USHAURI: Nini cha kufanya kama mwenza wako alikuficha kuwa ana mtoto, Ukaja kujua baada ya miaka zaidi ya 10 baadaye?

Mara mia mwanamke useme mwanzoni kuwa wewe ni single mother tuchague kukuoa au kukuchezea kuliko ufiche alafu tuje tujue mbele ya safari . Hakika hausameheki
 
Nikiona nyuzi kama hizi huwa nalia sana.Anyway kila jambo anapanga Mungu.
 
Namuelewa Mleta mada,

Itakuwa anajiuliza kama ni hivyo huyo mwanamke atakuwa amemdanganya mambo mangapi nyeti tangu wajuane
na kuanza kuishi pamoja hadi leo?

Hawezi kumuamini tena!
 
Mbona humu wanafundishaga jinsi ya kuktambua mwanamke alokwisha kuzaa?

Hukujua @ Mleta mada?
 
Watu hawajuagi tu.

It takes years to be build a trust, but it takes a minute to destroy it.

Asomaye Na afahamu.
 
Halafu wanawake hawajuagi tu,

Wapo wanaume wengi tu huwa wako tayari kukuoa hata kama umekwisha zaa ilimradi amekuridhia.

Kwanini umfanyie hila kubwa hivyo?
 
Alichopitia huyo mwanaume si bure avunje ndoa
 
Thread 'Agundua mumewe ana mtoto wa nje baada ya ndoa'
Agundua mumewe ana mtoto wa nje baada ya ndoa

Nimeikuta hii
Thread nimegundua binadamu haswa mwanaume ni kiumbe MNAFIKI SANA.
Comments zinanichekesha sana

Eti leo mwanaume alificha mtoto alafu mke hataki kuelewa wanasema ana roho mbaya ila huku wanasema mme amwache mke kwasababu alificha mtoto. Stupid kabisa
 
Umesema sahihi Mkuu, ndiyo maana inashauriwa usifanye maamuzi ukiwa katika hali ya Furaha sana ama Hasira kali.

Huwezi kuja kuvunja ndoa wakati mna watoto wa miaka 20 plus, wameshindwa hata kukaa chini na kuyajenga.
 
Umeishi na mtu kwa miaka 15, mmezaa watoto 4, unakuja kumuacha kisa hakukwambia kua aliwahi kuzaa kabla!!?

Ukisikia kutafutiana sababu ndio huko sasa.

Nitakuwa na uhakika upi kuwa hata hawa wanne nao ni wa kwangu pia??

Hiyo ndiyo tunaita kama unaweza mtie kamba mumeo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…