Ushauri, niwahusishe watoto wangu wa nje ya ndoa kwenye urithi?

Ushauri, niwahusishe watoto wangu wa nje ya ndoa kwenye urithi?

Yaani nawashangaa wanawake wanaoolewa siku hizi, kwanini uolewe? Kwanini unakubali kwa akili zako timamu kumpa mtu mwingine Uhuru wa kukuumiza kihisia na kukosa furaha maisha yako yote? Yaani kwanini?? Huwa naelewa nikiona wale ambao maisha kidogo yamekua magumu naona labda anataka wa kumlisha na kumhudumia, Ila mtu una kazi una weza kujihudumia kila kitu kwanini unajiingiza kwenye jehanamu inayoitwa ndoa?? Ndoa ni tamu Sana kwa mwanaume Ila kwa wanawake hahah dah ni huzuni Ila oleweni wenyewe mnasema ndoa ni heshima, sijawahi kuelewa logic ya ndoa kabisa zaidi ya kujitafutia maumivu ya kihisia, stress, pressure in your 30s, na kufa mapema kwa magonjwa ya kuletewa.
Inawezekana ndoa si muhimu.

Lakini ulivyoandika unaacha swali lingine.

Kwani usipoolewa ndiyo huwezi kuumizwa?
 
Yaani nawashangaa wanawake wanaoolewa siku hizi, kwanini uolewe? Kwanini unakubali kwa akili zako timamu kumpa mtu mwingine Uhuru wa kukuumiza kihisia na kukosa furaha maisha yako yote? Yaani kwanini?? Huwa naelewa nikiona wale ambao maisha kidogo yamekua magumu naona labda anataka wa kumlisha na kumhudumia, Ila mtu una kazi una weza kujihudumia kila kitu kwanini unajiingiza kwenye jehanamu inayoitwa ndoa?? Ndoa ni tamu Sana kwa mwanaume Ila kwa wanawake hahah dah ni huzuni Ila oleweni wenyewe mnasema ndoa ni heshima, sijawahi kuelewa logic ya ndoa kabisa zaidi ya kujitafutia maumivu ya kihisia, stress, pressure in your 30s, na kufa mapema kwa magonjwa ya kuletewa.
Tatizo ww ushazoea uzinzi ndo mna huoni faida ya ndoa

Subiri ukikua utajua nini maana ya ndoa
 
Your friend is.....au basi.
Nyie wanaume nyie ni.....au basi tu.
Sasa kama mkewe ni mke bora na hakua na kasoro yeyote huko nje mnaenda kufanyaje nyie wapuuzi🤣🤣.
Angekua hataki mkewe aumie si angetulia nae?

Anyways.Yeye ni baba wa hao watoto wa mchepuko na hao watoto wana haki sawa sawa na hao wa ndoa.Awapatie watoto haki yao ya urithi asilete upuuz.
 
Amshirikishe mke wake aone atasemaje,ila nafikiria kuwa hao ni watoto wake
Yes this is it, Si kila mke ni mbaya, unaweza kuzuka ugomvi ila mwisho wa siku mke akakubali yaishe na akaboresha mahusiano between kids.

Binafsi kitawaka, ila sababu siwezi ku-undo hiko kitu nitawakubali tu watoto.

Kukiwasha maana yake si mbaya, rules are rules huwezi kuexpect umecheat kwenye ndoa halafu nikuchekee!
 
Mwenye mali ndiye anajua kwamba mali hii na hii iende kwa mtoto huyu na yule, aweke kwa mandishi kwa msaada wa mwanasheri, iwe ni sehemu ya usia wake.

Kwa sasa cha muhimu ni kuangalia kesho ya watoto wote, wa ndoa na hao walio nje ya ndoa.

Muhimu: Hili alifanye mapema na iwe siri yake na mwanasheria, na hao ndugu wanaofahamu hali halisi.
Kwa sheria zetu, ukiwa na ndoa, mke ni lazima ashuhudie wosia wa mwisho wa mumewe. Kwa hiyo kama ataandika wosia na kuwa siri yake na mwanasheria tayari utakuwa ni wosia batili, yaani utakuwa hauna maana. Ni sawa na kusema amekufa bila kuacha wosia.
 
