Mfanyakazi mwenzangu naishi nae kwenye nyumba ya shirika, mkewe amevuka mipaka hadi ya kupeleka kodi ya meza kanisani.
Huyu mwanamke kwao ni waislamu typically, ila kaanza kwenda kwa wahubiri na kaiva hasa na sanaa zao.
Jamaa yangu anasali RC. Kila siku mwanamke anakuja na wito kuwa anaitwa na Mchungaji kuwa ameona kuna watu wanachezea ndoa yao (wanarogwa). Yaani mwamba anapigwa hela hadi basi.
Mwanzoni nilijaribu kumpa ushauri, na kila nilichomwambia alikipeleka kwa mkewe. Nikaamua kukausha na sasa kila akitaka ushauri namkwepa.
Mbaya zaidi watoto wakiumwa ni mwendo wa kuwapaka na kuwaogesha maji yenye mafuta ya kanisani, hospital ni mpaka mtoto afikie hatua mbaya.
Kuna wakati jamaa alifiwa na mama yake na tulienda Moshi kwa ajili ya mazishi. Ilikaribia 40 ya kumaliza msiba, jamaa hakuwa vizuri mfukoni na aliona auze asset yake moja kwa 3,000,000/= ili akamalize msiba.
Akamshirikisha mwanamke na mwanamke akaenda kumshirikisha Mchungaji. Na baadaye majibu ya mwanamke yalikuwa kwamba wagawane 50% ya mauzo na mwanaume akatumie ile ya kwake kwenda kumalizia msiba ila ya mwanamke itabidi akatoe fungu la kumi kanisani. Imepita miezi minne sasa hawajaenda kumalizia msiba wa Mama wa mwanaume.
Kuna siku nilishangaa zaidi mwanamke alipomletea bahasha yenye fomu inayohitaji kujazwa taarifa za kazi ya mwanaume, ikiwamo mshahara. Nilimwambia mwamba huo ni mtego, ila baada ya siku mbili akaniambia kabanwa sana na mkewe na ikabidi ajaze ile fomu na kuirudisha kanisani.
USHAURI:
Wanaume tuwe makini sana na haya makanisa ya kiroho, mengi yamejaa wasanii.
Wanachofanya ni kuangalia weakness ya mwanamke ili waweze kucheza na akili yake na hatimaye kukuteka mwanaume na uchumi wa familia nzima.