Ushauri, niwahusishe watoto wangu wa nje ya ndoa kwenye urithi?

Ushauri, niwahusishe watoto wangu wa nje ya ndoa kwenye urithi?

Kabisa kuna watu wanandoa wanaishi kwa amani kuwezi amini. Kuna familia moja naifahamu jaman wameishi zaidi ya miaka 30 hawajawahi kugombana wala kupeleka mashtaka kwenye familia wala marafiki.

Hadi leo hii kama chakula kipo tayari mmoja hali hadi mwenzake arudi. Labda kama anaratiba imembanana majukumu tena wanapeana taarifa. Acheni tu

Sent using Jamii Forums mobile app
Yah bro
 
Hii kauli wanaume wasipo izingatia basi tu.

Mimi imenitokea kabla ya ndoa nilizaa na mdada mmoja, alipojifungua tu tilipishana tukaachana. Haikuchukua muda nikaoa, na wakati naoa huyo bidada wa ndoa nilikuwa nishampiga mimba kiasi cha mtoto wa kwanza na huyu wa ndoa wanapishana miezi nane tu.

Nilichokifanya ni kumjulisha wife niko na mtoto nilizaa tena nikamtisha kwamba wako wawili sehemu tofauti ili baadae akiona mmoja aone nafuu. Mtoto yule wa nje alipotimiza miaka nne nikampanga mama yake kwamba mtoto inabidi aje home ili atengeneze mahusiano na wenzake tangu akiwa mdogo ili asionekane baadae kafuata urithi tu. Haikuwa rahisi kwa mama wote wawili lakini kama mwanaume nilishupaza shingo. Hata mama wa ndoa aliponipa majaribu nilimwambia kama haoni thamani ya mwanangu kuwa pale niko tayari kuvunjika ndoa ili nilee mwanangu. Baada ya msimamo mtoto yupo home tangu akiwa na miaka 4, now standard three, 8 yrs anaishi bila kelele.

Namalizia kwamba UDUGU NI UTOTONI. Hapo ndipo chimbuko la hisia.

Sent from my TECNO BA2 using JamiiForums mobile app
Sasa kesi yako na huyu ni tofauti.
Huyu alizaa nje akiwa yupo kwenye ndoa kabisa kaka. Watoto au mtoto uliempata kabla ya ndoa kuwatambulisha sio ngumu kaka.
 
Kama kweli jamaa anawapenda wanae aliozaa nje ya ndoa kamwe asiwatelekeze kwenye mirathi Yake.
Ahakikishe kila mtoto anapata urithi wake ipasavyo
 
Wagawane na mkewe nusu Kwa nusu then mgao wake agawe Kwa watoto wote wa4.
 
Kama kweli jamaa anawapenda wanae aliozaa nje ya ndoa kamwe asiwatelekeze kwenye mirathi Yake.
Ahakikishe kila mtoto anapata urithi wake ipasavyo
Sawa ndio ila nyie ndo zenu nyie wanaume, mnapanga na wale zenu kuwa mali ni zenu na watoto wenu , baadae yanatokea hivyo inaumiza sana.
 
Wakina mama ukiona mume wako kaja tuu kukwambia anamtoto nje ya ndoa ,

Yani maana yake mahusiano yenu hayajajengwa kwa kuaminiana.

Yani mumeo anakuona kama kinyago tuu hapo home.

Na ni sawa tuu kwa upande mwanaume kwa mkewe.
SIO MTOTO TU,AKIKWAMBIA FLANI NITAMUOA NA USHAHIDI UNAO JUA KABISA WEWE MWANAMKE HUPENDWI NA UKO KAMA TAKATAKA HAPO,KIMBIA
 
Nimekuelewa ila nilichokujibu ni kuwa lazima confession iwepo kwa sababu bila kujali mali ni zake binafsi, lazima wosia umhusishe mke kama shahidi, sasa usipomwambia ukweli mkeo atakubali vipi kushuhudia wosia wako!!
Lengo ni kutoa attention ya kuwa kuna watoto nje... Whether wosia ni valid au sio valid... Watarithi tuu kwa sheria ilivyo sasa
 
Habari,

Kuna rafiki yangu mmoja nilizoeana nae mda kidogo na tunafamianane kutoka na biashara zetu yeye anaumri wa 43 now. Ila kwa sasa anahali mbaya ya kiafya anaumwa magojwa yasiotibika haya kupona haiwezakani kabisa.