Tatizo dogo hilo:-
  • Kwa sasa anatakiwa amilikishe mali zote kwa mkewe, kadi za gari zote zisome jina la mkewe pamoja na nyaraka za mali zingine.​
  • Baada ya kuhamisha umiliki wa mali zote kwa mkewe, ndipo amueleze ukweli mkewe.​
  • Kuhusu watoto wa nje; kama fungu lipo, awawezeshe mtaji na awaambie wazi hawatahusika kwenye mali zake alizochuma na mkewe.​
 
Njia nyingine ya ku deal na hii ishu ni kuwajengea maisha hao watoto wa nje huko huko waliko wao na mama zao. Mfano unaweza kumfungulia mama yao biashara na ukawajengea mji wao, ili wajitegemee huko wasije kudai urithi uliochuma na mke wa ndoa.
Naona sababu mwanaume anaumwa anahisi atakata moto soon. Atamuwezesha lini?
 
Mwenye mali ndiye anajua kwamba mali hii na hii iende kwa mtoto huyu na yule, aweke kwa mandishi kwa msaada wa mwanasheri, iwe ni sehemu ya usia wake.

Kwa sasa cha muhimu ni kuangalia kesho ya watoto wote, wa ndoa na hao walio nje ya ndoa.

Muhimu: Hili alifanye mapema na iwe siri yake na mwanasheria, na hao ndugu wanaofahamu hali halisi.
Mali mke anamkono wake mkubwa tuuu
 
Simple and clear ingawa sijasoma comments zote ni kuwa kisheria hao watoto wanaoitwa wa nje ya ndoa hawana Chao iwapo km baba yao hatawatambulisha kwa ndugu zake na kwa MKE halali alie naye kabla hajafa. Ila akifuata utaratibu huo tena ikibidi kuwatambulisha kwa kikao maalumu cha ukoo basi watapata haki ya baba yao. Kinyume na hapo, hakuna kitu.

Pia mambo haya yanategemeana na imani ya mtu. Likienda kiimani huwa na changamoto sn bora liende kiserikali (mahakama ndiyo iamue). Kwa Mfano, kwa Waislam watoto wa namna hii huitwa watoto haramu(wamezaliwa kinyume na sheria na taratibu za dini ya Kiislam aka wamepatikana kwa kuzini). Sasa kitu kikiwa tayari ni haramu hapo unatarajia nini.

ili kuondoa mshikeri, ni simple tu, baba anapaswa kuwagawia chochote hao watoto kabla hajafa. Hapo hata km MKE atajua na kutia ngumu inakuwa rahisi kutumia uanaume wake kuwapa vitu km pesa (mtaji-kwa kuwafungulia akaunti benki) au kuwamilikisha viwanja kwa majina Yao au hata kuwanunulia magari/nyumba km uwezo upo . Hapo hata baba yao akifa watakuwa wanachekelea tu.
 
Mi ni mhanga wa hilo.

Nilimchukua kijana wa nje wa mme wangu. Alipokuwa mkubwa alihakikisha ndoa imesambaratika.

Mme alipokufa ilikuwa shida, nilifukuzwa msibani yaani yule kijana alihakikisha naondoka pale, sikulala.

Ndugu wa mme wakawa upande wa mtoto wa nje.

Ninachoshukuru nilikuwa nimemwambia mme wangu asiandike wosia, alisikia, cheti cha ndoa kilinisaidia kupambana mahakamani.

Nyumba ikauzwa, na pia alikuwa na watoto wengine wengi nje.

Kila mmoja akapata kiasi.

Mtoto wa nje ni tatizo.

