Ushauri: Nimepewa RB kwa kosa la kufanya fujo kanisani

unafikiriaje aisee. Na kanisani kwenu mnafundishana mambo ya ajabu sana. Yeye hakwenda kumkamata muumini alienda kumchukua mkewe. Kwenye dini yako hamfundishwi mke amtii mumewe? Huyo mchungaji asiyejua Watoto wanatakiwa kunyonya ili waishi ana tofauti gani na yule muuaji wa Kenya?

Mimi baada ya tukio hilo ingekuwa ni marufuku watu wanaohusika na kanisa kukanyaga au kuhusiana na mimi.
 
Wanaokutana kanisani au msikitini wanaitwa waumini na wote eneo lile waliwepo.pale ni waumini chini ya uongozi wa kanisa au msikiti pale ni waumini wako kanisani au msikitini sio waume au wake za watu wako kanisani au msikitini

Yule alikuwa muumini akiwa kanisani.Mume ndiye kajichanganya aende polisi akakutane nao ndipo atajua usemi unasema tii Sheria bila shuruti Kila eneo au ukifanyacho kwanza angalia Sheria zinasemaje usikurupuke utaumia
 
Tafuta namna bora ya kuachana nae kama ameshalowea kwenye hayo makanisa Yao ya kina Baba mchungaji,,utanishukuru baadae,,Mwambie achague kulea familia au Kunena Kwa lugha??
 
Mfanyakazi mwenzangu naishi nae kwenye nyumba ya shirika, mkewe amevuka mipaka hadi ya kupeleka kodi ya meza kanisani.

Huyu mwanamke kwao ni waislamu typically, ila kaanza kwenda kwa wahubiri na kaiva hasa na sanaa zao.
Jamaa yangu anasali RC. Kila siku mwanamke anakuja na wito kuwa anaitwa na Mchungaji kuwa ameona kuna watu wanachezea ndoa yao (wanarogwa). Yaani mwamba anapigwa hela hadi basi.
Mwanzoni nilijaribu kumpa ushauri, na kila nilichomwambia alikipeleka kwa mkewe. Nikaamua kukausha na sasa kila akitaka ushauri namkwepa.

Mbaya zaidi watoto wakiumwa ni mwendo wa kuwapaka na kuwaogesha maji yenye mafuta ya kanisani, hospital ni mpaka mtoto afikie hatua mbaya.

Kuna wakati jamaa alifiwa na mama yake na tulienda Moshi kwa ajili ya mazishi. Ilikaribia 40 ya kumaliza msiba, jamaa hakuwa vizuri mfukoni na aliona auze asset yake moja kwa 3,000,000/= ili akamalize msiba.

Akamshirikisha mwanamke na mwanamke akaenda kumshirikisha Mchungaji. Na baadaye majibu ya mwanamke yalikuwa kwamba wagawane 50% ya mauzo na mwanaume akatumie ile ya kwake kwenda kumalizia msiba ila ya mwanamke itabidi akatoe fungu la kumi kanisani. Imepita miezi minne sasa hawajaenda kumalizia msiba wa Mama wa mwanaume.

Kuna siku nilishangaa zaidi mwanamke alipomletea bahasha yenye fomu inayohitaji kujazwa taarifa za kazi ya mwanaume, ikiwamo mshahara. Nilimwambia mwamba huo ni mtego, ila baada ya siku mbili akaniambia kabanwa sana na mkewe na ikabidi ajaze ile fomu na kuirudisha kanisani.

USHAURI:
Wanaume tuwe makini sana na haya makanisa ya kiroho, mengi yamejaa wasanii.
Wanachofanya ni kuangalia weakness ya mwanamke ili waweze kucheza na akili yake na hatimaye kukuteka mwanaume na uchumi wa familia nzima.
 
Kareport kituoni pia kafanye DNA usije ukawa unawahangaikia watoto ambao sio wako hadi wife ananishangaa hili jamaa vipi watoto sio wake Ila linajifanya km baba watoto wakati Baba watoto nipo nae kanisani huku tunaendelea kupeana upako
 
hawa matapeli wa kiroho tusipokuwa makini nao watatuharibia ndoa na familia zetu, nilishamwambia wife siku akikanyaga huko na talaka itamfuata huko huko
 
Kitendo cha mkeo kukushitaki ni kakudharau sana. Kwa hiyo anataka ufungwe au upigwe faini? Fikiria mara mbili huna ndoa hapo mkeo ni lipumbavu la kugawa bure

Sent from my SM-A217F using JamiiForums mobile app
 
Karipoti kituoni ukiwa na wanao hao. Hadhani maafande watakuelewa tu, nao ni wazazi kama wewe
 
Hatari iliyo kuu ni pale mke wako anapoiva kwa sanaa za Mchungaji, basi fahamu 90% ya taarifa zako zipo kanisani hata kama hausali katika kanisa hilo.

Mnajuwa ni kwanini asilimia kubwa ya waumini wa makanisa haya ni wanawake?

IPO HIVI: Kwa maeneo mijini kama Mbeya, Dodoma, Mwanza na mengineyo, Mchungaji huanzisha kanisa akiwa na wanawake wachache na huwapa uongozi wale anaowaona wawamfaa baadaye.

Baada ya muda anawashawishi hawa viongozi kuhakikisha wanawaleta wamama wengine ili kanisa liongeze maokoto. Na hapa wale viongozi wanaahidiwa commission kwa kila kichwa kipya kitakachokuja kanisani.

Hapa ndipo wamama wanaingia field kushawishi kila wanayehisi ni potential kwao. Huwa wana mbinu nyingi sana ila ya kwanza ni kuanzisha urafiki wa karibu na mkeo na mwishowe kumualika Jumapili moja akasali kanisani kwao. Na hapo ndio unakuwa mwanzo wa yeye kuwa mfia kanisa na akasahau majukumu yake.

Haya makanisa huwa hawaangalii dini wala dhehebu lako, ndio maana wana kauli yao 'TUNAWAKARIBISHA WATU WA DINI ZOTE, MADHEHEBU YOTE, IMANI ZOTE, MAKABILA YOTE, MATAIFA YOTE.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…