Ushauri, niwahusishe watoto wangu wa nje ya ndoa kwenye urithi?

Alitakiwa kuwatengenezea urithi wao watoto wake huko huko kwa mchepuko wake mapema habari za kuanza kuomba ushauri sahivi baada ya maji kufika shingoni sio mazuri katafuta Mali na mke wake wa ndoa Mali zibaki kwa watoto hao wa ndoa ,awarithishe watoto wake wa nje Mali walizochuma na mchepuko wake .
 
Unajua gharama za kubadili hati wewe? TRA wanachukua 10% ya gharama ya nyumba na uwanja! Bado kuna Valuer etc
 
Huyo jamaaa kama bado anazo cent ni vyema akawajengea huko nje AO Watoto wengine / au ata akauza magari Kimyah Kimyah atoe urithi wawatoto wa nje kinyume na hapo maumivu,
 
Mke hakutaka kuwa mnyonge akalipa kisasi🤣
 
Wengi huwa wanawarithisha watoto wao wa nje kimya kimya,jamaa awape mali zao sasa hivi bila familia ya ndoa kujua ili kupunguza utata na uadui...ila anaweza kuwatambulisha wajuane.
 
Hii hapana aisee, kama jamaa alikubali hili basi ni bwege.
 
Michepuko na watoto wao huleta umasikini, vifo vya haraka na madhira mengi katika ndoa.

HOSEA 1: 2-9

Kama umezaa nje ya ndoa tubu hiyo dhambi.
Watoto ni wa Mungu atajua hatma yao.


Rudi Tulia kwenye ndoa maisha yaendelee.

Mwisho andika Mirathi isiyowatambua hao watoto wa siri wala mama zao.

Ikikupendeza ikiwa unajiweza wape kidogo Chao (vijizawadi mbuzi) mapema kabisa msifahamiane.

Ingawa hiyo haina umuhimu wowote hata kidogo, na sishauri kuifanya.

NB. NAKUPIA WEWE MWANAUME MZINZI KAMWE HUTOKAA UNUFAIKE NA CHOCHOTE KWA HAO WATOTO WAKO WA UZINZI.

ENDELEA KUTII MATAMANIO YAKO YA MWILI, HATMA UTAIONA .
 
Katika vitu naviogopa kwenye ndoa yangu ni siku mume aniambie amechepuka hadi kupata mtoto huko nje, sijui tu ntalipokeaje. Kuniletea ushahidi kwamba alichepuka ni jambo gumu jamani. Nahisi ntaomba likizo kidogo nikapumzika mahali kwa muda usiojulikana.

Sent from my CPH2185 using JamiiForums mobile app
 
Njia nyingine ya ku deal na hii ishu ni kuwajengea maisha hao watoto wa nje huko huko waliko wao na mama zao. Mfano unaweza kumfungulia mama yao biashara na ukawajengea mji wao, ili wajitegemee huko wasije kudai urithi uliochuma na mke wa ndoa.

yes hii nakubali
 

oooh halleluya praise the Lord[emoji3059]
 
Wanawake mna story za uongo na kijinga sana mkiamua kujitutumua,kutiana moyo na kushauriana ujinga.
 
Kuna vitu unachanganya, na inabidi uwe makini navyo.

Ndoa ni mahusiano yako wewe na Mwanamke mliochaguana kua wenzake katika maisha, Kwa shida na raha kama ni kweli.
V/s
Watoto wako ni generation yako inayoendelea kutoka vizazi vyako vilivyopita kama babu yako, akamzaa baba yako, ukazaliwa wewe, kisha wanao, kisha wajukuu zako,etc.

Mke wako kama sehemu ya familia yako anastahili kupata chochote kutoka kwako. Vivyo hivyo watoto wako nao wanastahili kupata pia kutoka kwako.

Kwamba hawa ni Watoto wa mama yupi kati ya wa ndoa ama mchepuko hayo tunayaleta sisi binadamu kuwekeana kauzibe na kubaguana. Mtoto yoyote aliethibitika kua ni wa kwako basi ana haki juu ya mali zako, regardless status ya mama yake kwako.

Labda tofauti iwe kua wewe mali zako kuna zenye mmechangia na mkeo wa Sasa hapo ndio itabid mtenganishe au mgawanyishe ili zibakie zako kama zako
 
Sasa kesi yako na huyu ni tofauti.
Huyu alizaa nje akiwa yupo kwenye ndoa kabisa kaka. Watoto au mtoto uliempata kabla ya ndoa kuwatambulisha sio ngumu kaka.
Acha ujinga hata iweje kosa lako mtoto hana hatia. Ni jukumu lako haki zake zote. Unaweza mdharau mwanao, kesho munaachana na huyyo mwanamke. Mtoto wako ni ndugu yake sio mkeo.

Sent from my TECNO BA2 using JamiiForums mobile app
 
Kuna cha kujifunza hapa,
Mzee aliwachanganya Bado mkiwa wadogo na pia aliwagengeneza kwa kuheshimiana wote mnasikizana
 
Ww ni demu
Ni kweli na pia inabidi ajiongeze sisi wanaume tunajielewa. Nikiona siwezi kutulia nachukua Golikipa maana najua hata nikimletea watoto hawezi kusumbua. Sasa unakuta mwanamke analalamika wakati hana kitu cha maana. Unakuta hata biashara aliyonayo kafunguliwa na mumewe. Halafu anataka kumuacha mume wake kisa mtoto wa nje. Jamani kuweni serious kama mwanamke unaweza ukajitegemea sawa. Na kujitegemea hiyo wengi wenu mnaishia kudanga hata kama mna elimu. Maana hata yule aliyeimba wanawake na maendeleo mmesikia kesi yake. Mwisho wa siku inabidi mkubali ukweli.
 
Wanaume sisi sijui tupoje yani kitu akifanya mwanamke ni kosa ila akifanya mwanaume ni sawa
Kwa sababu mwanaume ndiye anahudumia familia. Ndiye anaesomesha watoto. Na kuprovide ila wavulana na wanawake wanalingana. Kama mumeo ni mvulana hili ni kosa kubwa sana. Ila kama ni mwanaume sio kosa ni bahati mbaya.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…