Nilihangaika.
Pole sana
 
Tatizo dogo hilo:-
  • Kwa sasa anatakiwa amilikishe mali zote kwa mkewe, kadi za gari zote zisome jina la mkewe pamoja na nyaraka za mali zingine.​
  • Baada ya kuhamisha umiliki wa mali zote kwa mkewe, ndipo amueleze ukweli mkewe.​
  • Kuhusu watoto wa nje; kama fungu lipo, awawezeshe mtaji na awaambie wazi hawatahusika kwenye mali zake alizochuma na mkewe.​
Yah kweli inaweza saidia
 
Ninao ndugu wa nje kutoka kwa mzee wetu. Mambo ya mali siangaliagi, mi nshasomeshwa kiroho safi nalala mbele. Mama angu mwenyewe anasemaga sina muda wa kugombea ardhi ntazikwa kwenye eneo dogo. Natafuta za kwangu niwaandikie wanangu. Mume wangu akiamua mengine apambane na hali yake. Sasa hivi nalenga unyakuo ukija niondoke na Yesu asiniache nyuma. Hizi mali siendi nazo kokote. Ee Bwana nisaidie.
 
Aandike wosia tuu ataje idadi ya watoto wake wote plus wa nje... Na pia mgawanyo wa mali zake binafsi sio walizochuma pamoja ..

Hakuna haja ya kuncofess.. wosia wa marehemu unaheshimika sana kisheria
Wosia bila kumshirikisha mke utaleta ugumu kuthibitisha kuwa hizo alizozitaja ni mali zake binafsi. Ndio sababu ya kutaka mke atie saini yake kwenye wosia (kama shahidi) ili kuepusha migogoro kama hiyo ya kujua kama mali ni za binafsi au za wanandoa wote. Bila kuconfess sasa mke atasaini vipi wosia wako? Wosia unakuwa batili
 
Yaani nawashangaa wanawake wanaoolewa siku hizi, kwanini uolewe? Kwanini unakubali kwa akili zako timamu kumpa mtu mwingine Uhuru wa kukuumiza kihisia na kukosa furaha maisha yako yote? Yaani kwanini?? Huwa naelewa nikiona wale ambao maisha kidogo yamekua magumu naona labda anataka wa kumlisha na kumhudumia, Ila mtu una kazi una weza kujihudumia kila kitu kwanini unajiingiza kwenye jehanamu inayoitwa ndoa?? Ndoa ni tamu Sana kwa mwanaume Ila kwa wanawake hahah dah ni huzuni Ila oleweni wenyewe mnasema ndoa ni heshima, sijawahi kuelewa logic ya ndoa kabisa zaidi ya kujitafutia maumivu ya kihisia, stress, pressure in your 30s, na kufa mapema kwa magonjwa ya kuletewa.
Omba Mungu atakupa wa kufanana nawe na kukufuta machozi.Pole pia kama ulishaumizwa huko nyuma kwenye mahusiano Yako.
 
Binafsi inategemea kama baba alimuoa mke wake akiwa tayari amejijenga kiuchumi mke kaendeleza ni busara akawapa watoto wa nje urithi. Lkn kama ndo walianza kutafuta mali na mke wake kuanzia 0 hapo pagumu.

Ndo maana huwa nasema kama mwanamke unakubali kuzaa na mume mwenye familia hakikisha unaweka msingi mzuri wa watoto wako unaozaa. Isifike hatua unaanza kulalamika wanawake wana roho mbaya. Fikiria mwanamke mwenzako alikua halali au wakati mwingine wanalala njaaa ili watatute mali.
Leo hii aambiwe nyumba fulani wanapewa watoto njee. Ni ngumu kubeba. Kwanza unakuwa na maumivu ya kusalitiwa pili unawaza juhudi zako ulizoweka kupambana leo hii unaenda kumpa mtoto aliyepatikana kwa usaliti.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Muhimu tujue kuwa binadam tumeumbwa tofauti sn. Kwa wanawake wengi watoto wa nje ya ndoa wa waume zao huwa ni Haram, na kwa wanaume ndiyo usiseme maana ikitokea mkeo akakwambia anamimba ya mtu flani ila ni shetani tu kampitia, hapo ndoa inavunjika pia.

