaenda Kwa jirani kusiko.kwako na kumfanyia vurugu kwake bila kuwa na legal document yeyote una mharass na kumuondolea peace of mind yake akiwa Yuko peacefully Yuko kwake

Angeitiws jambazi wakamuua usingeongea uongeayo haya Sasa ule uvamizi ni wa kijambazi sababu hauna legal document au legal backing hata moja

Kaibuka tu hakushirikisha serikali ya mtaa Wala mjumbe Wala RB ya polisi huyo ni jambazi mia Kwa mia aliyeenda kuvamia kanisa la watu .Sema walimhurumia walitakuwa kuitia jambazi jambazi kavamia kanisa umati uje umpe.kipigo Cha mbwa Koko Hadi akate roho sababu pale hakuna mahakama ya kuthibitisha yeye mumewe alienda na vyeti vya ndoa kuthibitisha yeye ndie mumewe? alimuonyesha nani? Kwa Nini asihukuliwe kama jambazi mteka nyara muumini au
Au kafika pale kisheria Kwa kufuata taratibu za kisheria Hiyo kesi kisheria sio nyepesi kama unavyofikiri
 
Polisi waliona hicho cheti Cha ndoa kama uthinitisho kuwa huyo ni Mkewe? Pili waliona vyeti vya kuzaliwa vya hao watatu ? Tatu waliona kitambulisho.cha taifa kuwa huyo mlalamikaji mwenye Hilo jina ndilo Hilo linasomeka cheti Cha ndoa na vyeti vya kuzaliwa vya watoto?

Huyo mchungaji ana akili ndio maana akakimbilia polisi kuwa kavamiwa na jambazi kanisani kwake sababu hakupewa document yeyote ya kisheria Hao Polisi nao wajinga kama hawakuzingatia yote hayo itakula kwao mahakamani
 
Aise hapo kuna tatizo kubwa sasa kusali gani huko hadi mtu anasahau familia, u need to have serious talk na wife wako na familia yake atleast aelewe majukumu yake, family ndio priority namba moja kwake na haruhusiwi hata kidini kutoka bila ya ruhusa yako, wewe ndio mume wake those are basic principles za ndoa
 
Hakuna kitu kama hicho yule ni mke wake halali kaenda kumchukua kaenda nae nyumbani fujo gani aliyofanya? Hata arnde mahakama gani hakuna hakimu anayeweza kuentertain kesi hiyo maana haina mashiko
 
Ila haya makanisa yanavunja ndoa familia nyingi zinateseka kwa kukosa akili za wanawake na wanawake watoto wanabaki wanahangaika sijui tufanyeje!!!
 
Hakuna kitu kama hicho yule ni mke wake halali kaenda kumchukua kaenda nae nyumbani fujo gani aliyofanya? Hata arnde mahakama gani hakuna hakimu anayeweza kuentertain kesi hiyo maana haina mashiko
Documents aliwakikisha Kwa kiongozi wa kanisa kabla ya kufanya mivurugu yake ili kwanza kanisa lijue yeye ndie mume wake halali wa ndoa na watoto ni watoto wake halali kisheria ? Alienda na vyeti vyao vya kuzaliwa?

Mchungaji ajiridhishe kuwa huyo ndie mwenyewe?
 
Hapo hakuna dispute kama yeye ndio mume halali maana hilo halina ubishi, ila hata kama wewe ni polisi unaweza kumfungulia kesi mtu aliyoenda kumchukua mkewe ambaye katekeleza watoto wadogo? Huyo mchungaji ndio hana busara alitakiwa aongee na huyo mke ili atekeleze majukumu yake ya kidini na kifamilia maana jukumu la kutunza familia ni wajibu kidini na kisheria
 
Ila wanawake sijui kama vichwani mwao Kuna ubongo!
 
Kanisa kama Lina usajil be very careful kesi mbaya sana itakayokuumiza ukajuta maisha Yako yote kitakachokukuta wakikuburuza mahakamani kuwafanyia fujo utakoma sababu mkeo hakupekeleka cheti Cha ndoa kama sharti la kujiunga na Hilo kanisa liwe la kweli au la kitapeli.Jiandae kuumia

Ukibanwa mahakamani waweza umia Bure Kwa mihemuko ya kidini ya kidini chako na hatakuja paroko Wala askofu Wala papa Wala katekista au mchungaji au au sista au shehe atakuja mahakamani kama shahidi itakula kwako hawaji uwe.makini mihemuko.ya kidini Yako iliyopitiliza kuliko mapadre,mashehe,wachungaji nk wa dini Yako utaumia Hadi basi ukome.Maumivu huwezi gawana na papa,askofu, mchungaji shehe au mchungaji

Tuliza kichwa wewe
Makanisa ya halali na ya kitapeli Sasa hivi viongozi wasomi sana Wana madgrii kibao huwababaishi chochote utaumia sheria zote wanajua Tena za mahakamani
Tofauti na zanani watakuummiza
 
Hakuna kanisa lolote wala msikiti litakaloweza kunizuia kumchukua mke wangu popote atakapokuwa nina mamlaka juu yake yanayotambuliwa kisheria , siyo kwamba ukisema umefanyiwa fujo basi mahakama itakuamini wewe kisa kanisa ni lako unapokaa na wakw zetu pia ujuwe tuna haki nao kushinda wewe na hilo kanisa lako uchwara acha uoga mahakama ipo kwa ajili ya haki sio vitisho na uzushi
 
Wewe ndio hujamuelewa ,watoto hawatumii maziwa yakopo ,ila alilazimika kuwanunulia maziwa maana walikua na njaaa
 
Mtu akisoma comments zako haimchukui muda kujua kwamba na wewe huna akili kama huyo mwanamke au huyo mwanamke ni wewe, na nahisi wewe ni mama mwenye upeo mdogo. Kama ni mwanaume na umeoa basi lazima unatombewa mkeo. Thread nzima ni wewe tu unayetetea mchungaji njaa aliyemteka mke wa mtu kiakili, una akili kweli!?,.. mke wako akiacha mapacha wa miezi minne hawajanyonya halafu yupo bize na kuombea watu utaendelea kumchekea!??... Schwein kabisa wewe..
 
Wewe ndio hujamuelewa ,watoto hawatumii maziwa yakopo ,ila alilazimika kuwanunulia maziwa maana walikua na njaaa
Huyo hana akili mnajibizana nae bure, thread nzima anamtetea mchungaji njaa..
 
Mnaochumbia chukueni notes, msije kutengeneza ajali huko mbele.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…