USHAURI: Nini cha kufanya kama mwenza wako alikuficha kuwa ana mtoto, Ukaja kujua baada ya miaka zaidi ya 10 baadaye?



Hiyo sio sawa. Wanaume tuna wivu sana. Hayo mambo mengine ya awali usitake kabisa kuyafukua.

Inamaana alitarajia mdada wa watu awe alikua anamsubiria yeye tu?

Kama wote wamekutana used hakuna wa kumlaumu mwenzake, haijalishi anawabeba kwenye kirikuu, IST, baiskeli au mwendo Kasi.
 
Upo sahihi kabisa, kama umempenda yanini kudeal na past ya mtu.

Ndiyo maana hata project huwa zina starting date, kwahiyo reference yangu hupenda ianzie pale tunapoanza naye mahusiano na sio kuhusu mambo yangu ya zamani.

Wazee hawakuwa wajinga kusema "Mavi ya kale hayanuki"
 
Mbaya sana, huenda angependwa hata akiwa na mtoto
 
Niliipaste huko juu wameiruka kama hawaioni,
Mimi hua nawashangaa sana Wanawake wanaowatetea Wanaume wa Kiafrika, wachache sana wanajielewa wengi wao ni wabinafsi na wenye roho mbaya sana,

Mijinga mijinga tu dawa yao ni kuwapiga spana kali hadi yapanic na kuweweseka.
 
Ndiyo ungesikia wanawake wana roho mbaya, nasema naye amwachie watoto wake wote .
Umeshauri kitu kizuri, huyo Mama angeondoka kama alivyokuja watoto akamuachia hapo yeye akaanze upya, maana mtaani tena atapokea masimango ya kuitwa singo maza.
 
Watu ni wanafiki sana, unakuta mwanaume anasema siwezi oa mwanamke mwenye mtoto halafu yeye akiwa kwenye ndoa anazaa mtoto nje ya ndoa, na anataka mke ampokee! Mie hapana bora nionekane kiatu hilo bao lao wakalitunzie huko huko!
 
Kuna watu hawawezi kuupokea uongo, yupo tyr apewe ukweli wa namna yoyote ile.....ww unahakika kama hawakuulizana hayo mambo, na vp kama alisema hajawahi kuzaa? Hii nakumaind ww na ukoo wako af mazoea yanakufa
Kuna link kaleta humu.
Kuhusu dada mmoja mume wake alimdanganya kuhusu hana mtoto.
Kaja kumwambia baada ya miaka 2 ya ndoa.
Afu mtoto wa kike yupo form 3 anataka alete amlee sasa mkewe ukute hata miaka 30 hajafika.

Ukiangalia comment za kiume wanalamanani mke..
 
Haha.. yan kwakua mtu mmoja kakubaliana na jambo kwa situation husika basi mnapenda wote tuwe hivyo kwa situation tofauti.

Wanawake🤣🤣
Hata humu jf Kuna uzi za mke kudanganywa na mume kipindi cha uchumba.
Anakuja kuambiwa wapo ndoani afu analazimishwa amchukue mtoto
 
Mkuu mimi nimewahi kukuta case hii.

Dada mmoja alilalamika sana , kipindi wapo wachumba alimuuliza mchuma una mtoto akamwambia hana. Tena alimuuliza marakwa mara unamtoto akamwambia hana.

Sasa baada ya ndoa wakakaa miaka 10.
Akajakujua mume wake anamtoto anaumri wa miaka 15 kupitia maongezi ya simu wanapanga na familia yake jinsi ya kumleta mtoto home pale. Mtoto anaumri wa miaka 15.

Sasa kwa situation kama hii dada huyu akikataa utamuita anaroho mbaya??
 
Mkuu vitu hivyo vipo hata wanaume zipo nyuzi humu mwanaume kaficha mtoto miaka 20. Kuna mtu alileta uzi humu.
 
Hayanaga akili kabisa nashangaa wanavyo dharau wanawake wakati yenyewe yapo kama mazombi
 
Huo uzi
 
Daah! Sema uyo mr kazingua japo alidanganywa angefaa akubaliane na hali,Sasa mama huyo na watoto wa4 na ukubwa uo ataenda wap tena? Jamaa angefaa apo afanye busara akubali kasha pigwa .maisha yaendelee
 
Kuna Mwanaume mmoja naye alimficha Mke wake hivi hivi, mwisho wa siku yule Mwanamke akagundua alilia sana sana Mume na wakwe wakaomba msamaha yakaisha mpaka sasa hivi wako kwenye Ndoa yao wanaishi vizuri.
Wanakuwa wanafanya makusudi.
Utakuta wakwe walishirikiana kumficha.
 
Umeshauri kitu kizuri, huyo Mama angeondoka kama alivyokuja watoto akamuachia hapo yeye akaanze upya, maana mtaani tena atapokea masimango ya kuitwa singo maza.
Ndiyo hivyo yeye anaondoka na kilicho chake watoto anamwachia hapo, ili atafute mwanamke mkamilifu.
 
Sasa hiki kitu nasikia pia imetokea pia aa kwa tajiri mmoja wa kule kwetu
Jamaa ni tajrii kweli ila inasemekana mam yule Ana mtoto alimficha
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…