USHAURI: Nini cha kufanya kama mwenza wako alikuficha kuwa ana mtoto, Ukaja kujua baada ya miaka zaidi ya 10 baadaye?

Ila wanaume huwa mnanishangaza jambo moja. Nyinyi mnazaa na michepuko yenu ilhali mpo kwenye ndoa, wake zenu wanakuja kujua mkishakufa. Mbona hawa vimbi mashavu kama mnavyovimba nyinyi??? Wengine mnawaletea kabisa nyumbani, na wanawapokea maisha yanaenda. Sasa huyu wa zamani kabla ya ndoa mnaumia nini. Wanafki nyinyi muwe mnatunza energy mnayoyafanya yakirudi kwenu mvumilie
 
Hapo shida sio mtoto
Ametumia sababu hiyo kama kisingizio, inaonekana kuna mengi yanaendelea kati yao, kuchokana nakadhalika. Pia kuna kumbukumbu mbaya kwa mwanaume kuhusu mke wake, labda alikuta bikira ya bandia n.k. In short hapo mwanaume kapata kupumua kiurahisi, watu watahangaika na ishu ya mtoto yeye anawaza kusogeza kimada wake wa siku nyingiiii
 
Na kama mtu hayupo tayari kuzungumza ya nyuma kwanini alazimishwe??? Kila binaadam ana siri yake na maamuzi yake yanapaswa kuheshimiwa, huwezi jua hilo tukio lilimuumiza vipi akaamua kulifukia na kuanza upya.
Tusihalalishe upumbavu kwa kigezo cha maamuzi binafsi.

Kutotaka kuongelea umelala na wanaume wangapi hiyo ni hiari yako ila sio kuwa na mtoto na kuficha.

Unapoingia katika ndoa kuna baadhi ya haki unazipoteza na moja wapo ni uwazi wa uzao wako kabla ya ndoa.

Mtoto sio kijipu kusema utakificha mwisho kipotee.

Kuna watu wanawake kwa wanaume hawapo tayari kuingia kwenye mahusiano na mtu mwenye mtoto/watoto kabla. Sasa hapo haki iko wapi kwa mwanaume endapo ilikuwa hana azma ya kuoa mwanamke mwenye mtoto na mwanaume mwingine.

Haijalishi unaitazama kwa jicho gani, kuficha kuwa una mtoto kabla ya ndoa ni jinai kubwa katika mahusiano na mwanaume kuamua kutoa talaka ni ndani ya haki yake kwa jinsi alivyolichukulia.
 
Nakupongeza kwa moyo ulionao mkuu, wewe ni zaidi ya malaika aiseee....😊
Lakini ngoja nikugusie kidogo kuhusu sisi wanaume..... kwanza sisi ni wabinafsi kiasili, pia tunatabia ya kunyamaza lakini niwagumu sana kusamehe. Tofauti na ninyi hua mnaongea sana na kutoa maneno, lakini kesi zenu hua zinaisha na mnasamehe. Na hapa ndipo nimalizie tu kwakusema kwamba wewe ndie usirahisishe mambo kwasababu ungekua mwanaume pengine unge elewa hiki ninacho kizungumza na kilicho mkuta huyu mbwana kwenye hii mada.
 
Wakati mwingine tusiongozwe na hisia bali utashi wetu.

Kwani ni kosa mtu kuzaa, ni heri huyo amezaa maana kuna wengine wametoa zaidi ya mimba 7 hadi kuolewa kwao.

Ningekuwa Mimi huyo mtoto ningempokea na kumfanya mmoja ya watoto wangu, kwanza kwa mujibu wa mila zetu mtoto wa mkeo nao ni watoto wako
 
Alafu kuna kisa kimoja kimemtokea mwenzetu wa ofisini kimenishangaza kwa alivyo react ila nikasema acha nije nishirikishe na wanajamvi huku.

Huyu dada kakaa kwenye ndoa kama miaka mitatu hivi. Sasa anakuja kugundua mume wake aliwahi kuchepuka na ex wake tena sio mara moja kipindi wapo kwenye mahusiano. Yaani kabla ya ndoa. Yani wame date miaka saba, mwaka wa nne mwanaume akawa na mahusiano na ex wake wameenda kama miaka miwili na ex malavidavi kama yote ila huyu dada anasema hakuwahi kuhisi. Sasa mke mtu kaja kujua wakati wameshaoana. Anasema ye bado kinamuuma kwasababu alimuamini sana mme wake inakuwaje alimsaliti kipindi ambacho alimpenda na kumuamini.

Wengi tukamshauri aache yaliyopita wagange yajayo. Akauliza ingekua nyinyi mngesahau na kusamehe? Nikasema wanajamvi mpo kibao mna majibu em mshaurini na nyinyi.
 
Usichokijua: saikolojia ya mwanaume ni tofauti kabisa na ya mwanamke.
 
Tatizo siyo kuzaa, ila uongo.
 

Mimi nawekaje hasira na mihemko kwenye uzi usionihusu? Hapa tumeitwa tutoe ushauri nakushangaa unapanic kwenye comment yangu,

Unavyosema tusijadili kimazoea ya Kiswahili kwa hiyo tujadili kigeni kwa Kizungu au Kichina? Maana hao hili tukio wakipelekewa ndio kabisaa watazidi kumshangaa huyo Mwanaume,

Umesema mwanzo wa mahusiano mnaulizana moja, mbili, tatu, umejuaje kama hii couple tunayoijadili hapa waliulizana yote hayo!!??

Pia elewa maana ya privacy, kama hajataka jambo lake liwe wazi sio vema kumlazimisha, yule ni mwanae yeye ndie alikua anajua zaidi.
 
Hisia za kiume na kike ni tofauti kabisa.

Mwanaume ana uwezo wa kulala na wanawake hata 100 lakini upendo wake wa dhati ukawa ni kwa mkewe tu. Ila mwanamke anapomvulia chupi mwanaume basi na hisia zinajengeka hapo hapo.

Men think with their dicks while they love with their hearts.
Women think with their hearts and love with their vaginas.
 
Shangaa na wewe, mijanaume ya Kiafrika hua ni mibinafsi sanaaa, hii habari ingekua ni mwanaume ndie kaleta mtoto na Mwanamke ndie kataka talaka ungeona vile wanamshambulia Mwanamke na kumuita majina yote ya ajabu,

Mambo ya mtu na mtoto wake wao wanaguswa na nini eti kwanini kanificha kwani aliwahi kuulizwa?
 
Wamechokana tu hao hamna lolote, jamaa alikua amechoka akapata pa kutokea! Yaani 4-1 si ni fare kabisa!
 
Huyo ni Mwanaume suruali, halijui jando, hajafundishwa chochote kuhusu ndoa walizoana zoana tu wakaapa basi,

Hakuna jambo kubwa la kuachana hapo unless alikua amemchoka ndio kapata sababu.
 
Kwenye ubinafsi ndio point kubwa, naweka sawa WANAUME WA KIAFRIKA NI WABINAFSI WENYE ROHO MBAYA,

Hapa sasa tutakua tumeelewana na mjadala uishie hapa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…