Hivyo, hakuna kuchekana. Maisha ya ndoa muda mwingine huwa ni ya kuviziana ili mmoja afanye kosa ili iwe sababu ya kuachana au kukusema hovyo au kukutusi Kila siku. Ila ukweli ni kuwa ingawa wanawake wengi hawapendi watoto wa nje ya ndoa kutoka kwa waumie zao, hata wao wamekuwa na mimba nyingi tu nje ya ndoa zao ingawa wao wamekuwa wakizitoa hizo mimba zao pindi anapobaini kuwa kapewa mimba na mchepuko wake. Hili la kutoa hufanyika chapu na kwa usiri mkubwa kwa MUME ili kulinda ndoa yake. Tena mara nyingi hizo abortion hufanyikia mbali na Wilaya au mkoa wanaoishi. Wewe ukiona mke anakuwa na safari ya ghafla ya kuchukuwa siku 4/5 au wiki na anaporudi hataki tendo la ndoa kwa sababu za uchovu wa safari au eti yupo period na hali hiyo ikadumu kwa wiki ujue kuna kitu umechezewa. ☑️ Ingawa hili siyo formula kuwa muda wote huwa ni kweli. Ila kwa % kubwa ndivyo ilivyo.
 
Sante Sana! Sante Sana.

Kwa Sisi Watibeli. Ikiwa itatokea Mwanaume akapata Mtoto Kwa Mwanamke wa nje(mchepuko au Malaya au danga)
Hesabu inakaa kama ifuatavyo;

1. Mtoto wa nje hurithi vya nje, na mtoto wa ndani hurithi vya ndani.

2. Ni jukumu la Baba/mwanaume kumuandalia urithi mtoto wa nje bila kuhusisha Mali za Familia (familia kuu) kama ilivyo ikiwa mwanaume ataamua kuoa MKE mwingine basi Mali za ndoa hazitahusiana na ndoa ya MKE Mpya. Yaani atafute zingine.

3. Baba ni lazima atambulishe mtoto wa nje ili ajuane na Ndugu zake. Lakini hiyo haitamaanisha mtoto huyo anahusiana na Mali za familia ya ndoa,.
Itategemea na busara ya Mke au Watoto waliopo ndani ya familia na wala Isiwe Haki ya mtoto wa nje.

4. Mtoto wa nje hapewi urithi isipokuwa Zawadi. Ni jukumu la Wanawake kuhakikisha wanazaa ndani ya Ndoa bila kutoa kisingizio chochote kile. Ili kuwaepusha Watoto kuingia katika matata.

5. Mtoto wa nje atakuwa hana wajibu wa kumlea Baba yake labda iwe Kwa busara zake tuu.

6. Haki ya mtoto wa nje nu kupewa malezi na matunzo tuu mpaka atakapokuwa MTU mzima.

Hivyo ndivyo Watibeli tunavyoshughulikia mambo yetu.
 
Duu kuna kaka mmoja yeye ana mkewe walikuwa na watoto 3 wakike tupu. Sasa akaamua kwenda kuzaa nje kutafuta mtoto wa kiume alifanikiwa na kwenda kumtambulisha kwa ndugu kama wote mkewe aligombananae ila wakamwambia tuh huyu ni mtoto wake hata ukachukia haisaidii akakukubali.

Ndugu wa mwanaume wakamwambia kaka yao huyo ni mtoto wako mchukue ukae nae azoeane na wenzie. Yule kaka akamchukua akawa anaishi nae mkewe akanyamaza. Mawifi wakawa wanamsema tuu dada yule kuwa hamtaki mtoto wa mume wake.

Sasa mkewe nae akaamua kuzaa nje, yeye na mkewe ni weupe kwa hio watoto wote ni weupe mpaka wa mume wa nje.

Ila mkewe akachepuka na mwanaume mweusi, mtoto kazaliwa mweusi , mume eee.

Mkewe wake akamwambia huyu mtoto sio wako anaBaba yake.

Kwenye cheti cha kuzaliwa mama akaandika Baba yake halisi na sio mume wake. Yule kaka alilalamika sana kwao.

ILA baba yale alimwambia kuwa Hata wewe ulifanya hivyo hivyo kuwa mpole tuu najua unaumia kuwa mpole tu.

Dada zake walimtukuna sana yule dada. Ndoa ya kikristo. Wakawashauri tuu tulieni mlee watoto hao. Sasa hivi wote ni wakubwa kipindi cha likizo wa nje wote wanaenda kwa wazazi wao kuwasalimia likizo ikiisha wanarudi. Familia inawatoto 5 sasa.
Hii ni ya kwanza naiyona hapa wallah
 
Back
Top Bottom