Ushauri, niwahusishe watoto wangu wa nje ya ndoa kwenye urithi?

Kwa sababu mwanaume ndiye anahudumia familia. Ndiye anaesomesha watoto. Na kuprovide ila wavulana na wanawake wanalingana. Kama mumeo ni mvulana hili ni kosa kubwa sana. Ila kama ni mwanaume sio kosa ni bahati mbaya.
Sio kweli uhongo.
Kuzaa nje ni uhamuzi awe mke au mume. Sio bahati mbaya.
Kuchepuka ni maamuzi ya mke au mume mwenyewe na ni kosa kwa wote.
 
Kwa hio mke akiwa ana kazi yake aliyotafuta yeye mwenyewe na biashara zake alizoanzisha yeye mwenyewe.
Akizaa nje ni fresh kama mume???
 
Kwa hio mke akiwa ana kazi yake aliyotafuta yeye mwenyewe na biashara zake alizoanzisha yeye mwenyewe.
Akizaa nje ni fresh kama mume???
Ni sawa kama mume wake ni mvulana. Yaani kama mume wake hasimamiii vizuri majukumu kama mume. Kama mume wako ankupangia zamu ya kulipa ada au kodi. Anakupangia matumizi ya hela zako . Huyo mumeo ni mvulana alikuletea mtoto wa nje ni kosa. Ila kama hela yako unaitumia kwenye mambo ya kifamilia ukijisikia bila kupangiwa na mumeo. Na mumeo ana simamia almost 90 percent ya kila kitu. Basi jua mumeo alikuletea mtoto wa nje alikuwa ashakuandaa. Maana kumuacha utaishia kudanga maana ushazoea kuwa almost kila kitu anacover mumeo.
 
Sio kweli uhongo.
Kuzaa nje ni uhamuzi awe mke au mume. Sio bahati mbaya.
Kuchepuka ni maamuzi ya mke au mume mwenyewe na ni kosa kwa wote.
Haujanielewa tunaokojoa tumesimama tupo tofauti kuna wanaume na wavulana. Na kwenye maisha tuna main objective na sub objective. Hawa wavulana main objective ni kula wanawake wengi iwezekanavyo na kula Bata. Lakini wanaume wa kweli inakuwa kuprovide. Hakuna mwanaume asiyependa ngono. Lakini kuna wengine hii inakuwa ni starehe ya mara moja moja. Na kuna hawa wavulana ambao kila wiki anataka abadilishe mwanamke. Sasa kama umeolewa na mvulana shida ndo inakuja hapa.
 
Mvulana ni nani kwanza ?
Unajua maana yake??

Kutoka nje ya ndoa ni kosa hata kama mume ni tajiri na mke ni msikini , mume akitoka nje ya ndoa ni kosa na anahitaji kuomba msamaha kwa mke wake.

Ukienda basi hata kwenye mifano ya Bible mume akitoka nje ya ndoa.
Na kuwa na mtoto Mtoto huyo hata kuishi kwa Baba hakustaili na hata urithi kwa Baba yake.
Mfano mtoto ishumal mtoto wa Hajiri na Baba wa imani.
 
Kachemka, wakati akiwa mzima alitakiwa awajengee msingi hao watoto wake wa nje ili akifa warithi chao huko huku bila kuwaletea nongwa wale wa ndoa wala bila ya huyo mama kujua.

Hao watoto hawapati kitu hata akiandika Mirathi leo kuwamegea ngoma inaenda mahakamani hiyo na hawatapata hata mia mbovu huko kwa pilato.

Hii tunaiita "Tragedy of miscalculations" kitaalamu.
 
Mwanamke analipiza kwa kuzaa nje ya ndoa, halafu jamaa akaishia kulalamika tu basi?????

Ningekuwa mimi, huyo mwanamke angeenda kuishi n'a huyo aliyezaa naye !

Kuna vitu wanawake wanajisahau sana na kujifanya kushindana, tangu dunia iumbwe sijawahi kuona ndoa ya mitala inayohusisha mwanamke mmoja na wanaume 4, haipo! Lakini ndoa ya mwanaume mmoja wanawake 3,4 n.k ni kawaida kabisa!

Sasa ujasiri wa mwanamke kwenda kuzaa nje anautoa wapi????
 
Ndg usiamini sana in providing, hawana shukrani hao,utakuja uwaa au kujiiuwaa kama wenzio walio tangulia mbele ya haki kisa mapenzi! Waweza provide kwa asilimia mia na bado ukapigwa na kitu kizito kichwani na Wajanja wa Mujini!!
 
Kwahiyo jamaa yeye maisha yake hana V8
 
Baba yako alikua mtu wa msimamo,sio mtu anaogopa kumwambia mkeo kua na watoto wengine...mimi mke wng anajua watoto wng watatu ambao sio wke
 
Huyo ni mwanaume bwege....mimi napiga chini fasta
 
Sis pole sana dunia uwanja wa fujo,huyo kijanga kwasasa maisha yake yakoje,anafamilia?
 
Ndg usiamini sana in providing, hawana shukrani hao,utakuja uwaa au kujiiuwaa kama wenzio walio tangulia mbele ya haki kisa mapenzi! Waweza provide kwa asilimia mia na bado ukapigwa na kitu kizito kichwani na Wajanja wa Mujini!!
Ukipigwa na kitu unafukuza inavuta mwingine wapo kibao wanatafuta ndoa. Sio siri hauwezi kukosa mke. Na hata ukimletea watoto wa nje akikataa unafukuza. Hauwezi kukosa ukikaa na unafikiri sana utajipa stress utashindwa kutafuta hela.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…