Sasa miaka kadhaa ya nyuma alipata mchepuko, katika kukutana na mchepuka akampatia ujauzito akafanikiwa kupata mtoto wa kiume, kafananae sana maana nimemwona kwenye picha. Baada ya miaka miwili akachepuka tena na huyo huyo mchepuko wake akampa tena ujauzito alimlumu, ila mchepuko alimwambia kuwa mimi nakupenda.

Akaamua kuvunja mahusiano na mchepuko. Ila baadae akaona ngoja tuu awatambulishe watoto kwa kaka zake na dada yake. Alifanikiwa kuwatambulisha ila kwa mkewe hakufanya hivyo. Kutokana na kuaminiana na mke wake.

Sasa ni mogonjwa yeye na mkewe wamejenga nyumba tatu na biashara zao na vitu vingine kama magari. Yeye na mkewe wamezaa watoto 2 tuu.

Shida inakuja hizo mali zote limeandikwa jina lake ila ameshirikiana na mkewe wa ndoa kabisa. Yeye kaniambia tangu aishi na mkewe hajawahi kugombana nae wala kumuona mkewe anashida yoyote. Amenikambia kuwa ni mke mzuri sana na mama bora, hana shida yoyote, hicho ndio kilipelekea hata kuwaambia kaka zake na dada yake wasimwambie mkewe. Hataki mkewe aumie.

Wadau ushauri, maana anaona akiacha tuu mali watagawana na kumuacha mkewe na maumivu makubwa sana. Yeye hilo hataki, sasa alikuwa ananiambia mimi kuwa abadilishe hati ya nyumba na mali zingine kwenda kwa majina ya watoto wa ndoa tuu. Mimi nilikuwa sina cha kumjibu nilibaki namwangalia tuu.

Nikaona isiwe shida ngoja nije hapa JF. Maoni yenu wadau anataka afanye sasa.
awape watoto wake wa ndoa maana hata akiwapa na hao watoto wa nje umoja wa familia hautakuwepo tena. kuzaa nje ya ndoa ni kuisambaratisha familia. mimi naenda zangu
 
Lengo ni kutoa attention ya kuwa kuna watoto nje... Whether wosia ni valid au sio valid... Watarithi tuu kwa sheria ilivyo sasa
Hapana mkuu, as long as jamaa anataka kuandika wosia ni lazima aconfess kww mkewe. Halafu hii ya kusema watarithi kwa sheria ya sasa sio rahisi kihivyo. Watoto kama hawajatambuliwa kwa ukoo (pamoja na mke) hao hawawezi kurithi chochote, mahakama ya Rufani ilishaamua na ikasema kuwa watoto haramu watafurahia maisha na mali za baba yao wakati wa uhai wa baba yao, siku baba akifa, ndio mwisho wa mchezo.
 
Nipe hiyo case ya wazee... Mkuu
 
Nipe hiyo case ya wazee... Mkuu
VIOLET ISHENGOMA KAHANGWA AND JOVIN MUTABUZI vs THE ADMINISTRATOR GENERAL AND MRS. EUDOKIA KAHANGWA [1990] TLR 72(CA)
Walifanya reference kwa kesi ya Kiingereza ya In re Harrington [1908] Ch. 678 where it was held that,

A putative father's obligation under a bastardy or affiliation order ends with his death, that such obligation is personal and the arrears under such an order are not recoverable against his estate.
 
Aache u selfish,,,Kama ana uhakika ni damu yake Wana Haki ya kupata urithi watoto.
Na hii tabia t.ya kuithamini Mali Kama tumehamia duniani sijui hata imekaaje yaani.
 
VIOLET ISHENGOMA KAHANGWA AND JOVIN MUTABUZI vs THE ADMINISTRATOR GENERAL AND MRS. EUDOKIA KAHANGWA [1990] TLR 72(CA)
Walifanya reference kwa kesi ya Kiingereza ya In re Harrington [1908] Ch. 678 where it was held that,

A putative father's obligation under a bastardy or affiliation order ends with his death, that such obligation is personal and the arrears under such an order are not recoverable against his estate.
Mbona kama hii precedent imekuwa overruled na hizi case za Elizabeth mohamed case na Judith Patrick kyamba case
 
Back
Top Bottom